Juzi, waziri wangu wa upigaji, sorry, wa njuluku na uchumaji uitwao uchumi, fedheha, sorry, fedheha alikuwa kwa Joji Kichaka nilikomtuma akakwapue njuluku ya mkopo akagomewa kwa sababu nazifuja. Zao au za mafyatu? Bila hili na lile niklsukuti nikafyatuka na kugundua njia rahisi ya kufyatua njuluku za mafyatu! Kwanini kutesa ubongo wangu wakati mafyatu wangu wasiofyatuka wapo? Nilijisemea. Niliamua kuwafyatua ili nipate njuluku za kuendekeza, sorry, kuendeleza makamuzi na matanuzi kama sina akili nzuri.
Inshu iko hivi. Nitabadili noti za Fyatuland na kutangaza tenda ya kufyatua mpya. Zilizopo hazikidhi viwango! Hivyo, nitachapisha mpya za viwango zitakazoitwa Fyatudafu. Hapa, najua fika. Yatajitokeza makampuni ya kimataifa tayari kupiga njuluku. Kabla ya kutoa tenda, lazima wanipe tenda ya kuwafyatua kahongo. Kumbe kuna mazabe na ufyatuaji vifyatuliwavyo vikaishia kuwa fursa! Nilipanga kuwafyatua wapigaji wa viwango visivyo viwango ila viwango vya kipigaji lakini nikasita vilipotokea kuwa fursa kwangu kuwafyatua mafyatu na kufyatua mshiko mrefu tena wa haraka kirahisi. Kweli, akili ni mali na uzwazwa ni mzigo! Mwenye akili Fyatuland hafi maskini wala kulala njaa.
Wasiojua madili yanavyofyatuliwa wanaweza kusema huu ni ubinafsi, ufisadi, ufisi, na uhujumu. Kwani, tunapoimba maadili hamjui tunamaanisha madili! Shauri yenu mtaliwa mwajiona. Hata hivyo, kwani kazi ya akili na unene ni nini hasa mafyatu wanapojigeuza nyumbu wakakataa kufyatuka na kufyatua tunaowafyatua? Nyumbu wana uzito mkubwa na wingi kuliko chui, fisi, na simba kwa pamoja. Hawafyatuliwi kila uchao wakishuhudia bila kulalamika? Sasa mimi ni simba na mafyatu ni nyumbu. Lazima niwafyatue na kuwanyumbua kama sina akili nzuri. Huu mwanzo tu. Nikishabadili noti, nitampa Bi Mkubwa wangu na kitegemezi chetu tenda ya kupiga njuluku zaidi. Nitabadili mitaala na kutoa kandarasi ya kutunga vitabu vya kiada. Hapa, ‘kushinda’ kuingiza vitabu kwenye mitaala ni njuluku siyo ujuzi mjue. Hakipiti kitabu hata kiwe kizuri namna gani bila kupitisha kitu kwa Bi Mkubwa na kitemezi chetu.
Zaidi, nitamwambia Bi Mkubwa amteue shoga yake Angel aunde kampuni ya kuchapa vibao vya barabara na mitaa ndo tufyatue tenda nyingine Fyatuland nzima maana, njuluku zipo bwerere tena nje nje. Ukiwa munene, kazi yako ni kusukuti na kufyatua sababu na visingiziio vya upigaji. Japo Bi Mkubwa hufyatua njuluku kwa madili haya, wakati mwingine hujiwa na huruma. Kuna siku alisema kuwa tunwafilisi mafyatu. Nilimshangaa sana na kuchukia nikatamani nimfyatue karata lakini nikaogopa atafichua siri zangu. Isitoshe, Mgosi Machungi anaweza kufyatuka na kubeba mzima mzima tukaanza kufyatuana wenyewe kwa wenyewe.
Kujitetea nilimfyatua kuwa tusipowafyatua nyumbu, wengine watawafyatua. Ilikuwa wakati nilipokuwa nikikopa njuluku toka benki ya gunia. Wasiwasi wa Bi Mkubwa ilikuwa kuwa nilikuwa nawatwisha mzigo vizazi vijavyo. Who cares kwani, nawajua? Deni nakopa na kutanua mimi na wenzangu. Walipaji ni wengine ambao hata hatujui walipo kwa sasa. Hapa, kosa la nani? Ulimwengu wa nyumbu ni kufyatuana. Asipowafyatua chui, atawafyatua fisi au simba au siyo?
Turejee kwenye dili lenyewe la kubadili noti za Fyatuland. Najua. Wapo viherehere watajifyatua na kutaka kuhoji. Nshaandaa majibu fyatuzi. Kama nilivyofyatuka hapo juu, wa kulaumiwa ni wawili yaani mafyatu waliogoma kufyatuka na kufyatua na idara ya viwango iliyojifyatua na kujiwekea viwango visivyo viwango iliyopiga dili la kwanza likazaa hili bab kubwa la pili. Mafyatu wanapojigeuza nyumbu mimi nifanya nini zaidi ya kufyatuka na kuwafyatua? Kama hawataki kufyatuliwa si wafyatuke nao wawafyatue wanaofyatua tena kizwazwa. Nisipowafyatua mimi, wale jamaa wa roho na uroho mtakakitu watawafyatua kwa kuwaita makondoo. Heri nyumbu yupo huru japo kidogo kuliko kondoo. Au niite Fyatuland Kichwachachiziland, Sheepland, au Fyatuliwaland kama siyo Zwazwaland?
Uzuri wa kufyatua nyumbu, sorry, mafyatu wa Fyatuland ni kwamba, hata kihiyo tena taahira, anaweza kuwafyatua wasifyatuke na kumfyatua. Ni rahisi sana kuwafyatua ilmradi ujue namna ya kuwapiga changa la mato kama hili la kubadilisha noti. Ukitaka kuwafyatua zaidi, waletee upuuzi kama vile ushabiki wa timu za futiboli la kigeni, michiriku, miziki ya ngoni, kukusifu, kujisifia ujuha na mengine mengi. Hakuna kitu kimenisaidia kuwafyatua mafyatu kama kuwaambia kuwa nataka watumie noti kama zile za Ulaya. We! Wasivyo nazo, kusikia hivi, si walianza kutunga mapambio, mashairi, ngojera, nyimbo, na mashairi kunisifu wasijue nawafyatua na kuwaona manyumbu.
Sasa nasikia muziki mzuri wa majisifu ambamo mafyatu wanasema Fyatuland itakuwa kama Ulaya. Mnaijua Ulaya au mnaota? Ulaya hakuna nyumbu bali mafyatu fyatuzi wafyatukao hata kwa kitu kidogo. Nadhani, kutokana na uzwazwa huu, nitakapokaribia kuachia ulaji lazima niwafyatue kwa kuwaletea mashine ya kuwabadilisha mafyatu wawe manyumbu wa kweli ili kiumane. Na hakika kitaumana.
Tuache mchezo. Kweli inaingia akilini kufyatua vitu visivyoingia akilini tukategemea mabadiliko na maendeleo au ni kujitoa ufahamu tukidhani ndiyo kufyatuka?
Chanzo: Mwananchi J'tano leo.

No comments:
Post a Comment