The Chant of Savant

Friday 3 August 2012

Je ni mwanzo wa mwisho wa ndoa ya Kagame na Marekani?

Chelsea Clinton, Bill Clinton and Paul Kagame
Hakuna ubishi kuwa taifa la Marekani limejenga uhusiano wake wa kimataifa kwenye kauli mbiu isemayo; Hatuna rafiki au adui wa kudumu ila maslahi ya kudumu. Kwa kuzingatia falsafa hii, kwa wanaoujua sura halisi ya taifa hili beberu duniani, hawakushangaa lilivyowageuka waingereza na kuchukua nafasi yao baada ya vita ya pili ya dunia. Pia hawakushangaa kuona taifa hili likiwageuka vibaraka wake kama vile Saddam Hussein, Osama bin Laden, Charles Taylor na sasa Paul Kagame wa Rwanda. Kulingana na habari zilizoandikwa na magazeti ya Uingereza ni kwamba kuna uwezekano wa Kagame kushitakiwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kule the Hague. Magazeti ya Uingereza yalikariri mamlaka za Marekani zikisema wazi kuwa Kagame anaweza kukabiliwa na kile alichokabiliwa nacho imla wa zamani wa Liberia Taylor ambaye alipatikana na hatia ya kusaidia wapiganaji wa Revolutionary United Front (RUF) cha gaidi Fodday Sankoh nchini Sierra Leone. Taylor alihukumiwa kwenda jela miaka 50. Kwa wanaoujua mchango wa Kagame kwenye kurejesha utangamano nchini mwake baada ya mauaji ya mbari ya mwaka 1994 na jinsi Jumuia ya Kimataifa ilivyoacha maelfu kwa maelfu ya watu wauawe, wanashangaa mwelekeo huu. Kagame amekuwa akituhumiwa kwa kuwasaidia waasiwa M23 nchini DRC tuhuma ambazo amekuwa akikanusha. Je Kagame anatendewa haki? Je huu ni unafiki na kigeugeu cha Marekani? Je hapa nani anamkomoa nani na kumhandaa nani ukiachia mbali kutoana kafara?Wadadisi wa mambo wanajiuliza, je huu ni mwanzo wa mwisho wa ndoa ya Kagame na Marekani? Kwa habari zaidi BONYEZA hapa na HAPA.

No comments: