The Chant of Savant

Friday 3 August 2012

Kufuru ya wenye pesa


Wakati mwingine neema huzaa makufuru. Watu wamechoka kuishi kwenye visiwa alivyoumba Mungu. Wameamua kutengenza vyao kama hicho hapo juu. Meli hiyo hapo juu ni kama kisiwa ikiwa na barabara, helipad au sehemu ya kuegesha helikopta beach na makandokando mengine ambayo mtu huyafaidi visiwani na kwenye miambao yake. Ama kweli wenye pesa wanajua kukufuru. Usishangae kugundua kuwa baadhi ya watu wanaofanya makufuru haya ni wale wale waliowaibia makapuku na kwenda kutumia kwenye upuuzi kama huu.

1 comment:

Anonymous said...

hiyo ndo kufuru ?
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la monduli Mh eDwaRD lowasa akikabisa sehemu ya tende kwa ma sheikh wa mji wa monduli kwa ajili ya FTARIII