Kuna vyombo vya habari vilivyozusha kuwa waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi amefariki. Ukweli ni kwamba huyu bwana hajafariki ingawa anaumwa na serikali yake inafanya siri ugonjwa na hali yake. Zenawi amejizolea sifa kwa mabaya na mazuri. Anasifika kwa kuubadilisha uchumi wa Ethiopia ingawa analaumiwa kwa ufisadi hasa kumruhusu mkewe Azeb Mesfin kuibia umma hadi akaitwa queen of mega yaani queen of mega-corruption au malkia wa ufisadi mkubwa. Pia Zenawi anashutumiwa kuwa imla anayependa sana madaraka. Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.
No comments:
Post a Comment