The Chant of Savant

Thursday 9 August 2012

Kikwete atajifunza na kuacha kuzurura lini?






Ingawa ni haki yake kwenda anapotaka kwa mujibu wa sheria, rais wa Tanzania Jakaya Kikwete hana huruma na walipa kodi wake. Pia hana muda wa kushughulikia masuala muhimu ya kitaifa zaidi ya kupenda kuzurura. Inafikia mahali watu wanajenga dhana kuwa anakwepa majukumu yake. Pia inaanza kujengeka dhana kuwa rais Kikwete haoni wala hana haja ya kuwa na makamu wa rais ambaye kisheria anapaswa kuwa msaidizi wake. Juzi alikuwa Kampala kuhudhuria mkutano wa wakuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki. Rais Mwai Kibaki mchumi asiyependa makuu alimtuma makamu wake, Stephen Kalonzo Musyoka. Kikwete alirejea jana na leo tunaambiwa yuko kiguu na njia na ujumbe wa maswahiba wake wasio hata na umuhimu katika ziara yake kuelekea Ghana eti kwa ajili ya mazishi ya rais wa nchi hiyo. Je kuzika ni bora kuliko masuala nyeti kama tishio la mgomo wa walimu au ule wa madaktari ambao bado unasuasua? Ni juzi juzi karejea toka Brazil kwenye mkutano ambao haukuwa na maana sana. Kama kawaida, Kibaki alimtuma waziri wake mkuu kumwakilisha. Kikwete, kama kawaida yake, aling'ang'ania yeye na mke wake kwenda kule kiasi cha kueleweka alikuwa akikwepa mgomo wa madaktari. Misiba imekuwa sehemu ya Kikwete kukimbilia majukumu na matatizo mazito. Walipoanza mgomo madaktari alitumia msiba wa msanii  wa filamu kujificha kabla ya kuondoka zake Brazil. Kesho likizuka tatizo jingine utamsikia huyo katimkia Afrika Kusini kujaribu kujadili tatizo la mpaka na Malawi. Kinachokera ni ile tabia ya Kikwete kuandamana na msafara mkubwa watu ambao hata si muhimu wala lazima. Kila siku ni kiguu na njia hadi watu wanamwita Vasco da Gama.
Je Kikwete ni mgumu wa kujifunza au ni kiburi na kupenda raha na kuzurura? Je atajifunza lini kuwa safari zake ni mzigo kwa taifa na chanzo kizuri cha utoro na matumizi mabaya yanayoongeza uzito kwa maisha ya malipa kodi maskini?

8 comments:

Anonymous said...

Hapa ni zeroo%
Kibaki tunamjuwa ni kiwete ataenda huko kufanya nini na wakati kalonzo yupo.Sasa unataka kusema kikwete akibakia hapa nyumbani ndo hiyo migomo haitokuwa ?
hii itakwisha 2015 habari za uchochezi

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Acheni ibada za sanamu hata kama mnananenepeshwa kwa mabaki ya ufisadi ya Kikwete. Huyu ni public figure isitoshe rais wetu lazima tumshauri hata kama nyemelezi wake inawauma. Siachi kumuandama ili siku moja yakimkuta anikumbuke wakati akiwalaumu nyinyi mliomuabudia hadi mkamsifu upuuzi na kumpotosha. This is my self-appointed prophecy. Sifichi sura wala jina langu hata JK na waramba viatu wake wananijua fika. Nyie mwalipwa kutetea upuuzi wakati mimi nimejitolea kupigania haki. Sina ninachokosa kama ndugu zenu. Sijui ukatikaji wa umeme wala mazabe mnayopambana nayo. Sina shida wala sababu ya kumchukia rais wenu. Sina personal vendetta naye zaidi ya uzalendo wangu.

Anonymous said...

wacha kujisifu Akujuwe nani wewe mtu mwenye sura mbili mara mie ni mcanada mara mie ni mtanzania.

mara umeandika:
rais wetu lazima tumshauri
mara umeandika:
Sina shida wala sababu ya kumchukia rais wenu.
sasa kama sio sura mbili nini
mara rais wenu mara rais wetu unafiki mkubwa

huwezi kupigania haki ya tanzania na wewe upo mbali halafu upiganiae haki ati mzalendo ? mzalendo pipa la taka
suti ya kukodisha

Jaribu said...

Sasa akiwa Mcanada au Mtanzania kuna tofauti gani? Jambo la msingi ni hoja inayozungumziwa. Kwa hiyo ukiwa nje ya Tanzania ndio huruhusiwi kumuuliza Dakta Mzururaji kuhusu huu ubadhirifu wa hela za umma kwa safari zisizoisha? Unafiki ni kutetea wizi na ujinga. Huko Ikulu kuna Idara Maalum ya kukusanya Obituaries kutoka kwenye magazati yote? Maana naona kila akikurupuka asubuhi swali ni, "Leo kuna mazishi wapi?" Angekua anafuata mpunga tungemhurumia, lakini rais mzima!

Anonymous said...

Jaribu
waramba matapishi hujuwi kuwa ukiwa mcanada na mtanzania kuwa kuna tafauti rudi shule
nyie wachochezi hamna lolote mnalofundisha humu ila uchochezi tuu jamii haipati faida yoyote
hii ndio katika blog zisizokuwa na maana hata kufungua lugha za kihuni huni tuu Bangi
Jambo gani la msingi lililoongewa? upuzi na taka taka za pua.
Mzalento na sio mzalendo Amkaaaaa

Jaribu said...

Sasa kama kuna tofauti mbona nyie na huyo rais mzururaji hamuishi kuvinjari na bakuli lake la kuomba omba, most of which inaishia kwenye mfuko wake na wapambe wake? Hela mnaiba kutoka popote duniani, lakini msiambiwe chochote kingine. Nani atakubali hilo dili?

Wewe humu unataka ufundishwe nini humu? Kama unataka ufundishwe kuwa Kikwete ni chaguo la Mungu inabidi ukanunue nakala yako ya Uhuru na Mzalendo. Hapa hamna mtakatifu. Tunaopitia humu tunaamini kuwa cheo ni dhamana, na haimaaanishi kujilundikia mali ya wewe na jamaa zako na safari zisizokuwa na tija.

Hiyo hoja ya uchochezi imepitwa na wakati. Makaburu wallitumia sasa hiyo kuwakandamiza watu weusi Afika Kusini na wakashindwa, sembuse nyie vilaza wa CCM. Watu tunachochea maendeleo, siyo wizi, rushwa na kutaka kuua madaktari.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Jaribu nakushukuru kwa majibu yako. Maana ningeendelea kumjibu huyu mtu mwoga anayeogopa hata kutaja identity yake ningeonekana najitetea. Acha ukweli ujisemee na hatutaacha kwa sababu yao. Historia ni shahidi kuwa Kikwete anakwenda kwenye vitabu ya historia kama rais wa hovyo aliyewahi kutawala Tanzania. He is but a political accident so to speak. Huyo anon anaonekana ni mtu anayehitaji shule sana. Ila ipo siku ataona ukweli pale hali itakapoanza kumgeuka. Hata wakati wa Mwinyi na Mkapa makapi kama haya yanayojipendekeza yalikuwapo. Kama anayenishutumu ni mtoto wa Kikwete sina ugomvi naye. Maana anatetea kitumbua cha baba yake ambacho ni chake.

Jaribu said...

Hamna tabu, Mhango. Wananikera majuha kwa kusema kuwa usipokuwa karibu ya Mabwepande hurusiwi kusema chochote kuhusu nchi yako. Nchi imewashinda sasa wanataka kuleta distractions. Ndio maana sikutaka kujibu hiyo hoja yake ys shule. Sasa nikirudhi shule huyo Professa ndio atakawa Dr Kikwete, kihiyo bar none?