Duranord Veillard (108) na Mkewe Jeanne Veillard, (105)
Ni wakazi wa Spring Valley New York licha ya kuwa na miaka mia na ushei wamedumu katika ndoa kwa jumla ya miaka 82. Je ni wangapi wanabahati kuishi miaka 82 ukiachia mbali kuishi katika ndoa kwa miaka hiyo? Nadhani kama kuna watu waliobarikiwa na ambao wanaweza kuonekana kama si wa kawaida si wengine bali Duranord na Jeanne. Tofauti na wenzao weupe wanaopelekwa kwenye majumba ya vikongwe na kufa huko kwa upweke, wanandoa hawa bado wanaishi na binti yao anayewatunza kama mila za kiafrika zilivyo. Wanandoa hawa waliobarikiwa walijaliwa kuwa na watoto watano. Baba alikuwa ni mtaalamu wa maabara hospitali. Kazi ya mama haikutajwa. Ila walihamia Marekani mwaka 1968. Pamoja na kutoona vizuri wawili hawa bado wanaweza kufanya utani na watu huku baba akiwa bado na uwezo wa kupiga push ups kila siku. Ni bahati mbaya hatukupata habari nyingi juu ya wawili hawa ambao ni katika wachache waliofanikiwa kuishi umri huu ukiachia mbali kuwa pamoja tena kwa miaka zaidi ya 80. Je ni bahati kiasi gani?
How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Sunday, 1 March 2015
Hawa ni katika wachache waliobarikiwa na kuwahi kuishi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment