The Chant of Savant

Monday 20 April 2020

NENDA NA UPEPO WA KISULISULI

R.I.P MCHUNGAJI DKT.GETRUDE RWAKATARE:SIKILIZA MANENO YAKE YA ...

Tangu uhuru wa kuabudu na kuanzisha dini utolewe, wengi walianzisha makanisa yao yawe ya kweli au ya uongo. Walifanya vituko. Na wanaendelea kufanya vituko. Hakuna aliyewahi kufanya hata nusu ya muujizi. Dunia itamkumbuka mmojawapo Getrude Rwakatare aliyesifika kwa kuwapatia wanawake waume wa kuwaoa japo yeye hakuwa ameolewa hasa ikizingatiwa kuwa mganga hajigangi na kinyozi hajinyoi. Sasa tumempoteza mwana mama machachari aliyefanikiwa kuwatuliza wengi huku akifanikiwa kuchanganya dini na siasa kwa kuwa mbunge na mchungaji wakati wananchi wanaaminishwa kuwa siasa na dini hazichanganywi.
Nenda Getrude Nenda na upepo wa kisulisuli.

No comments: