The Curse of Salvation

The Curse of Salvation

Friday, 14 February 2014

Cashgate: Joyce Banda crusader or pretender?

          Malawi’s cashgate is all over the place in the media. Cashegate is a mega theft of public funds involving millions of dollars ranging from $ 100 to 250 million.  Malawi’s president Joyce Banda’s nary lacked shockers. She recently came up with the purge on corruption in her country after the donor countries unearthed cashgate.  Banda told Malawians that she’s ready to even hit the road shall they deny her votes in the coming elections. Again, she boldly said that the job of stamping corruption out must be done and somebody’s to risk and do it. And she’s the one to do it no matter what. Despite her boldness and assurance, wary Malawians are asking: If she sincerely and seriously means business, why taking actions after donors unveiled the scam so as to refuse to release cash her cash-strapped government wants badly? They add. Why now when the country nears general elections? Does she want to get some of kind of mileage out of this war that she’s supposed to declare many months ago? Did she wait so that she could make some gains out this move against graft?
While questions are asked about the timing others are questing Banda’s "guiltlessness", seriousness and cleanliness as far as corruption is concerned. Detractors are asking: Is Banda clean or she is just whitewashing in order to get votes in the coming elections? Peter Chinoko, an outspoken head of the Catholic Commission for Justice and Peace in the Lilongwe archdiocese, has the answer as he’s recently quoted as saying: “We have concrete evidence about the president’s involvement and being part and parcel of the scandal.”  Interestingly, Banda did neither comment nor refute these damning allegations.
Apart from Chinoko, others are asking: What of her seven trips to Nigeria? Who footed the bills for her given that such trips are private ones? When Malawians wanted to know who Banda’s funder (s) was she squarely refused to divulge the person or persons who fund their president.
As for donors they categorically said, “We will not be able to resume support through government systems until we have a clear assurance, independently verified, that our resources are all being used for their intended purpose,” said Sarah Sanyahumbi, a British diplomat who heads the donor grouping, which includes European countries, the European Union and the World Bank. Britain has withheld £17 million of budget funds.
Detractors accusing Banda are not mincing words. They’re pointing fingers at her donors who happen to be the beneficiaries of the same monies Banda’s trying to retrieve. For example, a prominent business man Oswald Lutepo who also is a senior official in Banda’s party is said to have scooped over $ 6,000,000. Despite being accused, it came to light that Lutepo donated 22 vehicles to Banda’s party. This being the game-cum-situation many are questioning Banda’s cleanliness under such conflict of interests. Will she prosecute Lutepo according to the law despite charging him of theft and money laundering? Will partisan gimmicks come in and the case end up being sideshows?
Another suspicious character is Justice Minister Ralph Kasambara who is behind bars accused of ordering the shooting of one Paul Mphwiyo, Director of Budget who seems to have spilled the bins that lead to opening the floods gates Banda is facing currently.
Those of us who know where the heart of corruption in Africa is tend to suggest one remedy-declare your wealth and make it a national exercise for all citizens. One lifeline of corruption will be brought down. It is only in Africa where a person can acquire wealth or property just over night and nobody asks or task that person to divulge how she or he made such monies. This is why it is easy for many people to indulge in drug dealing, piracy, paid terrorism, corruption, robbery and whatnot. They know they’ll get away with it. It doesn't mean that our rulers don’t know it. They know it too well save that they don’t want to intervene for the fear of being forced by the diligent population to provide sound social services like in developed country. Instead they bless Mobutuism or Bongo-bongo whereby everybody plunders where she or he’s to survive without considering others who have no opportunity.  African proverb has it that a goat eats according the length of its rope. Call it a sin-by- all community whereby the bigwigs steal big sums while the small ones end up robbing whatever they put hands on and life goes on. If anything, pointless plundering and spending were what was going on in Malawi. For, it came to light that a mere junior public servant in the poorest country on earth’s found keeping over $ 300,000 in the boot of his car. Worse enough, most of those who stole the monies in question invested unwisely in posh cars, villas, and whatnot.
 If anything, corruption in many African countries is motivated by the lack of laws and political will forcing leaders and citizens to declare their wealth and file their tax return. How can prosecution work if at all there are some presidents who don’t even pay tax let alone to fail tax return or declare their wealth. 
Source: Business Time Feb. 14, 2014.

Thursday, 13 February 2014

Swali la leo: Iweje Faru na Tembo wauawe Bongo kampeni London?

Ivory destruction
Pesa ya wizi, ufisadi, rushwa, unga na ujangili wanaficha London.
Safari za kikazi wanafanya London.
Kampeni ya uzazi wa mpango London.
Mikutano ya uwazi London'
Kampeni ya kuangamiza ujangili London.
Je ni kwa nini au ni kwa vile hawa jamaa ndiyo waliotutawala?
Je ni roho kuwasuta wahusika ambao walirithi faru na tembo kibao toka kwa wakoloni?
Wakoloni walikuja wakatuibia lakini walikuwa na akili wakatubakishia.
Sisi tulipopata uhuru ambao umegeuka udhuru tumejitahidi kujiibia na kumaliza kana kwamba hakuna vizazi vijavyo. Sijui ndiyo huu uvivu wa kufikiri au kufikiri kivivu! Sijui ndiyo huko kuishiwa au sanaa za kuwaweka sawa wafadhili majangili ya ofisini na mbugani yakaendelea kupeta?
Nukuu ya leo ni toka kwa Mchungaji Peter Msigwa Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA).
Alikaririwa hivi karibuni akihoji,“Inakuwaje mtu anayevunja sheria za nchi hakamatwi. Waziri Nyalandu amekuwa mlalamikaji badala ya kutafuta suluhu, majibu yake na ya Serikali ya CCM yanadhihirisha kuwa mtandao huu unaogopwa unaihusisha Ikulu, wanasiasa, polisi, maofisa wanyamapori na wanajeshi.”

Wednesday, 12 February 2014

Vita ya CCM neema kwa watanzania

HAKUNA ubishi. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeingiliwa au tuseme kuvamiwa na kansa mbaya.
Hakuna kitu kinakitafuna chama hiki kama mdudu wa kupenda madaraka huku wanaoyatafuta wakiwatumia makada wa chama sehemu mbalimbali kuwapigia kampeni jambo linalosababisha migongano na hata malumbano yanayokiua chama taratibu.
Hali ni mbaya sana. Watu wamefikia kuvuana nguo hadharani kuhakikisha yule “wanayemtaka”, huku naye akiwataka na kuwatumia nao wakimtumikia anapita hata kama ni kwa watu wazima kufanya mambo ya kitoto kama kuvuana nguo hadharani.
Ni bahati mbaya kuwa CCM imeishiwa na kufilisika kiasi cha kutokuwa na kiongozi mwenye uthutubu wa kukaripia mitandao hii inayodhoofisha na kuua chama.
Asikudanganye mtu. Wote sasa ni sawa na kambale. Wana sharubu, tena ndefu sana. Mitandao ya kifisadi, kiulaji na kimaslahi imechukua nafasi ya chama kiasi cha kukiangamiza taratibu kama kansa inavyoonekana na kila mtu ana mtu wake na maslahi yake.
Hata Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete naye yumo kiasi cha kuhojiwa. Naye ana mtu wake anayeweza kulinda maslahi yake. Haya si maneno yangu. Rejea karipio la Malecela aliyekaririwa hivi karibuni akisema: “Kinachonishangaza ni ukimya wa viongozi wa juu wa chama, akiwemo Mwenyekiti wa chama wa taifa, Rais Kikwete. Naitaka Sekretarieti ya CCM kutafakari, kumjadili kwa kina na kumwajibisha Lowassa, ikiwezekana atimuliwe uanachama.”
Mtifuano wa Malecela na Mgeja unanikumbusha kisa cha ugomvi wa washirikina waliokuwa wakigombea kila mtu na kinyago chake ndicho kiabudiwe hadi wakataka kutoana roho ilhali vinyago vikiwa salama.
Mwisho wa yote, walipogundua kuwa vinyago vyao havina lolote wala maana, waliamua kuvichoma moto na kumtafuta Mungu wa kweli. Je, Malecela na Mgeja watafikia hatua ya kuachana na mitandao na maslahi binafsi na kukirejea chama?
Hata hivyo, mchezo huu unaoelekea kusababisha mauti ya CCM ni ukombozi kwa Watanzania kama wataweka kumbukumbu. Pia mchezo huu ni faida kwa wapinzani kama wataamua kuvalia njuga haya madudu yanayofichuliwa na makada wa CCM wenyewe. Hakika mitandao imetandawaza kila aina ya sababu ya kuanza kuiaga CCM taratibu.
Leo hii ni zamu ya makada, Hamis Mgeja, Mwenyekiti wa CCM wa Shinyanga na Makamu Mwenyekiti wa CCM mstaafu na Waziri Mkuu wa zamani, John Malecela. Baada ya Malecela kuita waandishi wa habari hivi karibuni na kukaripia tabia ya baadhi ya wana-CCM kuanza kutangaza kugombea urais hata kabla ya muda, amejichongea.
Malecela katika mkutano wake na waandishi wa habari alimtaja Edward Lowassa, mbunge wa Monduli na waziri mkuu aliyetimuliwa kutokana na kashfa ya Richmond wazi wazi kuwa hafai kuwa rais.
Siku mbili baadaye, Mgeja aliamua kumtolea uvivu Malecela jambo ambalo limetufanya kuuliza kulikoni Mgeja kumsemea Lowassa kana kwamba yeye ndiye wakili wake? Je, ametumwa au amejituma? Je, ana nini cha mno na Lowassa au ndiyo huku kutumiwa na kutumiana?
Mgeja alikaririwa akisema: “Huyu Malecela amesahau huko nyuma yeye alishawahi kutuhumiwa kuwa alipewa fedha kutoka nchi za Uarabuni na mpaka kubadilisha dini na kuitwa Jumanne ili aungwe mkono kupewa nguvu za kugombea urais.”
Laillah ila allah! Hatukuyajua haya na kama ni ya kweli basi kuna namna. Je, inakuwaje kwa Mgeja Muislamu aone kitendo cha Malecela kusilimu kama kitu kibaya kama hakuna namna? Pia Mgeja alisema kuwa Malecela alikataliwa na baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere hadi kumtungia kitabu.
Ajabu Mgeja huyo huyo sijui kwa kusahau kwa kutojua kuwa alitumia mfano mbovu, alisahau kueleza kuwa hata huyo Lowassa alikatiliwa na Nyerere huyo huyo.
CCM imeoza kwa rushwa jambo ambalo kumbe wananchi hawakujua. Kwani Mgeja aliongeza: “Malecela, Makonda na washirika wenzao wanajua kuwa wako baadhi ya wanachama wanagawa kalenda nchi nzima, wanagawa simu huku wakitumia magari ya serikali kugawa hizo takrima na inawezekana na wao pia walishawahi kuzipokea na wana-CCM wengi walishazipokea, hata mimi nilishapokea, mbona hizo hawasemi, nazo zinakivuruga chama?”
Je, hapa kinachogomba baina ya Mgeja na Malecela ni uchungu kwa chama au uchungu kwa mitandao? Je, Malecela ni kama Yusuf Makamba aliyeonyesha wazi wazi anamtetea na kumuunga mkono Lowassa? Wapo wanaosema kuwa anatumiwa.
Ni aibu kiasi gani kwa makada wa chama kuanza kuhongana na kutumiana kama nepi? Je, chama cha namna hii chenye uoza kuanzia kichwani hadi miguuni bado kina udhu na hadhi ya kuongoza taifa linalohitaji mkombozi toka kwenye rushwa ufisadi na majanga mengine ambayo CCM imeyasimamia na kuyatekeleza siku zote? Je, wananchi wanajifunza nini kutokana na vita hii ya mitandao maslahi?
Rushwa kwa sasa inatembezwa wazi wazi na waasisi madaraka wa ndani ya CCM. Watu wanauliza haya mabilioni yanayomwagwa yananunua nini na wahusika waliyapata wapi? CCM inanuka rushwa kiasi cha kutisha.
Rejea karipio la Malecela aliyekaririwa akisema: “Naomba niseme kuwa bila karipio au tamko la chama, hawa wanaotumia fedha hadharani kwa lengo la kutafuta umaarufu na ushawishi kwa vijana ili kupata madaraka, wataharibu misingi bora ya uongozi iliyowekwa na waasisi wetu ndani ya chama.” Kwa rushwa kama hii ya wazi wazi kumebaki kitu cha kuweza kuweka madarakani?
Watanzania wakifanya kosa wakarudia makosa kwa kuchagua chama fisadi na kinachoongoza katika rushwa wasijute wala kumlaumu mtu. Hawa watu wapo kwa maslahi yao fichi na si ya Watanzania. Laiti Watanzania wangewabana hawa watoa rushwa wakaeleza walikopata hizo pesa na wanataka kununua nini!
Tumalizie kwa nukuu ya Paul Makonda, Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi, aliyekaririwa akisema: “Lowassa amekuwa akiwatumia watu kusema ovyo, kwanza mwenyewe hana sifa ya kuwa rais wala kuwa amiri jeshi mkuu wa nchi, na kama wapo vijana hapa mjini wanaotaka fedha kwa haraka wamtafute.”
Kwa halli hii, Watanzania waliokuwa wemelewa mapenzi na imani kwa CCM wamejikuta mbele ya kinyago cha mpapure walichodhania ni Mungu. Kazi kwao. Wazee wazima wanafanya kile Waingereza huita, washing your linens in the agora.
Ukifikia hapo umeisha na kuishiwa. Watanzania wanapaswa kuifungisha virago CCM ili wenye uwezo waingie na kutawala. Hakuna tena sababu ya kuendelea kuiamini CCM isiyojiamini wala kuaminika.
Chanzo: Tanzania Daima Feb., 2014.

Kijiwe chafaidi mipasho ya CcM

    John Malecela







BAADA ya kulishughulikia li-Rweyependekezamu, tulisikia eti lililalamika na kulaani sana likitishia eti kumuona Mkamiawaandishi wahujumu gazeti. Hilo limeishiwa tu. Baada ya Chama cha Mipasho (CcM) kuamua kutoa burudani ya bure, kijiwe kimeamua kukaa na kutafakari na kufanyia uchambuzi hatua hii ya kupigiwa mfano na kushangiliwa, hasa na wale waliokuwa wakitatizwa na kitu hii.
Yote haya yalianzishwa na Mpemba ambaye inaonekana ni mfuatiliaji mzuri na mpenzi wa mipasho ya walevi hawa wa madaraka.
Anaingia akiwa na gazeti la Danganyika Leo. Anaamkua na kuagiza kahawa huku akiwa anatembeza uso wake kuzunguka kijiwe kizima kuona watu wanajisikiaje.
Anasema: “Mwafahamu kuwa kuna kijana aitwaye Maakondaa kwenye chama cha mafisadi aliyekonda kuona wazee wote wa chama yake wanatumiwa kiasi cha kutoamini kama hiki ni kitu cha kufumbia macho? Hivo, bwana ndogo aliamua kupayuka kiasi cha kuwakwaza wakongwe. Nanhusudu huyu kijana walllahi.”
Mbwa Mwitu anaamua kumtania Mpemba akisema: “Shehe unhusudu huyu dogo ili umfanzeni?”
Mpemba hajali. Badala ya kumjibu Mbwa Mwitu anamgeukia Mchunguliaji aliyekuwa akimezea gazeti na kusema: “Najua wapenda sana habari na magazeti weye. Basi tukua utusomee ili hata hawa wanolote utani kwenye mambo yaso ya utani wafahamu kinioendelea.” Anampa gazeti huku akimuonyesha pa kusoma.
Mchunguliaji naye anachukua gazeti na kuanza kusema: “Hebu sikia dogo alivyozoza. Haya si maneno yangu.”
Anasoma gazeti linalosema: “Lowa-sir sasa amekuwa akiwatumia watu kusema ovyo, kwanza mwenyewe hana sifa ya kuwa rais wala kuwa amiri jeshi mkuu wa nchi, na kama wapo vijana hapa mjini wanaotaka fedha kwa haraka wamtafute.”
Mijjinga anaonyesha mshangao. “Kumbe fisadi huyu ni kitega uchumi cha wachumia tumbo siyo!”
Kapende anajibu: “Ulikuwa hujui? Hukusikia Maakondaa akisema kuwa kama unataka ulaji wa dezo nenda kwa Lowa-Sir?  Hukumsikia mgosi akiapa kufanya lolote kuhakikisha anamtetea na kumlinda fisadi huyu Ewassa? Sijui amemfanya nini yarabi hadi anapagawa hivyo baba zima!”
Mgosi Machungi anakwanyua mic haraka na kujihami. “Niombe msamaha haaka kabla sijapiga mtu zongo. Siwezi kujizaiisha kwa vijipesha kidogo isitoshe kwa mtu anayetumiwa na hao waiomnunua kuja kuwanunua Wadanganyika wenye uchu. Jamani tiwe makini tinapoongeea haya mambo. Mimi si wa kujiuza kwa Owassa.”
Kapende hakawii. Anamnyang’anya mic Mgosi na kudema: “Mgosi nawe una papara. Kwani mgosi ni wewe pekee duniani? Namaanisha mgosi Joseph Makambaa si Machungi.”
“Hapo time understand. Maana tiishangaa kuona tinahusishwa na fisadi wakati sisi tinapambana na ufisi na ufisadi,” anajibu Mgosi Machungi huku akitabasamu kuonyesha kuridhika na majibu ya Kapende.
Mpemba anaingilia: “Nyie mwashangaa haya! Sie tushazoea hasa wakati wa yule kamandoo uchwara Salimuni Amri ambaye sasa ashasalimu amri. Walitokea hata magabacholi wakamramba viatu hadi wakawa matajiri. Alipotimka sasa mwawasikia hawana ladha tena. Wahaha kama mbwa koko.”
Kanji kaudhika kusikia neno gabacholi. Anakatua mic: “Choli iko mizi hapana ita dugu yako choli bwana. Sisi sote dugu.”
Kapende anachukua gazeti toka kwa Mchunguliaji na kunukuu maneno ya Malisera akisema: “Kinachonishangaza ni ukimya wa viongozi wa juu wa chama, akiwemo Mwenyekiti wa chama wa kaya, Rahisi Kikwe… Naitaka sekretarieti ya chama kutafakari, kumjadili kwa kina na kumwajibisha Ewassa, ikiwezekana atimuliwe uanachama.”
Msomi anakwanyua mic na kuzoza: “Anashagaa nini iwapo lao moja? Hakuna aliyeniacha hoi kama yule habithi toka usukumani aitwaye Mjega ambaye alisema kuwa agwe alikataliwa na Mchonga asijue hata huyo bwani wake Lowa-Sir alikataliwa pale aliposhindwa kueleza alivyopata huo ukwasi ambao sasa anawahongea hata wanaume wazima wakajidhalilisha.”
Mipawa anakwanyua mic: “Usinikumbushage Mchonga alipowakataa Ewassa na Kikwekwe wake kiasi cha kuokoa kaya asijue watarudi na kuizamishaga.”
Mijjinga aliyekuwa anabofya ki-ipad chake anadandia mic na kuzoza: “Huyu Mjega namfahamu sana. Ni mtu mzima hovyo ambaye anajigejuza a barking dog that does not bite.”
Msomi anampa tafu kwa kuzoza ukameruni kwa kusema: “They guy is but a lapdog that can’t become a watchdog.  Muhimu ni kwa wapinzani kutumia mwanya huu. Maana underdog can become top dog. Au vipi?”
“Waheshimiwa mlivyoamua kutuadhibu kwa ukameruni wenu sina hamu. Mmekuwa kama jamaa zetu waishiwa wa mjengoni wanaopenda kuchanganya Kiswahili na kikameruni!” Analalamika mzee Maneno.
“Samahani mzee mwenzangu. Nilichotaka kuonyesha ni uhovyo wa huyu Mjinga sijui Mjega sijui nini. Ukisikia kutumia, kutumiwa na kutumiana ndiyo huku. Hamkumsikia mgosi Makambale akiapa kwa miungu yote kuwa atakufa na Ewassa as long as naye anamkatia ili afaidi?”
Mbwa Mwitu anachomekea: “Urahisi si mchezo ndugu zanguni. Mtu anakula kuvaa na kutanua bure ndani na nje ya kaya.”
“Rais iko zuri sana. Kama nakuwa rais iko kula kunya, sorry, kunywa bure hadi toto na bibi yake. Mungu akupe nini dugu yangu?”
Machungi huku akiwa ameinamisha kichwa anasema kwa kunyong’onyea: “Imitisikitisha sana kuona mgosi mzima anajizaiisha kwa mwanaume mwenzake. Sisi kue Ushoto tishakubaiana akikanyaga tinamtia adabu kwei kwei sitanii.”
Bi Sofi aka Kanungaembe ambaye alikuwa kimya muda mrefu naye anaamua kukatua mic: “Mimi sioni ubaya watu kupashana kama wanalo la kupashana. Nadhani wale ambao si wanachama wangeachana na mambo ya chama na kushika yao.” Anamalizia akiwa amemkazia macho Kapende.
Kapende hangoji. “Haya si mambo ya chama bali kaya. Tuwapige chini ili wakapashane vizuri.”
Mpemba anakubaliana na Kapende. “Hawa kama siyo kusaidiwa na uchakachuaji, tungekuwa tushawasahau zamani wallahi. Maana walivoishiwa na kutifuana nadhani kila mtu aone ubovu wao.”
“Heri Mpemba umesema. Pia ongezea kuwa kama si njaa za wachovu na wendawazimu wao wa kupwakia takrima tungekuwa tushaanza kuonja matunda ya ukombozi. Hukumsikia baba yao Pio Msekua akisema kuwa wapingaji wakijiandaa vilivyo wakaungana wanaondoa manyang’au haya once and for all?” Anadakia Msomi.
Anakatua kashata na kuendelea: “Mie naona tatizo hapa si chama wala wakubwa zake wanovuana nguo hadharani. Hapa tatizo wachovu wenyewe kushindwa kutimua hichi chama kilichogeuka zigo tena la kunuka.”
Kijiwe kikiwa ndiyo kinanoga si likapita shumbwengu la Lowa-Sir akiwamo anamnong’oneza mgosi Makambaaa. Tuliwazomea na kulimwagia kahawa na kila mtu kutimka kivyake.
Chanzo: Tanzania Daima Feb., 12, 2014.

Monday, 10 February 2014

Mkiti wa CCM kizimbani kwa kuuza dawa feki

Mkurugenzi wa mashtaka Jinai (DPP) ameamuru mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa mkoa wa Dar Es Salaam, Ramadhani Madabida (Pichani) wa kwanza kushoto kufunguliwa mashtaka matano mojawapo likiwa ni kusambaza madawa feki yenye thamani ya mamilioni ya kurefusha maisha kwa waathirika wa ukimwi.
Hatutajadili kesi iliyoko mahakamani. Hata hivyo ukiangalia mrorongo mzima wa kesi na visa vya Madabida kujihusisha na uuzaji na usambazaji madawa feki havikuanza jana.Hapa unaweza kuona uovu na roho mbaya vinavyotawala Tanzania. Zamani wakati wa awamu ya kwanza mtu mwenye kutia shaka kama huyu asingeweza kuchaguliwa kiongozi hata wa shina. Ukisikia mfumo wa kifisadi ndiyo huu. Mke wa mtuhumiwa huyu ni mbunge ambaye bila shaka anatumia ubunge wake kutafuta dili kwa ajili ya madawa feki. Na hii si mara ya kwanza kwa Madabida kukumbwa na kashfa ya kuuza madawa feki. Mara ya kwanza alituhumiwa na mambo yakaisha kimya kimya. Huyu ibn muthnaq Madabida simtofautishi na habithi Ditopile Mzuzuri. Bila shaka naye atakufa mapema kama ilivyotokea baada ya Mzuzuri kuua na kulindwa na jamaa yake Kikwete asijue Mungu hana rushwa wala kujuana. Maana ukiangalia umati wa waathirika anaowaibia na kuwaua unashindwa kuelewa hata kilichowapa ujasiri CCM kuendelea kumbakiza kwenye wenyekiti.

Sunday, 9 February 2014

Robin Hood vs Hooded Robbers

Legendary English archer-cum-swordsman, Robin Hood and his merry men stole the show in Nottinghamshire before getting global notoriety. No literature tells exactly when Hood or Hudgin in Germany was born. What is clear is that Hood was a good man who aspired to form an egalitarian society based on justice and respect.  Ironically, he wanted this to be achieved through crime. An outlaw as he then was, Hood was renowned for robbing British plutocrats and offering his loots to the needy and paupers.  He did a good thing in bad way just like those who do bad things in a good way. Hood wore his heart on his sleeve when it comes to what he used to do. 
Hood didn't’t hide his true colour. By the way, Hood was a bibber like us. He loved kanywaji and justice. He hated corruption, greed and hypocrisy. This is why he didn't dispute the fact that he was a robber.  Again, he was a good robber who shared the loots with paupers. He risked to be jailed even killed for the sake of unprivileged. This is totally different from what we experience in the modern world whereby a cabal of people uses their power to rob those who voted for them. I like to call such venal creatures Hooded Robbers.  Our robbers, don’t admit their being robbers. So too, they don’t share their loots with the paupers. Instead, they just rob the paupers and stash money in the offshore-banks.
Whether Hood’s name came from the hood, he is likely to have been used to disguise himself or not, I won’t concentrate on that. Instead, I’ll concentrate on the modern hood of power and political positions our Hooded Robbers use to destroy our lives. What’s more, our greedy beings can be called economic hoons. They always drive at high and suicidal speed when they sense that there is money to be robbed. They don’t drive on the road you know. Nay! They drive in politics so that they can be entrusted the offices to rob.
 Robin Hood is a satire to our modern-time Hooded Robbers. Don’t tell me that you don’t know them. You know them. Maybe you’re one of them if not them. To get it, try to ask yourself how many fat thugs in power you know? Of course, you know countless. Don’t start saying hootis! You know what I mean. Don’t ask me where they live. So too, you know where they live. Don’t ask me where they stash their loots. You as well know that it is either in Swiss Banks or somewhere else from Jersey Island to the Island of Man, Cayman you name it. Call them hounds especially for those who invest in robbing us under many good names such as development partners, investors, shakers and movers. If anything, ours are but rabid dogs that need to be hanged whenever seen or discovered.
In case you've not gotten it, if you want to have a clear look into our Hooded Robbers, I’ll give you some qualities they posses as opposed to Robin Hood. Robin Hood hard a lion heart. They have rat heart so faint and dubious that they rob even unborn creatures. They sell everybody sometimes including themselves. They are more of psychopaths than normal human beings you've ever known. We need to decloth them in every manner. How can we stop declothing them if at all they don’t measure up to what they preach? They preach water and drink wine-super hypocrisy. People must be tired of hoo-ha offered by con men and women they think are their emancipators while they actually are their tormentors and prosecutors. They’d make them to pay whenever they rob them.  There must araise modern Robin Hood in politics, human rights, administration and what not. When these Robin Hood serve boozers must not expect to be recompensed when they take the role of emancipating the boozers. 
While Robin Hood did not feel guilty of what he was doing due to his good intentions, our Hooded Robbers feel no guilty for their dirty deeds. They don’t just because they’re strong at heart. Nay! They are faint hearted and blind to the extent that they can’t think beyond their noses. They are bêtes noix who use their stomachs to think instead of heads. Again, they still try to show their cockiness while they actually are sitting ducks if not lame duck who knows corruption in the place of accountability and delivery.
Source: ThisDay Feb., 10, 2014.

Saturday, 8 February 2014

Huyu soja vipi jamanini?

Kuna utendaji, uwajibikaji na uadilifu hapa? Kweli kuna usoja mle au kiriba tumbo na magonjwa ya kila aina kuanzia ya kitabia hata ya kibaolojia. Je nchi zenye masoja kama hawa zimo kwenye hatari kubwa kiasi gani? Hilo wowowo ndiyo usiseme. Ikija kwenye friji wow! Only God knows! Ngai Muthamaki tuhonokye! Mnakumbuka jinsi masoja wa Kenya walivyokwenda kwenye Westgate or Wastegate mall kujiibia kila walichoweza huku wakisahau wajibu wao? Je Bongo mnao maafande wangapi mafisi na mafisadi wakubwa kiasi cha kuwalinda na kuwaengaenga mafisadi wakuu? Msijali. Nilikuwa nawaza tu baada ya kuona picha nzuri ya kupendeza kama hii. Tafakarini hata hivyo.

Mlevi aonya walevi wa politiki


Baada ya mlevi kushuhudia na hata kusikia walevi wa politiki wakivuana nguo hadharani, ameamua kutoa somo ili kuonyesha tofauti kati ya walevi wa kanywaji na walevi wa politiki.
Ninafanya hivi kuepuka aibu inayotokana na mchezo huu mchafu wa mitandao ya kilevi ya kuhujumiana, kuumbuana, kutukanana hata kupakaziana ingawa mengi yanayosemwa na hawa walevi wa politiki yana ukweli.
Ila kwa vile mie si mlevi wa politiki yao nawaachia wenyewe sawa na aibu yao.
Bila kurudia mauzauza na mfukunyuku, kasheshe, mshike mshike kindaki ndani na ulimpyoto walivyoshuhudia wale wa taputapu baada ya walevi wa politiki kustukiana kuzidiana kete kwenye mchezo wa kuwanyonya walevi, napenda kusema wazi kwa niaba ya walevi kuwa sisi walevi wa kanywaji huwa hatuna upogo ufyole na ulimpyoto wa kuvuana nguo hadharani japo huwa tuna sifa ya kutoboa siri bila kificha na kutomuogopa mtu.
Hata hivyo, huwa tunafanya kweli panapo ukweli na haki na si kutafuta ulaji wa dezo kama wale.
Hivyo, leo nitaonyesha tofauti baina ya makundi haya mawili ili wasomaji na wachovu wajue.
Hii itaepusha dharau na kinyaa na kuepuka kuanza kutuona sisi walevi wa kanywaji hovyo sawa na wale mapolitiki.
Ulevi wa mataputapu una hatari zake kama vile kuangusha gari mitaani kiasi cha wahuni kutaka kukufanyia vitu vibaya ukiachia mbali kukamatwa na ndata mara kwa mara wanaotaka kukutoa kitu kidogo na kikubwa kutokana na njaa na ufisi na ufisadi wao.
Unaangusha gari na kupona wakati mwingine kuokotwa na wapita njia na mambo yanaishia pale.
Ukitoka pale unakwenda kuwekwa kiti moto na mamsap akidai ni kwanini unamuaibisha hivyo.
Unapiga magoti na kumshika miguu na kuomba msamaha ukiapa kwa miungu yote kuwa hutarudia kumuangusha na mambo yanaisha.
Bi mkubwa kwa vile ameishakuzoea, anasamehe yanaisha na kungoja zali jingine.
Zifuatazo ndizo tofauti baina ya walevi wa kanywaji na wale wa politiki.
Mosi, wakati walevi wa kanywaji huangusha gari yaani miili yao, tatizo la walevi wa politiki  ni kuangusha kaya nzima kiasi cha kuruhusu wezi wa kila aina waitwao wawekezaji kuja kuharibu na kuhatarisha maisha ya walevi wote na vizazi vijavyo hasa kwa kutumia kufisidi hata kuiba na kula bila kunawa.
Pili, sisi walevi wa mataputapu si wezi wala majambazi kwa kiwango cha haya ya politiki.
Tatu, sisi hujiibia vidani na vipesa vya akiba vya wake zetu. Ikizidi sana huiba vifaranga ili kuuza na kupata lau mnuso.
Nne, walevi wa kanywaji wakiiba vitu vidogo vidogo kama vile vidani vya wake zao, wale wa politiki huiba madini hata majumba na ardhi.
Mara hii mmewasahau walevi wa politiki walioiba nyumba za walevi wakagawana na kudai watajenga nyingine! 
Uliza hizo zilizojengwa ziko wapi na kama zilijengwa ziligharimu kiasi gani cha walevi?
Tano, wakati sisi tukiiba vifaraga tena vyetu vyenyewe, walevi wa politiki huiba wanyama mbugani kwa njia ya ujangili na wakati mwingine huuza hata wakiwa hai.
Mara hii mmesahau jinsi majambazi haya manono yalivyoiba wanyama wenu yakanajisi hata uwanja wenu wa ndege kwa kupitisha wanyama hai kwenda Umangani!
Nani anaongelea huu ujangili tena? Nani anayakamata haya majangili yaliyoshirikiana na jangili la kigabacholi yakavusha wanyama hai kupitia Kia? Sisi hujiibia vijisenti tena vya ugoro.
Yenyewe yanaiba kuanzia EPA hadi Richmonduli na kuendelea kujikausha kana kwamba hayajulikani wala hayahusiki.
Sita, sisi hujivutia bangi na kunusa bwimbwi kidogo wakati yenyewe yakiingiza na kutoa tani za madawa hayo tena wakijenga mijumba ya bei mbaya na wengine kutumia uchache utokanao na bwimbwi kuingia kwenye siasa ili wafanye zaidi.

Kwani hamjui siri ya kushindikana kuwakamata wauza bwibwi? Nani amkamate nani iwapo kambale wote wana sharubu?
Saba, sisi hatuwauzi wake wala watoto wetu tofauti na wao. Je! walevi wa politiki wanafanya nini? Wanawauza walevi mchana kweupe tena wakiwahadaa kuwa hayo ndiyo ‘better life for all while it actually is worst life of all’.
Tena wanauza hata vizazi vijavyo kwa ‘just ten percent of’ rushwa.
Nane, sisi walevi wa mataputapu hupenda mapupu na utumbo na finyango kidogo.
Walevi wa politiki hupenda salala ukiachia mbali kupenda mashangingi ya kibongo na ya Kijep ya Ujapani.
Hamkuwasikia mjengoni wakizodoana kuwa kila mtu ana chakula pale? Hamjaona vimwana wanaoibuka ‘from the blue’ na huishiwa na ‘Foundations’ za uongo na ukweli?
Kama bi Mkubwa wa WaMa anakula kwa njia hiyo, kwanini wadogo zake nao wasifaidi?
Wenzetu kwa kulewa politiki na mashangingi sina mfano! Hamkuona juzi mashangingi ya kisanii yakijiweka karibu na wao ili nayo yafaidi ulaji wa kishangingi na kishankupe wa kula bila kunawa kwa mikono miguu na hata mikia?
Hamkuyaona mashumbwengu, machangudoa, machangupaka na machanguchangu chakachua cha wenzangu ya kike na kiume yakijiweka karibu na mibaka na walevi wa kipolitiki ili yatufaidi?
Tisa, sisi walevi wa mataputapu tunajivunia elimu yetu ya kupayuka. Waulize wale wa politiki wanajivunia nini zaidi ya kuibaka hiyo elimu na kuiharibu kiasi cha kukosa maana?
Shukuruni Kawa-dog upo hapo? ‘Thank Lord’ mshirika wako Phil Muongo Mulugoo goo goo ame-go.
Atokomee mwana kutokomea. Nawe mshukuru mshikaji wako ambaye ameamua kutumia uswahiba wenu kuua elimu kama alivyowahi kusema Dokta Silaha.
Hata hivyo, mnajali nini na mnaogopa hasara gani iwapo viegemezi vyenu vinasoma ughaibuni na vingine hata kughushi huko?
Siku hizi kughushi ni dili. Faza na Maza wanaghushi hata watoto na wajukuu na vitukuu.
Kweli mbigiri huzaa mbigiri na mafisadi huzaa mafisi na mafisadi!
Acha niwahi kwenda kuwasuluhisha Malisera, Makambaaa, Makondaa Mshindwayi na Mjega wanaovuana nguo wakigombea maslahi uchwara ya mitandao ya ulaji wa dezo ya urahisi.
Naenda kuwapa ‘fwact’ kuwa wakiendelea kuvuana nguo kwa maneno tutawavua nguo kimakwelini na kitakachowakuta wasitulaumu.

Wajua nini kitawatokea? Si umma utawaona kuwasanifu na kuwacheka!
Chanzo: Nipashe Jumamosi Feb., 8, 2014.

Friday, 7 February 2014

THE POWER OF BEDROOMS IN POLITICS

Remember Professor Laurent Gbagbo former president of Ivory Coast currently caged in The Hague?  What of his wife Dr. Simone Ehivet Gbagbo?  The Gbagbos painted a grim picture as far as African elites are concerned. Gbagbo, the professor of History, made a bad history for not understanding history.  He mindlessly clung unto power so as to cause many deaths and many casualties.
Gbagbo’s saga is a test to our educational integrity and worth for us as a society. Many’d think.  Such highly educated person’d know basic things such as Human Rights, freedom and rule of law so as to uphold democracy especially elections. But nay, the guy thought though wrongly he’s but a king.
After Gbagbo’s unceremoniously dragooned out it came to light that his wife, Dr Simone, also the historian, harshly and greedily used him to tighten his grip on power and terrorize the country by ignoring all rules in the book.  
In this dirty business of dirty politics Gbagbo’s not alone. Who knew that a professor of law like Abdulaye Wade (Senegal) would tamper the constitution and extend his term in office on top of grooming his son, Karim, to inherit his presidency?  
Who’d risk thinking that a hyper academician like Robert Mugabe’d mess the way he’s always been doing by being hoodwinked by an illiterate like his wife, Grace Marufu so as to abuse the powers vested on him?
The sage’s it that when you want to tame a bull you’d know where its strength and weakness lie. For African big men their strength-cum-weakness is in the bedroom. So who occupies and controls their bedrooms control everything including them and their powers.  
    This can be seen in, among others, Simone, former political activist, was able to make or affect whatever decision Gbagbo made. She’s like president especially acting as an adviser to the president. Many who know her believe: Gbagbo’s decision not to cede power to a constitutionally elected president, Alasane Ouattara’s the result of Simone’s advice.
    When the world found that Gbagbo’d lost his sense of reasoning, it intervened to see to it that he’s booted out.  Interestingly, UN and Ivorian former colonial master, France, took a lead in getting rid of the tyrant.
The Gbagbos were humiliatingly bundled before the media after being dug out of the bunker in which they spent over two weeks hiding. Indeed, Gbagbo once again, proved the sage that education sometimes doesn’t emancipate the bearer if he’s unable to read the signs of times. So too, was his educated son, Michel, who’s severely beaten before the TV cameras. It’s a shame of its own magnitude for the former president and his family to be treated just like common criminals. All this happened just recently. But did our venal rulers make any note of it?
Today’s analysis is based on hidden presidents namely the first ladies and members of the families of the presidents. Simone’s described by many media outlets as the lady that’s feared more than the president himself. Moreover, she’s implicated in many scandals among which’s the disappearance of her husband’s rivals prominent one being French-Canadian journalist Guy-André Kieffer. Kieffer’s believed to have been hijacked under the instructions of Simone in 2004. Since then Kieffer’s nary been seen anywhere.  
What’s unveiled in Ivory Coast’s just a typical replica of what’s, for long, been going on in many African countries as far as power greed is concerned. It is more a tip of iceberg. Sadly though, when all this sacrilege is going on, those who oil the cog are encouraged to produce more as they slink to stinking poverty.
Presidency in corruption-rampant Africa’s the means to opulence not only for the holder of it but also his or her family, friends in other cases even the tribe.
The capital so much used by hidden African hidden presidents is nothing but sharing bed with the big man plus being able to manipulate him.
In today’s analysis we shall try to explore incidents where the “hidden Simones or presidents behind the curtains” are going on with business as usual.
In Uganda, Yoweri museveni’s wife Janet, the first lady and minister’s still a legendary when it comes to tame the man. It is alleged that her clan and kids are all benefiting from the government of the day and nobody’s blotting this nepotism.
In Equatorial Guinea the tyrant Theodore Obiang Nguema allowed his namesake son to scoop from the treasury as much money as he deems fit. This tinny country with the population of a half a million of which over 50 is living under a dollar a day is like Nguema’s private estate.  The son of president who also is a minister in his father’s government owns mansions and beaches worth millions of dollars in Malibu and a personal jet worth over $ 30,000,000 is untouchable. To add more flavour, the son of the tyrant spends a million bucks in every trip he makes to the US. Why is the US gagged? Wherever there is trouble, just drop a coin.
Not far from Equatorial Guinea there is Congo Brazzaville where the son of the tyrant, Denis Christel Sassou-Nguesso has all it takes even to stop IMF and WB from probing any malpractice involving public funds. Just like Nguema the boy can spend any huge amount of money without raising any alarm! Remember this is the country of just 4,012,809. The irony is. Despite having small population with where 50% lives under a dollar a day, the same country’s the income of $ 3,000,000,000 annually from oil. Where does the money go? Ask the tyrant, his son and cohorts. Anyway, this is Africa.           
In Kenya, Unga (Flour) scandal left Lucy Kibaki morally injured though it was put to rest just like Anglo-Leasing scam.
In Ethiopia the wife of former Prime Minister Meles Zenawi, Azeb Mesfin’s known as Queen of Mega thanks to being alleged to have an upper hand in mega corruption.
The last but not least player’s none other than Mugabe’s sweetheart Grace aka Gucchi. This lady’s renowned for over spending especially at the time Zimbabweans are dying in thousands thanks to poverty and mismanagement. Grace stole thunder when she’s linked with Bloody Diamond by Wikeleaks recently before the media uncovered her coveted love with governor of Reserve Bank of Zimbabwe (RBZ), Gideon Gono. Thanks to her ability to muzzle Mugabe. Nothing’s ever gone wrong in their convenient marriage despite the leak. Gono’s still the governor of RBZ and Grace first lady. This can show you how president behind the curtains are more powerful than those you see on the rostra.
Going back where we started, what’s unearthed in Simone Gbagbo sheds light on a true but grimmer picture of what’s been going on in Africa where presidents behind the curtains have inflicted a great deal of sufferings to our people and our economies. Think about that and evaluate your ruler. Anyway, I was trying to think like president or one of his majordomos. “Politicians and diapers should be changed frequently and all for the same reason,” José Maria de Eça de Queiroz.
Source: Business Times Feb., 7, 2014.

Wednesday, 5 February 2014

Je ni mwanzo wa mwisho wa Zitto Kabwe?


YAMEISHAANDIKWA mengi kuhusiana na hatima ya kisiasa ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA), Zitto Kabwe.
Kitu kimoja tu hakijaandikwa. Nacho ni kuandika tanzia yake kisiasa.
Ukiangalia uzito wa hali ya mpapariko na mparaganyiko aliyomo Kabwe, unashawishika kuandika tanzia. Hata hivyo, siandiki hii tanzia. Wengine watafanya hivyo.
Leo nitaongelea mgogoro wa CHADEMA. Rejea kile kilichoitwa Waraka wa Kuhujumu Chama wa Kitila – Zitto – Mwigamba. Sitaki kudurusu kesi iliyoko mahakamani kama ilivyofunguliwa na Kabwe kwa vile naheshimu mahakama sana.
Ninachoweza kusema ni kwamba ubunge wa Kabwe kwa sasa unatokana na mahakama na si chama chake. Hivyo, punde si punde, Kabwe atakuwa historia ndani ya CHADEMA na sasa nyingine kwenye duru za kisiasa nchini, vinginevyo itokee miujiza.
Wengi wanahoji Kabwe atakwenda wapi baada ya kutimuliwa toka CHADEMA? Nadhani Ansbert Ngurumo alitoa jibu la swali hili kwenye safu yake ya Maswali Magumu ya tarehe 12 Januari.
Sitaki nirudie alichoandika Ngurumo. Ila naweza kusema kuwa darasa lake la walipo wale wanasiasa machachari, tena wengine toka CHADEMA hiyo hiyo wakiwa na vyeo vikubwa kuliko vya Kabwe, ni jibu tosha kwa Kabwe ambaye linapaswa kumfikirisha ili ajiandae kisaikolojia kwa pigo na anguko hili la ghafla.
Kwanini nasema Kabwe au Mkumbo waandike tanzia yao kisiasa?
Kwanza, kukiri kwa Mkumbo Kitila ndiyo ushahidi utakaotumika kumfukuza Kabwe uanachama.
Kwa kukubali kuwa waliandika waraka uliokuwa na lengo la kuhujumu chama, watatu hawa walifanya kile ambacho Wahindi huita ‘suttee’ ambapo mara nyingi wanawake waliochoka na maisha hujichoma moto.
Pili, kile kitendo cha Mkumbo kusema waraka wao haukuwa kosa, lakini akaomba msamaha, ni ushahidi wa kutapatapa ambao ulisaidia CHADEMA kumtimua uanachama. Na hawawezi kusema walionewa. Walifungwa kwa maneno yao wenyewe.
Tatu, kama wenzake Kabwe wamevuliwa uanachama kwa kosa lile lile atanusurika vipi?
Nne, hakuna kitu kiliwavua nguo wahusika na kuwaonyesha kama wababaishaji kama kitendo cha kutaka kujiuzulu ili waondoke kwa heshima.
Wengi walihoji: Kama walichotenda si kosa walitaka kujiuzulu kwa sababu gani?
Tano, wapo waliodhani kuwa Kabwe na wenzake “wangemwaga mtama” kwa maana ya kufichua maovu ya CHADEMA. Bahati nzuri, japo nia ya namna hii ilikuwapo, hapakuwapo na “mtama” wa kumwaga ikizingatiwa kuwa CHADEMA wanafanya mambo yao wazi wazi kwa mujibu wa kanuni na sheria.
Kwa ngoa na usongo alivyonavyo Kabwe, kama kungekuwa na maovu yoyote yaliyotendwa na chama au viongozi wake, bila shaka asingeyataja tu bali angeyaimba kama shairi ili angalau kujifariji baada ya kupata lililompata.
Waswahili walisema: Ivumayo haidumu (hasa inapovumishwa pale isipostahiki kuvuma). Emma Bombeck katika kitabu chake “At Wit’s End”, aliwahi kusema; “Don’t confuse fame with success – usichanganye umaarufu na mafanikio.”
Naye Oprah Winfrey amewahi kusema; “If you come to fame not understanding who you are, it will define who you are – Kama ukiwa maarufu bila kujijua umaarufu utakuumbua.”
Nadhani hili ndilo linawasumbua wengi wanaokabiliwa na hali kama ya Kabwe. Hufiki mbali. Kutojitambua ni sehemu ya utoto ambao si kuvaa nepi bali kutenda kitoto, hata atendaye hivyo awe mtu mzima vipi.
Kabwe kweli alivuma kutokana na sababu mbaya tu. Au tuseme ajali ya kisiasa. Alivuma pale alipojitokeza kuwa mpambanaji mzuri na mtetezi wa haki za wananchi. Baada ya sifa kuingia kichwani, alifikia mahali kusema eti angetaja majina ya vigogo walioficha pesa ughaibuni. Baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema kumvua nguo, Kabwe aliishia kunywea kwa aibu ya kuongopa na kuzua. Hadi kesho tunauliza: Yako wapi majina ya majambazi na mafisadi walioficha pesa yetu nje?
Kitu kingine kilichommaliza Kabwe ni ile hali ya kudai kuwa asingegombea ubunge kwa mara ya pili. Badala yake angwenda kufanya kazi anayopenda ya kufundisha chuoni.
Msimu wa uchaguzi ulipowadia, Kabwe aligombea huku akisahau aliyokuwa ameahidi. Kwa wapiga kura hili lilikuwa pigo kubwa. Nadhani hata CHADEMA waliliona hili na kulihofu. Wenye busara walihofu na kuhoji hili.
Yanini kupayuka wakati unaweza kujiondokea kimya kimya au kutangaza kutorejea siasa wakati wa mchakato wa kutafuta wagombea? Kupenda sifa kwingine kwaweza kuwa kitanzi kwa mhusika.
Pigo jingine kwa Kabwe ni ile hali ya kushutumiwa kuwa anatumiwa na CCM na asikanushe na kutoa majibu mujarabu. Wapo wanaoona kama ni ukweli. Maana ungekuwa uongo Kabwe, bingwa wa kuongea, asingekaa kimya.
Ukiunganisha na uvumi kuwa Kabwe atarejea kwao CCM, unaona ukweli japo kwa wanaojua mizengwe ya CCM, akifanya kosa akajirejesha kule, watamtema kama ganda la mua.
Kwa waliosikia nukuu za Januari Makamba kuwa kiongozi wa nchi awe ni mtu mwenye kujua kutunza familia yake, walishajua kuwa Kabwe hawezi kukatiza pale ikizingatiwa kuwa neno mke au mtoto bado ni msamiati mgumu tu japo nasikia ana mtoto.
Alioa lini? Watamchunguza kuanzia dada zake hadi mama yake ili wamchafue. Huu ni ushahidi kuwa huko CCM nako hakubaliki. Wameishamtumia. Hawamuhitaji tena ili asiwachafue. Kama amewasaliti wenzake, atashindwa nini kuwasaliti waliomtumia, tena kwa kumlipa jambo ambalo hajakanusha?
Licha ya ushiriki wa Kabwe kwenye kuandaa waraka husika, hakuna kilichomuumbua kama kudai kuwa hakuwa na taarifa za mpango huu mzima.
Alichodai Kabwe ilikuwa sawa na kumficha msichana unayetaka kumuoa uchumba halafu bado ukasema una mpango wa kumuoa.
Ushahidi wa kimazingira ni kwamba Kabwe alijua na kuratibu kila kitu. Kuna wanaoona kama hapa kilichokuwa kikifanyika ni kutumiana yaani wawili kumtumia Kabwe naye kuwatumia.
Hata hivyo, tuseme CHADEMA imekuwa na subira kupita kiasi, hasa kwa Kabwe na siasa zake tatanishi. Nadhani kwa uamuzi waliochukua dhidi ya Mkumbo na Mwigamba na hatimaye Kabwe utakuwa somo kwa wengine kuwa kumbe CHADEMA inaweza kung’ata, tena kwa makali zaidi.
Tumalizie kwa kumpa Kabwe nasaha fupi ya Kilatini; Consilio, quod respuitur, nullum subest auxilium – asiyekubali kushauriwa hawezi kusaidiwa.

Hivyo kaka, Acta est fabula, plaudit – mchezo kwishnei kwa lugha ya watoto wa mjini. Huo ni ushauri huenda unaweza kukusaidia kama utakubali kushauriwa.
Chanzo: Tanzania Daima Feb. , 5, 2014.

Iwe Rwiyemaaamu unafwikiri tutaacha kujadili mizigo?



BAADA ya juzi kujadili CV ya Saaada Mkuuuya Saalimu, kijiwe kilipata salamu toka kwa mtu wake wa karibu akiomba tumhifadhi. Nasi tuliwatuma wamwambie kuwa kazi yetu si nepi wala gagulo kumhifadhi mtu.
Tutamfichua yoyote atakayetaka kutuhujumu kama jamii. Ndiyo maana wanakijiwe huwa hatuna simile na yeyote.
Leo hii kijiwe kimeamua kumshukia fisadi mmoja wa kimawazo aitwaye Silva Rwiyependekezamu. Ambaye kwa ufupi huitwa Rwiye.
Naona mgosi Machungi anaingia akiwa na ndita usoni. Si bure lazima kuna jambo, tena kubwa limemuudhi.
Anatuamkua: “Asaaam aikum wagosi.” Tunaitikia: “Wa leykum ssalaam.”
Mbwamwitu anachokoza kwa kujibu: “Alaina wa Alaikum.” Mgosi anamdharau wala hampuyukii.
Msomi Mkatatamaa anauliza: “Mgosi mbona umekunja ndita kunani ndugu yangu?”
Mgosi anajibu: “Leo nina hasia ya kuua mtu. Hivi ukumisikia yue kanjanja Saiva Rwiyemaaaamu akisema eti tisiongee mizigo ya bosi wake aiyotutwisha kana kwamba hatiumii!”
“Alaa kumbe unaongelea huyu msaliti na mchumia tumbo anayefanya kazi ya unepi kwa jamaa! Huyo nshamdharau miaka mingi. Tangu lini mtu anayefikiri kwa utumbo akawa na mantiki Mgosi?”
Mpemba anakwangua Mic: “Yakhe huyu jamaa nshenzi sana. Hajui kuwa kulalamika ni haki yetu kikatiba? Basi aambwe na afahamu kuwa hatutaomba ruhusa mtu wala nani.”
Kapende anaidaka mic hata kabla ya Mpemba kuitua na kuzoza: “Huyu jamaa mpuuzi kweli kweli. Yaani hata kama mizigo inaendelea kutuelemea na kutunukia tusilalamike? Au hawa ni kwa vile nao ni mizigo ndiyo maana wanatetea mizigo kwa vile hawajui ilivyo mizito? Akome na akomae hata kama amekataa kukua.”
Mijjinga naye hajivungi. Anakatua mic: “Beng’we hili li Rweyependekezamu lingenyamazaga kabla hatujalitia makofi. Jitu limeishiwa God knows. Huwa nadharau jitu linalosaliti taaluma yake na kwenda kuendekeza njaa hadi linageuzwaga nepi.”
Mzee Kidevu anamnong’oneza mzee Maneno kuhusu Mijjinga anavyobukanya Kikameruni.
Naye Mijjinga kagundua na kuendelea: “I swear to God. One day I will nyonga somebody.”
Kijiwe hakina mbavu jinsi Mijjinga anavyochanganya Kikameruni na Kiswahili.
Mbwamwitu anaamua kuingilia kwa utani. “Mzee Mijjinga naona ng’eng’e lako la mama haswa.”
“Ulikuwa hujuagi kuwa mimi naongea Queen English! Basi nimeamua kuchanganyaga ili wote wajue. Kama huyu mzushi aliyetaka kututisha aliongea Ukameruni kwanini sisi tusimjibu akajua tunajua kuliko anavyojua?” Anajibu Mijjinga huku akijifagilia.
Kanji anajitia urweyependekezamu naye.  Anasema: “Mimi jua ili bana iko soma Britain na naongea good English.”
Mzee Maneno anaamua kukwanyua mic: “Tushazoea mawazo yenu mgando. Mbona Wachina hawaongei hiyo guudu ingilishi na bado wanaendelea?”
Kanji hajivungi, anakwanyua mic na kuchonga: “Veve iko compare Chinese na Danganyika. Acha tani bwana. Chinese iko viumbe ya juu sana.”
“Kanji acha ubaguzi wa kipumbavu. Baada ya kusema China iko viumbe ya juu utasema gabacholi iko viumbe ya juu pia kwa sababu iko kuja hapa honga mizi kuba yetu pata tenda hata pesa ya EPA.”
“My friend hapana mimi pumbaf wala shiriki iba pesa ya EPA. Hata ile Hindi naachiwa na tukufu juzi siyo dugu yangu. Dugu yangu nyinyi hapa.”
Kijiwe hakina mbavu Kanji anavyotaka kutuhadaa kuwa sote ni dugu wakati dugu yake ni fisadi yenye daraka.
Bi. Sofi Kanungaemba lazima ampe tafu mshikaji wake Kanji. Anakwanyua mic na kuzoza: “Kanji wapashe wapashike. Wanaosema kuwa mheshimiwa Silva hajui kimombo wana vichaa. Angekuwa hakijui angepewa usemaji wa Kurungezi?”
“Sofi umeingiliwaga na nini dada yangu? Mimi nilimsikia akibukanya na kuchanganya kiswangilish akisema eti kaya inapaswa ku-move forward. Hii ina maana gani? Bosi wake mwenyewe hakimanyi kama Nchonga itakuwa yeye?”
Msomi anagundua kuwa maongezi yanaanza kuhama toka kwenye mada kwenda kwenye kujadili watu. Anakunywa kahawa yake na kunyoosha vidole vyake na kusema: “Waingereza husema, healthy minds discuss philosophy. Sick minds discuss personalities. Yaani akili zenye afya huongelea falsafa na masuala. Akili zilizougua hujadili watu. Nasi tusijadili huyu Rwiyemaaamu bali alichosema ambacho ni kutaka kutunyamazisha.”
Kabla ya kuendelea Mpemba anadakia: “Yakhe hapo nimekupata uzuri. Ndiyo, twapaswa ongelea masaala badala ya huyu kidhabu ati.”
Mgosi Machungi anakwanyua mic na kulonga: “Tikubaiane. Huyu Weyependekeza azima ajipendekeze ndipo mkono uende kinywani. Muhimu timwambie hata bosi wake aliyetitwisha mizigo yake kuwa hatinyamazishwi na hatiogopi mtu. Kwani mbwai mbwai bwana?”
Kapende anadandia: “Hakuna huyu mpuuzi aliniacha hoi kusema eti tuache mjadala ili kuwapa nafasi mizigo kuchapa kazi. Wachape kazi gani wakati waliishaivuruga miaka mingi? Mie nawaonea huruma akina Kinamna na Mapepe Ninaye waliotaka kutumia mizigo kuimarisha chama wasijue bosi wao atakifumua.”
“Mie naona Rweyependekezamu hajakosea ati. kama yeye yu nzigo twambeba kwanini asitake tubebe na wenzake kama yeye? Bila shaka haya ndiyo mantwiki alotumia bosi wake kurejesha mizigo ili tubebe. Kwani tukishabeba mizigo hatuwezi jikomboa hata kidogo kwa vile yatuelemea na kutuumiza ati.”
“Ami hujakosea. Hukusikia akisema eti kama rahisi ameona wanafaa basi nasi tuwaone hivyo. Kwani sisi hatuna akili hadi tuamuliwe na mtu ambaye naye ni mzigo kama hao anaowatetea? Maana Waingereza, samahani leo nitatumia maneno ya Kiingereza, husema, show me your friends I will tell you who you are. Au tuseme Waarabu wa Pemba hujuana kwa vilemba. Hivyo, huyu mchumia tumbo ni wa kudharauliwa na kuendeleza mjadala. Kwani kaya hii ni ya rahisi na mizigo yake au wachovu?”
“Msomi nakuunga mkono sana. Sisi ndiyo tinaipa kodi wanayotumia kutanua. Hii kaya ni yetu wala si ya mkuu wala mizigo. Tina haki ya kumijadii yeyote hata kama ni mkubwa.”

Kijiwe kikiwa ndiyo kinachangamka si likakatiza gari la Rweyependekeza. Kila mtu alizoa mitope na kulimwagia huku tukimzomea hadi akatimka huku akiwa anatetemeka kama aliyevamiwa na homa ya ghafla. Ole wake! Siku tukimpata tutamfanya kitu mbaya.
Chanzo: Tanzania Daima Feb 5, 2014.

Tuesday, 4 February 2014

Kweli Jogoo alifundisha vifaranga “kupuu” ndani!

Baada ya kichwa ngumu mkulu mwenyewe kuwashiti akinakiherehere Andalaman Kinamna na Mape Mapepe Ninaye waliowaita wateule wake mizigo, ametoa mpya.  Si amerejesha mizigo na migushi hasa pale alipowapandisha ulaji walaji ambao CVs zao zinaonyesha walivyo vihiyo walioghushi. Hapa ni kama vile matapeli wawili wametosana. Kwanini kuwatumia walevi kupata sifa? Nadhani hawa nao, kama vibinti vya shule za msingi vinavyopachikwa mimba, wameponzwa na kiherehere chao. Hakika kilichotokea ni sawa na kuruka mkojo na kukalia na si kukanyaga manonihino. Ama kweli jogoo aliwafundisha vifaranga kunya ndani! Sijui inaleta picha gani inapotokea yule mliyedhani atalinda maslahi yenu anapokuwa mstari wa mbele, kwa mfano, kuwakingia kifua majambazi, vibaka na waharifu kila aina? Msitu ule ule na nyani wale wale. Kinachogomba ni wale wanaofanya makosa ya kuwaamini wakidhani wana jipya wakati waliishiwa miaka mingi iliyopita tangu aondoke mzee Nchonga.
Kutokana na mlevi kusoma sana somo la Research Methods, aliamua kufanya kile ambacho akina Edward Snowden na Julian Assange huita udukuzi. I decided to bug some new appointed ministers particuluraly Saidia Mkuya Salimu na Naibu wake aitwaye Adam Kigoma Milima. Lolololooooo! Niliyogundua ni makubwa God knows. Bahati nzuri wakati nikifanya ugunduzi na udukuzi huu sikuwa nimevuta wala kupata kanywaji. Nilikuwa mzima na timamu kiakili hata kimwili na kiroho. Ndiyo nilikuwa natoka gymn kutunisha misuli baada ya kutoka kwenye tambiko ambako nako nilikwenda baada ya kuandika article moja kwa ajili ya jarida moja la walevi la ulimwengu kuhusu jinsi wakubwa wanavyoweza kubebana na kufichiana uoza wao.
Kwa vile nilikuwa naandika kuhusu uoza wa wakubwa uchwara, niliamua kutembelea wavuti wa mjengo wa Jamhuri ya Mgongano wa Danganyika na kupata haya madudu. Leo nitacheza na Mkuiya na Milima. Hata hivyo, ifahamike. Wawili hawa ni kile ambacho wakameruni huita typical replica ya kile kinachoendelea kwenye kaya ya Danganyika.  Hakuna kitu kimebarikiwa na kuhalalishwa kama kughushi kwenye kaya hii. Warning, kughushi ni halali kwa vigogo si kwa fito na wachovu. Ukiwa ni kigogo na mzito unaweza kughushi utakavyo hata vitegemezi vyako. Hii ndiyo maana kuna uwezekano wa Milima kughushi na hakuna anayemgusa kwa vile dingi wake alikuwa kizito wa wizara ya njuluku.  Kuna ubaya gani akirithishwa wizara ya baba yake? Laiti wizara hiyo ingebadilishwa jina ikaitwa wizara ya Milima ya Fwedha. Maana kuna kakurithishana fulani. Usishangae dokta Hossein Muinyi siku moja akataka arithishwe ikuu ya dingi wake. Bado mlevi anafanya kazi ya ziada kujua huyu Mkuiya anabebwa na kupaishwa kwenye ulaji kwa sababu ya nini. Hajajua kama ni kitegemezi au kishikaji au kilaji cha kigogo fulani.
Mambo ya vigogo na vishikaji na vilaji na vitegemezi vyao tuyaache. Tuangalie kinachotarajiwa kufuata. Kwa kitaalamu nasema what I am going to do is predict what forgerers and the agents of ruining outfit will do in the ministry of dosh and njuluku.
 Tumeishaonyesha kuwa mkuu wa wizara na naibu wake wa njuluku ni vihiyo. Hivyo, huyu naibu wa sera za ukwapuaji aitwaye Mwehujuu Lameeeki Michemba atakachofanya ni kutumia hawa vihiyo kuchomoa njuluku kwa ajili ya uchakachuaji ujao. Nadhani yote hii itafanyika ili kupatikana kiraka kingine kitakachofunika madhambi ya majamba wazi makubwa yatakayoondoka. Mara hii mmesahau jambazi wa Kiwila na nkewe, vivyele na mashoga zake bila kusahau bi mkubwa Annae Tamaa Makapi wa Makapu? Unadhani waasisi na wanufaika wa HEPA wataepa vipi lupango kama siyo kuwawezesha majambawazi wengine ili wawalinde kama walivyomlinda Tunituni Ben Denjaman Makapu? Are you thither guys? Mnaliwa mnajiona msipoamka. Mliwe hadi wapi na lini ndipo msituke Yarabini?
Hebu twende kwenye mada ya mizigo na migushi. Mizigo ishatua kwenye ulaji na hakuna anayeigusa. Hata wale akina Mapepe walioifichua sasa wanaitetea wakijifanya hawakueleweka kama wakati ule waliposhupalia magamba wakaishia kugeuka magamba wenyewe kama ambavyo wamegeuka mizigo huku mizigo yenyewe ikipeta na kutesa. Hamkumsikia Silvia Rweyependekezamu akisema kuwa tuache kupiga kelele kwa vile bosi wake ameishatimiza wajibu wake wa kutubebesha mizigo? Hamkumsikia akiongea kama vile hana akili nzuri. Ungemwangalia usoni huyu Rweye……mu alivyokuwa akitoa jasho na povu, unagundua kuwa naye haamini alichokuwa akisema. Sema njaa ndiyo ilikuwa ikimsukuma atetee upuuzi na mizigo. Huyo tushamzoea aliyesaliti taaluma yake akageuka nepi ya jamaa.
Niliposoma CVs za hawa vilaza sorry waishiwa sorry wahishimiwa niligundua kitu kimoja. Mkuiya anasema ana masters mbili lakini hana bachela wala haelezei alipozipata hizi mastaz! Ni Bongolalaland pekee ambapo mtu anaweza kunyaka masters wakati hata hiyo bachela hana. Nani angeamini kuwa Milima aliweza kutoka darasa la 12, tena failure, akaweza kufanya masters? Tembelea wavuti wa mjengoni uone utapeli na upuuzi vya kitoto hadi ulewe bila kunywa wala kuvuta. Nimeyaona mengi huko.  Kuna watu wamepewa ulaji wakati hawana chochote zaidi ya kujishebedua kwa wakubwa wenye uchu wa nyuchi na mambo mengine kama hayo.
CV nyingine iliyoniacha hoi ni ya huyu mwingine ambaye nilim-bug, yaani mgosi toka Zenj daktari Hossein Muinyi anayedai ana PhD ya madawa na kukuta kumbe ni mtupu. Maana kwenye maandiko ya kisomi wala hana hata moja zaidi yay ale yanayomnukuu akiwa waziri wa afya. Mpaka leo sijaamini kama kweli mtu mwenye PhD ya kweli asiwe na andiko hata moja la kisomi. Huyu jamaa si ndiye alisababisha milipuko kule Mgongo wa Mboto? Sasa anarejeshwa kwenye ujeshi ili kuua wengine zaidi siyo?  Utapeli mwingine wa kitoto God knows.
Funga kazi ni kuteuliwa kwa kasuku mmoja toka Dodoma aitwaye Ju-ma Mkamiawaandishi na mtuhumiwa wa rushwa toka serikali za mitaa aitwaye Erasto Dhambi. Huyu ana madhambi God knows. Mwenzie waliyekuwa wakiomba rushwa pamoja anasota akingojea hukumu wakati yeye akipewa ulaji! Ama kweli jogoo aliwafunza vifaranga kupuuu ndani!
Chanzo: Nipashe Jumamosi fEB. 1, 2014.

Sunday, 2 February 2014

This is why I adore Danganyikans and boozers


lowasa 47b14
When the good govt that doesn't pay its energy bills hiked power at the tune of 40%, I wrong thought that there’d be some sparks either from the boozers or power generators. Nay! Nothing did happen. I wrongly thought that I’d see some offended paupers taking to the streets at least to tell the world they oppose what’s going on.  Nope!
Whenever power hike occurs everything goes up from daladala to mbavu za dog.  Everybody’ll use what’s possible to top up. Teachers will tell pupils that if they don’t attend their tuition they must expect to fail. Nurses, too, will charge patients not to mention bartenders who, of course, will beg like crazy. Dada poa, too, will increase the prices of their sins. Small houses, too, will hike their services. Truly, all aspects of life will haunt you. While all this menace’s going on, opposition politicians drop the bombshell that the national debt is skyrocketing waiting for you or the next generations to pay it. Before long, the high and mighty in ulaji pointlessly and carelessly will increase their matanuzi knowing that their cash cow, you’ll foot their bill. As if isn't enough, investakers will increase tax evasion on top of many and long tax holidays they always enjoy. As you weigh what to do, Mr Sossie Muhongo the minister of gas drops another bombshell that the gas is for foreigners not locals. Petrol prices swell as the electricity price surges.
I didn't know.  Our sheepish boozers and Danganyika are smarter than I wrongly thought!  Guess what. When you hike power tariffs and prices, they increase illegal connections. They gang up with vishoka and vijembe who illegally and covertly and overtly connect power to the houses.  Who knew that even big factories schools and other ventures could connect power illegally? St Mary’s are you there? They say: Ngoma droo. You think you can take them for the ride little knowingly they beat long before.
Before knowing how Bongo’s ran I goofed. I used to look down at our boozers. I likened them with sheep that can be slaughtered at the will of a shepherd be it in the church or in the barn. Now I know. I was terribly wrong. Boozers are smarter than I am.  Bongolalalanders remind of Samuel Butler’s quote that says, “The truest characters of ignorance are vanity, and pride and arrogance.” Don’t take this serious. For, it is my kanywaji transliteration. Importantly, the point is: We’re pretending to know while we actually cause our own calamity by not acting promptly timely and decisively especially when some goons and swindlers take us for a ride.
Sometimes, fake smartness is ignorance and stupidity altogether. Shall this become the order of the day as it’s always seems to be, when are we to forge ahead just like others? Whom are we punishing? True, we’re but ruining and punishing our coming generations that’ll one day urinate on our graves for being mediocre and stupid. Despite all this megalomania and insanity, I truly love our boozers and the way they commit suttee in the name of being smart.
I still ask myself. How can small hunks such as Burundi, Kenya and Rwanda have reasonable price and reliable supply of electricity in spite of having no reliable sources while we who've them don’t?  What’s a miss? Did you hear how students of University of Nairobi took to street when there occurred power cuts just for a short while?
Again, who cares if at all this is the hunk of the smarter? Bongo ya wajanja hata kama mafala. If you want to know what I mean, just ask yourself. The guy works 365 days a year and his salary can’t buy even a quarter of his needs. Yet, the same guy builds a mansion not to mention enrolling his kids in academics that hike education as well. Wait. The wife of the same guy is always donned in gold and all expensive wiwalo. Nobody questions all this science! Surprise! surprise! You can find that the same guy might have one or two nyumba ndogo and other loss-making ventures such as getting kanywaji every weekend where fat offers are generously made to one or two people. Wait. You can find that the same punk’s a very nourished account not to mention another villa in his village and the oil guzzler. Does this click for you?
 Have you forgotten how artistes are becoming tycoons overnight simply because they use art to deal with drugs? Again, this isn't my take. This is what I hear in the streets of Bongo that nary become bankrupt of rumours and gossips. Faint not my friend. This is Bongo where Bongolalalanders live and do their things. You know them. You can easily and truly see them through yourself. Au vipi? What have you done to stop or erase the injustice of hiking power and other essentials? Aren't you one of them? Include me not. I’m doing my part by telling you the same things you’re supposed to know but you don’t. Why? Hayanihusu is the tendency of everybody. Martin Luther Jr once said, “Nothing in the world is more dangerous than sincere ignorance and consciencious stupidity.”
Source: The Guardian Feb., 2, 2014.