The Curse of Salvation
Saturday, 18 October 2014
Friday, 17 October 2014
Mlevi afaidi filamu ya RugeSingasinga
Pamoja na kupiga bangi na kanywaji, wiki jana nilifaidi filamu iitwayo IpTL yaani Interdependent pilfers in Tanzia Limited (IpTL). Katika filamu hii yenye wahusika wengi japo wanaojulikana ni wawili, inaonyesha ukatili, uroho, roho mbaya hata upofu wa aina yake na vitu vingine vya ajabu ambapo majuha na matapeli tena wenye elimu za kutia shaka wanawatumia wasomi wanaojiona kukubuhu kumbe mabunga.
Filamu hii ilinikumbusha filamu nyingine niliyomaliza kuitaza wiki chache zilizopita iitwayo UdA yaani United and dangerous Animals ambao nao kama IpTL wamewatumia watu unaoweza kudhani wamepiga vitabu kumbe hovyo kuibia walevi kwenye nchi ya kufikirika ya Mizengwe inayopatikana kwenye kitabu cha Saa Ya Ukombozi kilichotungwa na mlevi. Hata hivyo, napanga kuwashitaki watunzi wa filamu hizi mbili kwa kunukuu kitabu changu bila kuomba na kupewa ruhusa. Hayo tuyaache.
Turejee kwenye filamu ya IpTL. Ukiwachunguza wahusika wakuu tagundua kitu kimoja ambacho ni kuzidiana akili na kila mmoja kujifanya mwema na mjanja. Katika unyama na ujambazi huu, vyombo vya habari viliripoti kuwepo kwa barua za msanii mmoja aliyekuwa akijifanya kuionya serikali ya Mizengwe si kwa kuipenda nchi yake bali kutaka kutumia nguvu na kupata chumo la wizi pamoja na kumkomoa mwenzake ambaye aligundua kuwa kumbe alipiga dili la dola kama milioni mia tatu bila kumhusisha yeye wakati yeye ndiye aliyesuka mpango mzima akishirikana na watawala majambazi wa Mizengwe.
Matapeli ni watu wa ajabu. Katika filamu hii mmoja wa wahusika wakuu aitwaye Jimmy Rugeruge Malira toka kaya ya Nshomile anajionyesha kama mzalendo kwa nchi yake wakati ukweli nyuma ya pazia ni jambazi katili ambalo laweza kumuuza hata mama yake ilmradi lipate njuluku. Hivyo anachofanya Jimmy Ruge Malira si upendo wala uzalendo bali unafiki. Unadhani aliandika aliyoandika kwa kuipenda Mizengwe? La. Ni kwa sababu mwizi mmoja amemzidi akili mwenzake.
Ruge Malira anashirikiana na ponjoro Harbinger SeSinga toka kaya ya Gabacholi kuibia kaya ya Mizengwe wakishirikiana na wakubwa zake vipofu na waroho. Ni filamu nzuri yenye kufikirisha na kuonya wale wote wanaojikuta kwenye mazingira kama haya. Pia inafundisha kuwatahadhari matapeli wa nyumbani na wa kigeni. Minyoo hawa nyemelezi kwenye migogo ya wakubwa ni hatari kuliko hata Ebola, ukoma na Ukimwi.
Mtunzi wa filamu hii amejitahidi kuonyesha wasifu wa wahusika kwenye filamu yake. Wote wanatia shaka kuanzia maisha yao elimu zao hata huo ukwasi wao utokanao na wizi na utapeli. Wawili hawa ni viumbe wa hatari sana katika jamii yoyote. Kwani wana sura nzuri na wako tayari kutumiwa na wakubwa wezi wa Mizengwe kuficha uchafu wao kwa kugawiwa kidogo.
Kitu kingine kinachowakutanisha licha ya hulka na tabia zao za utapeli, uroho na wizi ni ukweli kuwa wote ni wasanii au tuseme matapeli wa kimataifa wanaojirahisi kwa wakubwa wenye uchu kuwatumia kuwaibia walio wengi. Pia wana tabia nyingine ya kujifanya wana huruma na wale wanaowaibia. Hawakosi kuchangia upuuzi mbali mbali kwa kutoa vijifedha kiduchu hapa na pale ili waonekana wanaisadia jamii wakati ni mibaka makubwa yanayopaswa kuchomwa moto kama vibaka.
Sifa nyingine ni kwamba wote wana bahati Mizengwe bado haijaanza utaratibu wa kuchoma moto mijibaka. Huwa mara nyingi walevi wanapenda kuwachoma moto vibaka huku wakiwaabudia mijibaka wanaobaka kaya yao.
Ukichunguza mchezo ulivyoanza utalia kama siyo kutamani kujinyotoa roho. Je unaweza kuamini, hata kama ni katika kaya ya kufikirika, kuwa jizi linaweza kwenda kwenye banki kuu na kuchomoa mabilioni ya madafu bila kuwekwa lupango? Hata hivyo, nani aliweke lupango wakati wanaopaswa kufanya hivyo ndiyo waajili wa jizi na jambazi hili? Basi katika kaya ya Mizengwe ujambazi huu wa kwenye filamu ya RugeSingasinga ni kitu cha kawaida. Katika kaya ile inasemekana hata mkuu wao aliwahi kufanya kitendo kama hicho kwa kuiibia banki kuu ili kupata fedha ya kununulia kura ya kula. Na huwezi kuamini hata kama ni katika kaya ya kufikirika. Alifanikiwa na akawa anawaambia walevi wa Mizengwe kuwa angewapatia maisha poa wakati alishapiga njuluku zao. Jamaa huwa hana aibu hata kama ni rais wa kufikirika.
Filamu hiii japo inachusha na kuudhi, ina fundisho moja kuu, siyo kila king’aracho ni dhahabu. Kuna waja tena wakubwa tu kwa nyadhifa ambao ukiwaona unaweza kuwaamini na kuwathamini. Lakini nyuma ya pazia ni wachafu kuliko hata nguruwe. Ni waroho kama fisi. Ni vipofu kama watoto wa mbwa. Wana uchu kuliko hata fisi na wana mawazo mafupi kama nguruwe. Je utawajuaje? Utawajua kwa matendo yao fichi ambayo filamu nyingi huyafichua.
Kuna viumbe wanafanya mambo utadhani wataishi milele. Hata wahusika wakuu kwenye filamu hii ukiwatazama si wazima. Watakuwaje wazima wakati wanaua mamilioni ya walevi wa Mizengwe? Watakuwaje wazima wakati kila siku roho na nafsi zao zinawasuta zikitukuta na udhambi? Wanaweza kujionyesha kama viumbe wenye furaha mbele ya pazia. Nyuma ya pazia unaweza kukuta mijitu inayojutia inayoishi kwa vidonge vya usingizi ulevi na laana nyingine nyingi. Lako ni kuomba Mungu awaongezee mapigo wasifaidi kanywaji na bangi kama sisi walevi tunavyovifaidi.
Unaweza kuamini kuwa hata hili igizo la kuingiza walevi mkenge kupitia kwenye katiba ni bure? Walioko nyuma yake waweza kuonekana watu mbele ya hadhira. Nyuma ya pazia ni madudu ya kutisha mithili ya majini ya kwenye hekaya za mfalme Suleiman. Ni viumbe wachafu na wa hovyo kuliko hata kinyesi. Je utawajuaje? Tafakari kila filamu unayoletewa na wasanii wanaozitumia kutengeza ulaji wao. Onyo, usipende kutazama filamu za udaku wala kusoma magazeti yake.
Chanzo: Nipashe Oktoba 18, 2014.
Katiba-chakachuliwa ikipitishwa najinyonga
Uhuru wa kufanya unavyotaka ilmradi usivunje sheria ni haki kidemokrasia. Japo kujiua ni kosa la jinai, ni pekee kwa walio hai. Hivyo, kwa vile waliochakachua rasmu ya jaji Jose Warioba wanasema wamefanya hivyo kwa misingi ya kidemokrasia basi nami natumia misingi hiyo hiyo kujinyonga kama katiba yao itapita. Siko tayari kufa kwa ugonjwa wa moyo hivi hivi. Heri nawaachie wenye nchi yao wawafanyie watakavyo waliojiruhusu kufanyiwa kila upuuzi na ushenzi. Mie ni muungwana na lazima nife kiungwana kwa kujitia kitanzi kama Mkwawa.
Hata hivyo, kama mwamko na wimbi la kupiga kura ya hapana vilivyoonyeshwa na baadhi ya mashujaa wa katiba vingeendelea na kuipiga chini hii rasimu habithi, huenda waja hawa wageokoa maisha yangu sawa na yale ya vizazi vijavyo, kwa kukataa hujuma na jinai ya kutubambikia katiba inayolenga kulinda maslahi ya kikundi kidogo cha watu tena wasio na huruma. Wakitishwa au kupewa ulabu wakabadili msimamo wajue wameniua.
Naona yule anatikisa kichwa akidhani bangi ishanibangua kiasi cha kuongea kibangi na kigongogongo. Shauri yako! Mie ni shujaa asiyeogopa kifo. Naogopa aibu kuliko kifo. Hivyo, we kaa ukidhani ni bangi na gongo wakati nafanya kweli. Heri mie anayejinyonga kuliko nyinyi mnaonyongwa na kuishi kama punda vihongwe na watumwa. Hata hao wanaowatumikisha na kuwaibia nao ni watumwa wa hayo wanayofanya. Heri nijinyonge kuliko kuliwa na mafisadi utadhani mie samaki au ujaka.
Nina sababu za kufanya hivyo:
Mosi, mawazo na utashi wangu vimedharauliwa na kutupiliwa mbali. Nikikumbuka nilivyokesha na kusafiri kwa punda kwenda wilayani kutoa maoni nasikia kichefu chefu. Iweje niingizwe gharama kusafiri mwendo mrefu hivyo tena kwa mateso nitoe mawazo yadharauliwe?
Kwa vile nina hasira na ufisadi ambao nilidhani katiba mpya ingepambana nao badala ya kuupamba kama ilivyo, nahofia nisipojinyongwa wataninyonga hasa baada ya kumtoa fisadi roho kwa mapanga na marungu. Hivyo, heri nijimalize mwenyewe.
Tatu, niliwashawishi walevi tulianzishe wakagwaya wakijuruhusu kuliwa na kufanyiwa mahepe na kugeuzwa asusa kana kwamba mtoto si riziki. Hivyo, kwa kuogopa aibu hii lazima nijinyotoe roho na kuwaachi amauza uza yao ya kuibiana na kulana kama ilivyo. Kama waliochakachua katiba hawakuogopa kuua vizazi vijavyo, nikijiua mlevi kama mimi nani anajali? Sana sana wabaya wangu wanaosoma madude yangu yakawaita jokomoyo watasherehekea kuwa hakuna mlevi na mvuta bangi wa kuwapigia kelele na kuwaghasi kwa mauzauza wanayofanya mchana kweupe tena watu wazima ambao usingetemea kuwa wangekuwa hovyo hivi.
Wabaya zangu msikonde. Kama upuuzi huu ninaoona na kutamani kumtoa mtu roho utaendelea mie sishiriki wala kushuhudia wala kuuabudia na kuruhusu upite kwa kutumia jina langu safi. Heri nijifie kwa heshima kuliko kuishi kwa aibu. Heri kulala kaburini kuliko kutembea kwenye kaya ya dhuluma na hujuma huku nikigeuzwa punda kihongwe. Heri nioze na kuliwa na wadudu kuliko kuliwa na mafisadi. Heri nimwachia bi mkubwa wangu majonzi ya kunikosa kuliko mimi kukosa heshima na haki katika kaya yangu. Hivyo, natoa taarifa rasimi kuwa kuna wakati mnaniona na kuna wakati hamtaniona.
Wenye kusherehekea mauti ya wenzenu sherehekeeni utadhani nanyi hamtakufa. Mnadhani ni mchezo? Ipo siku nanyi mtakufa tu. Maana imeandikwa, “Kullu nafsin zallikat umaut.” Naona yule anacheka asijue mie bonge ya shehe. Hayo tuyaache. Japo mnaweza kudhani natania, hebu jiulizeni. Wamekufa watu wema kama Madiba na mzee Mchonga itakuwa nyinyi mahabithi na mabaradhuli ambao hata shetani akiwaona kutokana na wingi na ukubwa madhambi yenu huenda atawakataa. tokana na uchafu wenu. Wamekufa watu na utauwa wao itakuwa nyie mnaochakachua hata utashi na mawazo ya wenzenu kulinda aibu na tamaa zenu? Heri mie ninayejinyonga kwa kutetea haki kuliko wale wanaoishi kufanya na kuunga mkono au kuuvumilia uovu. Heri ya mlevi na mvuta bangi mwenye mapenzi na taifa lake kuliko kiongozi mwenye kuliteketeza kwa tamaa upogo na roho mbaya vyake. Heri ya mlevi mwenye kulaumu kuliko wapumbavu wawasifuo watesi wao. Kwani hamkuambiwa kuwa cha mjinga huliwa na mwelevu wakati cha juha na bunga huliwa na mjinga.
Sitaki wale mabingwa wa kushambulia vyombo vya habari kuwa vinawachukia vinapokosa jinai yao waanze kunishambulia. Sifi kwa vile nina hila wala chuki na katiba zaidi ya ilivyopatikana na yale inayosimamia ambayo ni kunila mimi kama ujaka na changu. Katiba ya walevi lazima ifanane na kutungwa nao. Katiba ya walevi haina gharama za kulipana mabilioni wala kuiba mengine ki-Escrow ili kutunisha mfuko wa uchakachuaji na uhongaji. Katiba ya walevi hupitishwa baa bila kuhitaji miezi ya kulipana mabilioni. Katiba ya walevi ni nafuu kuliko hata maji. Kwani unawapa michupa kidogo wanakutana chap chap na kuja kitu kinachoingia akilini. Ukiwapa pombe na bangi nyingi nao wanaweza kuvuta muda ili wapate zaidi sawa na hawa waliopoteza muda mwingi kwenye mipasho ili bora liende wapate mshiko. Wanadhani hatukumbuki hujuma hii kwa walevi? Tunajua sema tunawalimbika tu.
Siko tayari kuishi na kutawaliwa na katiba iliyopatikana kwa ghilba na laghba ili kulinda ufisadi ulafi na kila aina ya jinai. Siko tayari kuramba matapishi yangu kama Ali Kesi aliyekandia Katiba feki akaishia kuipigia kura. Nani anayetaka kutawaliwa na katiba ambayo imepatikana kwa njia haramu na chafu na kupuuzia mawazo ya walevi? Mie japo nina roho ngumu, siyo kama hawa wanaoweza kutumiwa kwa ahadi uchwara na zisitekelezwe wasijue wanaowaita na kuongea nao walikuwa wakivuta muda ili madude yao yapite.
Kabla sijafa naacha wosia. Nimemwambia bi mkubwa ashiriki kwenye kura yoyote ya kupitisha vitu vilivyosababisha kifo cha mumewe. Nichukue fursa hii kuwaasa walevi wasishiriki. Wakikaidi wakashiriki kitakachowakubwa wasinikumbuke wala kunililia wala kulalamika. Salamu za leo ni kwa wanafunzi wangu wa Kinondoni, Biafra na kwingineko.
CHANZO: NIPASHE
Tuesday, 14 October 2014
Rais anapohongwa saa ya dola 5,000!
Kuna wakati ukisikia tuhuma zinazowakabili viongozi wa Kiswahili unatamani ulie au hata ujitoe roho. Miaka michache iliyopita zilizuka tuhuma ambazo kwa kiasi fulani zilionekana kuwa za kweli kuwa rais Jakaya Kikwete alihongwa suti na tapeli mmoja aliyejifanya mwekezaji. Mwaka huu tena kabla ya kuachia ngazi mwakani imefumka kashfa ambapo rais amehongwa saa aina ya Rolex ambayo hata kwa per diem yake anaweza kununua. Saa hiyo inasemekana alihongwa na tapeli mmoja aliyemteua kuwa balozi wa heshima wa Tanzania Marekani jambo ambalo tulilipigia kelele. Je huyu tapeli anayedaiwa kuwa mbioni kupata mradi wa doola milioni 35 ni kuwadi tu na msimamizi wa biashara za bwana mkubwa au ni tapeli wa kawaida aliyemuingiza mjinga fulani mjini? Kama ni kweli au la? Hata kungekuwa na shaka, rais anapojiruhusu kuwa rahisi kiasi hiki lolote lawezekana. Nakumbuka jinsi rais wa zamani Daniel arap Moi alivyohongwa pesa ya Kenya shilingi milioni tano tena zenye picha yake akaitumbukiza nchi kwenye kashfa iliyoponea kidogo kuifilisi ya Goldenberg ambayo inahusishwa na jizi la IPTL Harbinder Sethi Singh. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA
Hongera Othman kufichua janja ya Shein
Japo kukosea ni jambo la kawaida kwa binadamu, makosa mengine yanaweza kuwa na matokeo yenye madhara makubwa kwa mhusika au tuseme mwenye kufanya makosa. Hakuna kosa watakalojutia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na hata marais Jakaya Kikwete na Dk Ali Mohamed Shein kama kumfukuza kazi aliyekuwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar (AG) Othman Masood Othman baada ya kukataa kutumiwa kama nepi na kudhoofisha ofisi na taaluma yake. Kitendo hiki kitawagharimu kwa kiwango ambacho hawakutarajia.
Tofauti na wanasheria nyemelezi wanaotumiwa kama nepi tuliozoea kusikia wakitetea uoza ili waendelee kula kutoka humo, Othman amesimama kidete kutetea haki, katiba, taaluma n ahata watu wake japo si mwanasiasa. Amethibitisha usomi wake ambao ni ukombozi uliomtenga na kutumikia tumbo huku akidhalilika na kuumia. Heri amefukuzwa akiwa na nafsi na dhamira safi kuliko wale wanaoendelea kukaa maofisini kufanya mambo machafu ambayo hata akili zao hazikubaliani nayo zaidi ya njaa zao. Nadhani licha ya kustahili pongezi, Othman anaondoka kishujaa na kwa heshima.
Othman amekataa ukuku na kukumbatia ukanga ambapo kuku hula na kushiba na kulala kwenye banda safi lakini bado akabakia kuwa mfugo tofauti na kanga alaye kidogo lakini akayaweka majaliwa yake mikononi mwake na muumba wake tofauti na kuku ambaye majaliwa yake yako mikononi mwa kiumbe mchafu aitwaye binadamu.
Je ni kwanini waliofukuza Othman watajutia?
Kwanza, kufukuzwa kwake kumefichua msimamo dhaifu wa Shein tokana na ukweli kuwa kumbe kwenye mjadala wa kuandika katiba mpya Zanzibar haikuwa na msimamo wala mtetezi. Je Shein yuko ofisini akilipwa kwa lipi iwapo ameshindwa kutetea maslahi ya taifa la Zanzibar? Je msimamo na tabia ya Shein si ushahidi kuwa amepachikwa pale kama nyampara wa kuwachunga wazanzibari kufuata matakwa ya Dodoma alikotengenezwa? Je wazanzibari watakubali kuwa na kiongozi asiyelinda maslahi yao? Je Shein alinyamazishwa au aliamua kufuata msimamo wa chama akijua fika kuwa bila nguvu ya Dodoma urais wake unakuwa mashakani?
Nadhani kama kuna anayechekelea sasa mbali na Othman si mwingine bali Maalim Seif na CUF ambao bila shaka wamepata hoja nzito na yenye mashiko kwenye kampeni za mwakani. Je CCM wameliona hili hivyo au walichukua uamuzi kwa hasira wasijue hasira hasara? Je kwa kufichuka ukweli huu kuwa Katiba ya CCM waliyopitisha hivi karibuni baada ya kuchakachua kura haina maslahi na Zanzibar wazanzibari watakaa kimya sawa na wenzao wa bara wenye historia ya ukondoo na kutojali? Je kama wazanzibari wataamua kuungana na CUF kuzuia kufanyiwa hujuma kama ile ya mwaka 2001 CCM na serikali yake itatuma jeshi jingine kuua tena na kuzalisha wakimbizi wengine au kuacha Shein alipie ukimya wake?
Kimsingi, hali hii ni tete na haina jibu moja rahisi. Kinachofurahisha ni kwamba, baada ya rais Kikwete kuwasaliti na kuwazunguka UKAWA akidhani yamekwisha, amepata kikwazokingine ambacho sidhani kama CCM wana watu makini wa kuweza kuwasaidia kukivuka kwa kuwashawishi wazanzibari ambao wameishachoka kutenzwa kama mkoa ndani ya muungano tata wa sasa chini ya katiba tata ya sasa.
Kitu kingine kitakachofanya CCM wajutie ni ukweli kuwa Othman sasa ni mtu huru anayeweza hata kuamua kujiunga na upinzani na kushiriki siasa. Hili likiongezea na sintofahamu baina ya Shein na mtangulizi wake Amani Karume ambaye shemeji yake anakabiliwa na mashtaka ya ajabu ajabu, uwezekano wa upinzani kuwa na nguvu Zanzibar zaidi ya wakati wowote ni mkubwa. Utashindwaje kuwa na nguvu wakati hawa wote watatu adui yao ni mmoja? Lazima wataungana kumkabili na kuzuia asiendelee kuwanyanyasa.
Hili likichanganyikana na ukweli kuwa CCM imegawanyika hasa kipindi hiki inapoisha awamu moja kwenda nyingine, uwezekano wa kutokuwa na mafuta ya kutosha kiakili hata kimkakati kuzuia nguvu ya Zanzibar ni mkubwa. Hapa bila shaka kila mtu atakufa au kupona kivyake hasa ikizingatiwa kuwa rais anayeondoka hana ushawishi wala kipawa cha kufanya hivyo ukiachia mbali kuacha kila mmoja kwenye chama ajifanyie atakavyo huku yeye akiangalia tokana na historia yake ya kutokuwa na udhu.
Kwa sasa CCM ina mitandao inayoviziana na kutishiana uhai huku na uchakachuaji wa katiba ukizidi kuiweka pabaya. Kwa Zanzibar ukiongezea na kufumka kwa ukweli kuwa kumbe kwenye mjadala wa kuandika katiba mpya waliuzwa, bila shaka hakutakalika. Hivyo, si vibaya kusema kuwa kishindo cha kutimliwa Othman na yale aliyofichua vitaiweka CCM pabaya kuliko ilipowahi kuwa. Ukiongozea na tuhuma za ufisadi wa ESCROW unaoendelea kuitafuna hasa baada ya wafadhili kutishia kugoma kuchangia kapu lake, ndiyo basi tena. Kwa bara wanaweza kufanya mizengwe na ulaghai wao.
Kwa Zanzibar, sitegemei umma uwaruhusu hasa ikizingatiwa kuwa hawakuhusishwa kwenye katiba inayopaswa kuwatawala bila kusuluhisha migongano baina yake na katiba ya Zanzibar. Je tujiandae kumuaga Shein na kukaribisha upinzani au kushuhudia vurugu? La vurugu na mauaji kama ya 2001 ondoa hasa ikizingatiwa kuwa watawala wengi wa Afrika wanaogopa kupelekwa The Hague.
Hongera Othman. Kufichua hila na jama dhidi ya wazanzibari. Kwani msimamo, ujasiri na ushujaa wako unaweza kuwa nyenzo mojawapo ya kuiangusha katiba kidhabi waliyopitisha kwa maslahi yao. Je Wanzanzibari watagoma kushiriki zoezi ambalo limeishachakachuliwa hata kabla ya kuanza?
Chanzo: Tanzania Daima Oktoba 15, 2014.
Kijiwe chawapongeza Mdee na Othman
Siku hizi hakiitwi kijiwe bali colloquium yaani mkutano wa wasomi wakitongoa na kujadili falsafa na madude mengine yaliyowashinda wahishiwa
Leo Mpemba kajilawa kweli kweli. Ana jambo si dogo. Baada ya kufika kijiwe na kukuta watu wachache aliendelea kusoma gazeti lake la Danganyika Daima. Allivuta muda huku akinywa kahawa yake taratibu.
Mara mtu wa mwisho kufika ambaye ni mzee Maneno anatua kwenye benchi.
Mpemba anakula mic, “Yakhe mwaionaje hii ya bwana nkubwa Made in Dom Dokta Shine kumtimua alokuwa mwanasharia wake nkuu shujaa Masudi Osman Osman?”
Msomi Mkatatamaa aliyekuwa akisoma gazeti la The Mail on Wednesday anakamua mic, “Kwanza huyu bwana shujaa kweli kweli. Pili, nadhani huko aliko anafurahia kufukuzwa kwake. Kwani ametolewa sadaka ili ukweli ujulikane kuwa Mpemba huko kwenu hamna kiongozi zaidi ya nyampara aliyewekwa kuwachuga msibughudhi ulaji wa wale waliomtengeneza na kumsimika pale.”
Kabla ya kuendelea Mheshimiwa Bwege anadakia, “Usemayo Msomi ni kweli. Huyu bwana anaweza kuwa amejipalia mkaa asijue. Nadhani mshirika wake Hamad Madevu wa Kafu sasa anachekelea kwa vile kujulikana kuwa Zenj haikuwa na msimamo wala mtu wa kutetea maslahi yake lazima kutajibiwa kwenye sanduku la kura mwakani. Napendekeza tujadili pia huyu bi mkubwa Halima Mndee aliyeburuzwa lupango kwa sababu za kitwahuti. Laiti wangeburuzwa akina Sam Sixx na Njaa Kaya huenda ingeleta maana.”
Msomi anakatua mic tena, “Uchambuzi wako ni makini sana mkuu. Kwanza nakubaliana nawe kuwa jamaa kajichimbia kaburi kisiasa. Nionye. Kama hawa wajivuni na matwahuti wataendelea na hila zao kwa kutegemea mituringa, kipindi hiki tutashuhudia machafuko zaidi ya yale ya Komandoo na Mkapu ambapo wachovu wengi walinyotolewa roho na kuzalisha wakimbizi kwa mara ya kwanza.”
Anabwia kahawa yake na kuendelea kudema, “Hakika huyu bi mkubwa Halima si mchezo. Naye kama Othman, ameonyesha jinsi mfumo wetu ulivyo wa hovyo sana. Uzuri wote ni wanasharia ambao vitendo vyao vimewaacha uchi wanasharia nyemelezi wanaotumika kama nepi kama vile Mura Freddie Wer-ema ambaye yuko tayari hata kumuuza bi mkubwa wake ilmradi ajaze tumbo lake lisilo na shukrani.”
Mijjinga aliyekuwa ana usongo wa kutia timu hatimaye anakwanyua mic, “Yote tisa. Kumi ni kufichuka ukweli kuwa kumbe ukimya wa Shine haukuwa na neema kwa wale anaodai kuwaongoza. Mie nilishangaa kutomsika kwenye kasheshe hii.”
“Ulitegemea aseme nini wakati bosi wake alikuwa ameishamaliza kila kitu? Nadhani walimnyamazisha ili kusiwepo misimamo tofauti hasa ikizingatiwa kuwa bosi wake huwa si mjenga hoja zaidi ya kuwa mviziaje wa kawaida na mtu asiyeaminika kufanya naye makubaliano kama ilivyotokea hivi karibuni kwa UKAWE.” Anapayuka Kapende huku akibofya kisimu chake cha kisasa.
Mijjinga aliyekuwa akimnong’oneza jambo Mgosi Machungi anaamua kutia guu, “Nadhani mwisho wa ubabaishaji unakaribia. Walidhani nguvu ya kuwang’oa ni UKAWA peke yake wasijue gonjwa limo ndani. Nijuavyo wazenj hawatakubali huu utwahuti unaofanya waendelee kumezwa.”
Mpemba hangoji, “Yakhe msemayo kweli. Sie hatukubali huu upuuzi tena. Kula mwaka waja na ghilba hii na ile. Kipindi hiki nawaapieni lazima tupige ntu chini. Utatendeleaje tawaliwa na jitu liloweka kuwezesha kunyonywa?”
Mgosi Machungi aliyekuwa kimya muda mrefu anaamua kula mic, “Kwanza wenzenu nina huzuni sana baada ya kufiwa na bi mkubwa Mahiza hivi kaibuni. Tilimzika juzi kue Mashindei Vuga. Hayo tiyaache. Mie namshukuu Subhana kwa kumtia hasira Shine akamtimua Osmani ili ukwei ufumke na kutuweka wote huru.”
Kabla ya kumaliza Bi Sofia Lion aka Kanugaembe anachomekea, “Dua la kuku halimpati mwewe. Tutaendelea kutesa na wenye wivu wajinyonge. Hivi mlitaka mheshimwa Shaini asimfukuze mtu muasi ambaye aliamua kujifanyia atakavyo badala ya anavyopaswa kufanya?”
Mipawa anakula mic, “Lawama nyingine hazina hata mashiko. Wewe ulitaka afanye nini wakati umeishaambiwa kuwa sirikali ya Zenj haikuwa na msimamo? Kwa vile yeye ana msimamo si aliamua kuuonyesha kwa wasio na msimamo kiasi cha kufukuzwa ulaji. Hapa hatuwezi kumlaumu Othman bali wale waliokosa msimamo na uchungu na haki za Wazenji.”
“Veve tegemea nini. Iko taka rahisi comment on everything kama Kapa? Hii bwana Sumani kosea rahisi sana paka tia yeye hasira hadi nafuta yeye. Kosa yake hapana laumu rahisi bure bwana,” Kanji anamwaga upupu wake.
Mpembaaliyekuwa akisikiliza kwa makini anaamua kutia guu tena. “Yeye apata wapi udhu wa kufukuza wakati apaswa fukuzwa yeye aregee kule alikotengezwa? Hebu nyie ngojeni. Mtajaona kile ambacho kilimfanya kuku asikojoe wallahi.”
“Unadhani wazenji mwaweza mtimua kazi jamaa wakati waliomsimika wapo wanaangalia?” Anauliza Mbwamwitu.
Mpemba anajibu, “Wemezoea vya kunyonga vya kuchinja hawaviwezi. Walizowea kutugawana makundi baina ya wa huku na kule wasijue siku moja watajatuunganisha kwa kukosa msimamo wa kulinda maslahi na utaifa wetu.”
Kijiwe kikiwa kinanoga si Othman akatia timu kijiweni! Kila mtu alisimama na kumlaki huku tukimpiga kwa ofa za kahawa. Baada ya hapo tulilazimika kuahirisha colloquium kwa vile tulimpeleka jamaa hoteli kufanya party.
Chanzo: Tanzania Daima Oktoba 15, 2014.
Monday, 13 October 2014
15 years without Mwalimu Nyerere
This is how this blog commemorates the demise of Mwalimu Julius Nyerere.
Mwalimu since you passed on things have changed. All rats are now operating freely after the cat left the scene. The narrative has changed. Equality is no longer an agenda for the nation.It is no longer in anybody's rote except for a few of your believers. Accountability has long died. They say it is time for MADILI but not time for MAADILI as it used to be under your watch. UJAMAA was felled an on its place UHUJUMAA took a front seat. As well KUJITEGEMEA became KUJIMEGEA. These days a dog guards meat while a hyena becomes a guardian of sheep. Those you castigated to be immature and inept are now in the big picture sigogglin. Mwalimu, tumekwisha! We are finished.For they eat as as pleased wantonly and pointlessly.
It is official now donor have suspended Tanzania aid
IPTL scandal has started to bite. It is official now. Donors have suspended Tanzania aid after the government has been dragging feet in dealing with the scam. History shows that IPTL was created by bigwigs during second-post independence president Ally Hassan Mwinyi whose laxity gave birth to grand corruption in the country.
For me info please CLICK HERE.
Sunday, 12 October 2014
IPTL is the brainchild of CCM
Those looking for the link between Independent Power Tanzania Limited (IPTL) and Chama Cha Mapinduzi (CCM) should carefully read an excerpt from IPTL dossier I got from a friend.
In a nutshell, IPTL is a brainchild of CCM and its bigwigs. The father of IPTL is Ali Hassan Mwinyi while the uncles are Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete, Kighoma Malima, Andrew Chenge, and many more.
Follow the story hereunder.
Ruling party CCM Secretary
General and Minister for Planning, Horace Kolimba (since deceased) was involved
in the original brokering that led to IPTL. In July 1994, Kolimba visited Malaysia and
raised the power-rationing problem with the Malaysian government. The latter
advised Kolimba that Malaysia
had solved similar problems by licensing and promoting independent power
producers (IPPs). The Government of Malaysia arranged for Kolimba and his
delegation to meet with potential Malaysian investors, who were then invited to
visit Tanzania
for an assessment of the situation. Datuk Baharuden Majid of Mechmar made his
first visit to Tanzania
in August 1994. Mechmar had already built a 2.75 megawatt wood-fuel plant for
the Commonwealth Development Corporation (CDC) in Tanzania (1993), and already
knew Tanesco well. He held discussions with the Minister for Water, Energy and
Minerals Jakaya Kikwete, Simon Mhaville of Tanesco, Esther Masunzu, Assistant
Commissioner for Energy, and Juma Ngasongwa, Personal Assistant to President
Mwinyi responsible for economic affairs, all of whom confirmed that Tanesco and
the government welcomed the IPP solution. A month later, an MOU was signed and
IPTL was launched.
Tanesco's Managing Director
Simon Mhaville was heavily pro-IPTL, as was his PS at the time, Raphael Mollel.
Mollel continued to support IPTL from the Treasury, where he was appointed
Deputy PS. A friend of Mhaville told me that Mhaville claims to have been
anti-IPTL, and Mollel claims he was “only following orders.” Mhaville's
successor, Baruany Luhanga has distanced himself from IPTL. Minister of Energy
and Minerals, William Shija, was pro. There is widespread agreement that
President Mwinyi gave IPTL his tarnished imprimatur. It is precisely the Mwinyi
heritage surrounding IPTL that Mkapa has struggled to contain since coming to
power in 1995.
A major player throughout
was Andrew Chenge, the Attorney General and a personal friend of Mkapa.
Chenge's office reviewed the IPTL contract on behalf of the government, and
found it acceptable to the letter. At the time, Tanesco advisors--Acres (Canada)
and Hunton and Williams (U.K.)--had written damning reports pointing out that
IPTL: (1) was a long-term solution to a short-term problem; (2) did not
constitute part of a ‘least cost' power policy;10
(3) constituted excess capacity;11 and
that (4) the project was highly overpriced.12
Both also criticised the proposed IPTL contract, which was generous to the
supplier and passed all the risk to the government of Tanzania. IPTL was not
time bound, and the final cost to Tanesco would be negotiated after the project
was completed!
The PPA was appraised for
the government by Mary Ndosi, a State Attorney in Chenge's office.
Acknowledging that the Acres and Hunton and Williams comments on IPTL had been
reviewed, Ndosi states, with magnificent insouciance: ‘Their advice should be
treated as part of our advice on this proposal only to the extent it is not in
contradiction to what is contained herein.' There is an affidavit (see below)
claiming that Mary Ndosi actively supported IPTL.
Dr Abdallah Kigoda was
appointed Minister of Energy and Minerals by President Mkapa in February 1997.
Kigoda's rise from a relatively junior post in the Planning Commission to high
office was meteoric. On becoming Treasurer to CCM, he joined the inner circle
of the ruling party. After one visit to Malaysia , he came home with a large
cash contribution to finance an important CCM meeting, though the amount that
was eventually used for this purpose is open to dispute. Until events forced
him to fall in line behind the Mkapa/Rutabanzibwa position, Kigoda was a
staunch supporter of IPTL. He had stated that there was no contradiction
between IPTL and Songas, and that both would be commissioned.
After the 2000 presidential
and parliamentary elections, Kigoda was replaced by Edgar Maokola-Majogo, a
career politician who had consistently toed the pro-IPTL/anti-Rutabanzibwa line
in Cabinet, arguing on at least one occasion for Rutabanzibwa to be sacked.
Mkapa's first Minister of
Finance, Daniel Yona, another senior pro-IPTL figure, likewise declared
nonchalantly that the government could always foot the bill if Tanesco ran out
of cash.
From early on, the
Prevention of Corruption Bureau (PCB), which reports directly to the President,
took a lively interest in IPTL. Edward Hoseah, Director of the Bureau and
Co-ordinator of the government's anti-corruption strategy, actively pursued the
case, and at one point was ready to arrest Rugemalira on corruption charges.
Hoseah was systematically thwarted by the Bureau's Director General, Maj. Gen.
A L Kamazima, who along with Chenge, repeatedly told the President that there
was no evidence of corruption in IPTL.
I was struck by the fact
that there was very little adverse commentary from the business community or
from the opposition parties concerning IPTL. Looking for a critical local
voice, I approached John Cheyo, an opposition Member of Parliament and Chairman
of the Public Accounts Committee (PAC). We met in the lobby of the Dar es Salaam Sheraton.
It was not a good choice. As we talked, none other than James Rugemalira came
over to greet him in the warmest manner. I hastily turned over my pile of
newspaper cuttings so that he could not see what we were talking about. But it
was too late. The following day, Cheyo held a press conference in which he sang
the praises of private investments in the power industry, telling the
government not to meddle with them! I later heard that he was aggressively
anti-Rutabanzibwa in meetings of the PAC. On
other occasions, Cheyo has been a strong critic of official misuse of public
funds.
Much of the anti-IPTL
commentary came from the donor community or from foreign journalists. The World
Bank's Resident Representative Ron Brigish was more guarded than his
predecessor Motoo Konishi, but he did not hide the Bank's concerns with the
economic implications of IPTL. Just before becoming Swedish Ambassador to
Tanzania , Sten Rylander also went on record criticising IPTL. The Swedish aid
agency SIDA, heavily involved in supporting Tanesco over many years, had noted:
Recent
events, especially the IPTL affair, (an unsound contract … for capital costs,
commercial arrangements, and security package resulting in a cost of procured
energy to Tanesco significantly above its own selling price) have shown that in
spite of support to least cost discrete infrastructure projects like Kihansi
and Kidatu, the total cost structure for power production can be jeopardised by
uninformed Government-private sector deals outside the agreed least cost
project frame. … The IPTL contract and the energy policy review have
highlighted the need for a proper regulatory regime, anchored in legislation,
to ensure competition on fair and equitable conditions … to make the market in
the energy sector work…' (Swedish International Development Agency, Dar es
Salaam, 1999)
The IPTL issue was raised
at the Consultative Group meeting between Tanzania and donor agencies in Dar es
Salaam in December 1997 and again in May 2000. In an interview with Reuters,
European Delegation Head Peter Christiansen gave voice to continued donor
concerns: ‘The European Union was concerned that the government was silent in
cases where top ruling party officials and senior government officers were
implicated as in the case involving Malaysian-backed IPTL.' (Guardian, 24 May 2000:1).
Reuters' Mark Dodd left
Tanzania in July 1998. He regretted that he had failed to get a final interview
with President Mkapa “to ask about the role of the Attorney General and
Minister for Minerals and Energy in the signing … of a contract … with IPTL …
described by the IMF as ‘an unsustainable burden on the economy.’ ” He
continued:
10 Hydro and
natural gas are much cheaper, and both locally available; fuel oil has to be
imported.
11 IPTL
clamed--though it was not part of the PPA--that they would run at a minimum
capacity utilisation rate of 85%; otherwise they would increase their price
from 10 cents per unit to nearly thirteen, or even more.
12 At that
time, neither advisor knew that IPTL had switched medium for slow speed
engines: the project was actually much more overpriced than either imagined.
New Constipation: Hat off to Mdee Othman
Dear Halima Mdee (MP) CHADEMA and Othman Masoud Othman former Zenj’s Attorney General (AG),
I'm writing this piece to wee bit celebrate your sacrifice and commitment. I do so with hope and happiness. It is boozers’ honour, recognition and appreciation of your noble cause which, essentially, is theirs.
Though what you did might be seen lightly as something any boozer can do, indeed, you’re our hero this year. You’re simply because of championing our God-given right of having a clean constitution written and enacted by us.
Mdee’s put behind bar simply because she fulfilled her obligation, organizing demonstrations that were butchered even before seeing the light of the day. On the other hand, Othman’s summarily and unceremoniously axed simply because he stood by his profession and justice. Ironically, all those macabre acts were committed in the same month in the hunk priding itself to be democratic while it actually isn’t.
Boozers salute you. They’re fully and totally behind you in your adventure of fighting for their rights, especially, your, unquestionable commitment and tireless efforts to foil the so-called new constitution that’s illegally enacted and passed recently by a few self-seekers intending to secure their ulaji, and avoid being dragged before the court for the heinous crimes they committed in office.
Though you’re victims of this plot, boozers believe, as Othman put it, truth will come forth and time will tell. Boozers aren’t waiting for the time to tell. Instead, they’re telling everybody that what’s done is wrong, immoral, illegal, and, of course, shameful, and dangerous for our hunk.
When you’re persecuted and axed boozers asked: Were you Chama cha Maulaji (CcM) cynics would you be maltreated and humiliated like that? The answer’s obvious. CcM’s goons, sympathizers, cynics and biggies are untouchable. They’re but sacred cows that’d not be touched. The cruelties you suffered has proved to boozers beyond doubt that you’re sacrificial lambs aimed at protecting sacred cows. Your predicaments are the results of lack of vision, leadership and sense of facing the reality for those who persecuted you.
They may disgrace, torture, humiliate and axe you. They won’t do the same to your relenting eagerness for justice. ANC radio Umukhoto we Sizwe had one beautiful slogan on struggles. It used to say in its mantra that “There is one path, one path only. It is the path of relentless struggles.” Therefore, relent not. Nay even regret. The cause you are persecuted and maltreated for is noble. As Othman put it, time will accurately tell.
Being ace lawyers and unwavering fighters for justice rest assured that boozers back you. Come rain, come shine. The crime you’re opposing is very obnoxious and dangerous for those espousing it save that their myopia hampers them from seeing it this way. Those who concocted it thought they’d get away with murder without a fight. Nay, alluta continua! However, we still have a long way to go, we still know our destination, justice and the felling of their fake document.
Dear Mdee and Othman, we salute your courage and attempt to pull down the whole thing. You verily showed the difference between yourselves and hyena-like lawyers that are willingly and blindly used by greedy supremoes to rob boozers. You've paved the way for a big thing to come. You've differentiated yourselves from those used like diapers by supremoes to fill their thankless tummies. I know. Sellouts and let-downs like Freddie Were-ma won’t like my stuff. Again, this is the truth. They’re abusively used like diapers. They betray disgrace and abuse their profession. They've no ethics but only one thing, eat whatever thrown at you even if it is the fresh of your loved ones. You indeed are heroes by all standards.
Differently from the above bêtes noirs, you’re as innocent and courageous as the child who told the king that he was nude whereas other cowards couldn't except to praise all nonsensical and insane undertakings.
I salute you on behalf of all boozers who are likely to be the dupes of the document shan't they stop it. Again, is there any logic for it to be given our consent? Why consenting to larceny and robbery of which we’re the preys? Are we such unreasonable and insane really? Nay, it can’t be boozers.
Folks, I know you've a lot in your plate especially at these trying times. Importantly however, never back off, give in or give up. Take it from king boozer. All boozers are behind you ready for whatever to see to it that the thing is pulled down. Dedan Kimathi once said, “Better die on your feet than living on your knees. Boozers won’t badge in this encounter. Thanks for your exemplary leadership, commitment and sacrifice fellas.
Source: Guardian Oct 12, 2014.
Sitta: Mshika mbili
Friday, 10 October 2014
Tuesday, 7 October 2014
Good news from Da Philo Ikonya and her book the Nightbird
![]() |
Philo Ikonya © 2014 Aidoo-Snyder Award for Still Sings the Nightbird
"The prize committee felt that Ms. Ikonya's work is extremely innovative and transformative." http s://www.facebook.com /pages/Philo-Ikonya- Publications/1127977 22129643?ref=hl I received an elating call from Nwando Achebe, a professor of History and this is what she said: "I am calling as the Co Convener of African Studies Association, Women's Caucus on behalf of the panel for the Aidoo-Snyder Book Award 2014 to let you know that your...
Se eller kommenter Philo Ikonya sitt innlegg » |
Tukatae katiba ya kifisadi
Hali ilivyo, na mambo yanavyokwenda, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vyama nyemelezi na washirika zake wamepania kutubambikia katiba. Hili halikubaliki na halipaswi kukubalika wala kuvumilika. Katiba ni mkataba wa kudumu baina ya watawala na watawaliwa unaolenga kuonyesha jinsi ya kutawala na kutawaliwa. Uzoefu unaonyesha kuwa katiba viraka ya zamani imetumiwa na genge la watu kulihujumu taifa bila kushitakiwa. Watanzania wakiendelea na ujinga, ukimya, woga na kutojali wataendelea kuumizwa. Hili nalo halikubaliki.
Ili kujinasua na jinai hii ambayo walaji wetu wanapania kutenda, lazima umma usimame na kuizuia. Ni bahati mbaya. Wananchi wamewaachia wanasiasa kazi ya kupinga jinai jambo ambalo linafanya mapambano kuwa magumu. Kuendelea kuwa watazamaji na mashahidi wa uovu huu ni kujiruhusu kuhujumiwa si sisi tu bali na vizazi vijavyo. Jamii yoyote yenye watu wanaofikiri sawasawa isingeacha kikundi kisicho na uhalali wowote, kimantiki na kisheria, kujitwisha jukumu la kuandika katiba ya watu yao. Nani kawapa madaraka ya kufanya hivyo? Jibu ni rahisi. Wamepora madaraka na kuteka mstakabali wa taifa. Wanasema kuwa katiba inayopendekezwa huko Dodoma ni aslimia 75. Hizo aslimia 25 zimekwenda wapi? Andrew Chenge Mwenyekiti wa Kamati bandia ya Uandishi ya Bunge la Katiba, alikaririwa akisema, “Bunge hili limeboresha Rasimu ya Katiba vizuri sana. Rasimu hii imebeba asilimia 75 ya maudhui ya Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba (Joseph) na nyie wajumbe mmeboresha kwa asilimia 25 tu.” Huku “kuboreshwa” kunamaanisha nini wakati hayo maboresho si mawazo ya wananchi? Je hawa walioondoa haya maoni na utashi wa wananchi kweli wanaweza kuboresha kitu au kuboronga? Bila shaka jibu ni kuboronga. Je jamii inayojiruhusu kuhujumiwa na kutekwa na kikundi kidogo cha watu ni hai kweli? Tunashindwa nini kuwaambia tena kwa sauti moja kuwa inatosha? Sidhani kama hili nalo linahitaji wafadhili au msaada toka nje.
Kwa kujiruhusu kuchezewa sisi na mstakabali wetu hivi, tumeonyesha udhaifu mkubwa kiasi cha nchi nyingine kutucheka. Tumezidiwa na hata viinchi vidogo kama Hong Kong ambao wamekatalia mizengwe ya taifa kubwa, China? Tumezidiwa na majirani zetu wa Kenya waliofanyiwa mizengwe wakakataa kata kata hata kwa kutishia kufanya nchi isitawalike? Watawala wetu ni ving’ang’anizi. Hawajui lugha ya majadiliano. Yako wapi matunda ya majadiliano na makubaliano ya hivi karibuni baina ya rais Jakaya Kikwete na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA)? Aliwaita na kuwahadaa ilia pate muda wa kuendeleza jinai hii. UKAWA wametimiza jukumu lao. Je wananchi wamefanya nini kuwaunga mkono?
Wapo wanaojidanganya kuwashawishi wananchi wapige kura ya hapana kupinga kupitishwa katiba hii feki. Uzoefu unaonyesha kuwa CCM imekuwa ikiiba kura (kuchakachua). Tukifanya kosa kuruhusu hichi kiini macho ilichotengeneza CCM na kukiita katiba ya wananchi, tutajilaumu na kujuta. Watashindwaje kuchakachua, kama kawaida yao, ilhali tume itakayosimamia kura ya maoni ni ile ile iliyobariki uchakachuaji? Watashindwaje iwapo polisi na vyombo vyote vya ulinzi na usalama ni washirika wakuu wa jinai hii kwa umma? Tuguswe wapi kama jamii ndipo tustuke? Tufanyiwe maudhi kiasi gani tustuke?
Kwa tuliosoma rasimu ya tume ya Kukusanya na Kuratibu Maoni ya Jaji Joseph Warioba (CRC), tulijiridhisha: Katiba iliyokusudiwa baada ya kukusanya maoni ya wananchi ilikuwa ya kimapinduzi na ya umma. Ilionyesha nia ya wazi ya kupambana na ufisadi uliotamalaki kiasi cha kuanza kuhalalishwa na watawala wanaoufanya na kunufaika nao. Hili liliwaudhi na kuwatisha watawala. Wapo waliohofia kusimamishwa mahakamani kujibu mashtaka ya hujuma na ufisadi waliofanya wakiwa madarakani. Wapo walioona kama mipango yao ya kupora madaraka imevurugwa. Hivyo, kwa pamoja, chini ya CCM, waliamua kuhujumu rasimu ya Warioba huku wakimtisha na kumshambulia asitishike wala kutetereka. Bahati mbaya, Warioba hajaungwa mkono vilivyo. Wametumia fedha na muda wetu kufanya mambo ya ajabu katika karne ya 21 nasi tunaendelea kujifanya kama hayatuhusu!
Ajabu, umma unapoendelea kujifanya hahuhusiki, utakuwa wa kwanza kulalamika kama katiba hii feki itapitishwa! Kwanini kungoja majuto kuwa mjukuu ilhali ipo kila fursa ya kupinga dhuluma na jinai hii? Tunaogopa nini iwapo tumeshuhudia nchi nyingine umma ukiingia mitaani na kuzuia jinai kama hii tunayotendewa? Je sisi ni kisiwa au kuna tatizo katika mkusanyiko unaoitwa Tanzania?
Je ni kwanini watawala wetu hawajali? Aliwahi kusema Earl Derr Bingers, “Careless shepherd make excellent dinner for wolf.” Yaani mchungaji asiyejali hugeneza kitoweo kizuri kwa mbwa mwitu.
Je ni kwanini umma wetu haujali? Imesemwa, “When is a revival needed? When carelessness and unconcern keep the people asleep,” Billy Ashley Sunday (1862-1935), mwanariadha maarufu na mwinjilisti wa kimarekani aliwahi kusema. Yaani, uamsho unahitajika pale kutojali kunapowafanya watu walale. Je watanzania hatujalala? Tuamke basi. Kuna kila sababu ya kukataa katiba feki nay a kifisadi iliyoandikwa na CCM. Tuna kila sababu na uwezo wa kufanya hivyo. Sana sana hatuna cha kupoteza bali hasara ambayo tutaipata kama tutaruhusu katiba hii ipitishwe kwa mizengwe, ulaghai na uchakachuaji ili kukidhi matakwa ya hovyo na hatari ya kundi dogo la watu ambao wameshindwa kuona mbele wakadhani wataishi milele.
Chanzo: Tanzania Daima Oktoba 8, 2014.
Kijiwe chawapongeza walokataa utwahuti
Baada ya wahishimiwa wenye akili kuliko Abunwasi kuwaliza matwahuti wanaohangaika kuchakachua katiba yetu kwenye Bunge Maalum la Kuula kule Dom, kijiwe kimeamua kuwatumia salamu za pongezi kwa kitendo hiki cha kizalendo na kishujaa.
Mijiinga anaingia akiwa amebeba gazeti la Wameipata Leo anaamkua na kusema, “Mmesikia jinsi Njaa Kaya na Sam Sixx walivyoingizwa mjini na wahhishimiwa waliotaka kuwaingiza mjini wasijue nao wana akili tena zaidi yao?”
“Kwa furaha nilo nayo kwa baadhi ya waja wenye taamuli kuanza onyesha njia, natoa ofa kwa yeyote atayekuja kijiweni hapa wallahi.” Mpemba anasema huku akitabasamu.
Mbwamwitu anadaka mic, “Wote wamenifurahisha isipokuwa Ali Kesi ambaye ameonyesha uzabazabina kama Joni Chibuda buda la kutupwa. Sijui kama akili zake ni sawa sawa. Maana ukiangalia alivyokuwa akijonyesha mzalendo kumbe hovyo.”
Msomi Mkatatamaa anaamua kutia daruga, “Nyinyi inaonekana hamuwajui wataka sifa na wachumia tumbo. Kwa ninavyojua visasi vya baadhi ya wanasiasa, nilitegemea Kesi angepiga kikesikesi kama alivyofanya.”
Kabla ya kuendelea Kapende anakwanyua mic, “Kwanini unasema ulijua atakavyopiga kura au mshirika mna uhusiano na ngurumbiri huyu?”
Msomi abwia kombe lake na kujibu, “Ni rahisi kujua ni kwanini alipiga kura hivyo. Kwa vile waliotishia kumnyuka walipiga kura ya kupinga, yeye badala ya kuangalia mstakabali wa kaya aliamua kupiga kupingana nao bila hata kujua kuwa suala lenyewe si la binafsi bali kikaya.”
“Hapo nimekupata.” Anajibu Kapende.
Mbwamwitu anamuuliza , “Umetosheka?”
Kapende anajibu, “Unaonaje? Unataka zaidi?”
Baada ya kuona utani unaanza kuharibu mada Mgosi Machungi anaamua kuokoa jahazi, “Sasa tinaweza kuanza kupumua kuwa huu upuuzi hautaruuusiwa upite kwa ajili ya kuhujumu sisi na vizazi vyetu. Sijawahi kuona mijitu inayofikii kwa matumbo kama hii. Mungu kweli si Asumani! Hawa waioamua kupiga kura ya hapana wamerejesha heshima ya uhishimiwa uliokuwa umeanza kugeuka uishiwa.”
“Tuanze kupumua! Unadhani hawa manyang’au na matwahuti wataacha mizengwe yao kutubambika mkenge ili waweze kujinusuru na vifungo huko tuendako kama tutapitisha chate letu wenyewe?” Anauliza Mipawa huku akiwa anamuangalia Sofia Lion Kanungaembe ambaye mara nyingi huwa ana bifu naye sambamba na Kapende na Mijjinga.
Kana kwamba walipeana ishara kuwa akiongea atajibiwa na Sofi. Sofi anakwanyua mic. “Uwe na adabu. Msipende kuita watu na heshima zao majina ya ajabu ajabu. Hivi twahuti kati yako na hao unaowatukana matwahuti nani? Shika adabu na adabu ikushike.”
Mipawa hangoji Kapende aliyekuwa akijanaa kujibu afanye hivyo. Anakula mic, “Watu na heshima zao ukiwaona utawajua au unaota mchana dadangu? Heshima na ukubwa wa mtu si cheo alicho nacho bali matendo yake. Kuna watu wadogo sana wasio na vyeo wala kazi lakini wana heshima kuliko hao wezi wanaotapanya njuluku zetu huku umaskini ukizidi kutumaliza. Kwangu mwizi hata hawe mkubwa kama tembo au awe na cheo kikubwa kama Sam Sixx ni mwizi tu.”
Kanji hakubaliana na mawazo ya Mipawa . Anaamua kula mic kumhami mshirika wake Sofia. Anasema, “Hata mimi pana taka tukana vatu howo howo. Hata kama kuba nafanya kosa dogo hapana tukana tusi kubakuba hiwo.”
“Kanji matusi unayajua au unayasikia. Hata hivyo, wewe una kosa gani wakati una uraia mia na moja?” Kapende anachomekea huku akigonganisha mkono na Mipawa.
“Nadhani kumjibu Kanji na Sofi mnapoteza majibu na muda wenu. Laiti ingekuwa kwao Bombay sijui kama Swahili iko pewa nafasi toa vazo kama Kanji pewa hapa kwa Swahili.” Mbwamwitu anabukanya Kiswahili cha Kigabacholi huku akimwangilia Kanji kwa dharau. Kanji anachekacheka japo moyoni anatukuta.
Mchunguliaji aliyekuwa bize akisoma gazeti anaamua kula mic, “Mimi pamoja na kuwapongeza hawa mashujaa wa ukombozi wa wachovu nasema. Laki tatu kuleni na kura wanyimeni ati! Yote tisa. Kumi namuonea huruma kiherehere Sam Sixx ambaye anajitia kuendesha show hii wakati mwenyewe yuko majukuu kwa mzee Joji Kichaka akitanua na vimwana, waramba viatu hata makalio na marafiki zake wakitanua.”
“Nadhani wanasharia waandae kesi dhidi ya hawa wafujaji walioruhusu njuluku za wachovu kuvunjwa kwenye upuuzi ambao sasa unapigwa chini na kuthibitisha uhalali wa umma. Kuna haja ya kupiga chini hiki kiini macho na kuonyesha ulimwengu kuwa wachovu wakijitambua na kuungana wanaweza kufanya lolote walitakalo kama jamii. Ni somo kwa walevi wa maulaji na madaraka wanaodhani kuwa walipo ni ujanja kiasi cha kupatumia kutetea uoza na upuuzi mwingine.” Anaongea Msomi huku akibofya ki-tablet chake.
Anabwia kahawa na kuendelea, “Kilichotokea kinapaswa kuungwa mkono na kuendelezwa hadi mwisho wa mapambano. Tukatae hii hujuma ya mafisi na mafisadi. Hawa mashujaa tuwaenzi, kuwahehshimu na kuwaunga mkono kuzuia kula ya maoni. Bila kuwazuia hawa matwahuti, wataendelea kuchezea njuluku zetu kwenye hujuma yao. How can a cabal of criminals enact a document of the people? Who authorized them to do so? Oh! Samahani nimepandisha mori kiasi cha kuongea ukameruni.”
Kijiwe kikiwa kinanoga si likapita shangingi la Sam Sixx. Kwa hasira na usongo si tuliamua kulikimbiza huku tukizomea tukitafuta kumnyofoa na kumtia adabu!
Chanzo: Tanzania Daima Oktoba 8, 2014.
Subscribe to:
Posts (Atom)


