How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Saturday 9 June 2012
Kikwete na aibu za kujitakia
Taarifa kuwa rais Jakaya Kikwete amezuiliwa kuwasililsha taarifa ya mpango wa Kujitathmini wa Umoja wa Afrika (APRM) ni pigo licha ya kuwa aibu. Kisa hiki kimemkuta Kikwete tokana na Tanzania kushindwa kuwasilisha ada yake ya kila mwaka kwa AU $ 100,000 kwa mwaka. Tanzania imeatamia deni lake hadi kufikia $800,000. Inashangaza kuona nchi inayoweza kusamehe wezi na majambazi kodi na pesa nyingine kujisahau kiasi hiki! Pesa iliyoiaibisha Tanzania ni sawa na pesa aliyolipa kashi waziri wa zamani wa Mali ya Asili na Utalii, Ezekiel Maige kununua nyumba. Pesa hiyo ni tone ikilinganishwa na ujambazi wa EPA au iliyopaswa kulipwa kwa kampuni ya Richmond. Huu ni ushahidi kuwa nchi yetu ni maskini wa mawazo lakini siyo pesa. Ingawa ni pigo kwa nchi, heri kashfa hii na aibu vimemkumba Kikwete ingawa siku zote ni mgumu wa kujifunza kutokana naye kuwa sehemu ya tatizo. Bila hivyo, waziri wa mambo ya nchi za nje hakuwa na kazi tena. Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment