Habari zlizotufikia ni kwamba mwenyekiti wa Jumuia ya Madaktari Dk Steven Ulimboka alitekwa na watu wa serikali na kumpeleka sehemu isiyojulikana ambako walimdhalilisha, kumtesa hata kujaribu kumuua. Ulimboka alikutwa na yote hayo kutokana na kusimamia haki za madaktari. Je kama serikali inatumia uhuni kama huu wahuni wa mitaani wafanye nini? Je kumuua Ulimboka ndilo jibu la migomo ya madaktari? Je huu si ugaidi unaotendwa na watu wanaopaswa kuuzuia? Tunalaamini uhuni na unyama huu unaofanywa na watu wanaokula la kulala kwa pesa ya umma na walioko kwenye ofisi za umma. Kwa tabia zilizoonyeshwa na serikali madaktari hawana haja kuiamini tena. Kadhalika madaktari waache tabia ya kuwaamini wanasiasa maana hawaaminiki na hawana maana. Ni juzi tu Ulimboka alipiga picha na rais Jakaya Kikwete alipoitwa pamoja na wenzake. Bahati mbaya madaktari walimchukulia serious Kikwete wasijue nyuma ya pazia Kikwete waliyekuwa wakicheka naye kulikuwa na yule ambaye yuko tayari kutuma watu wawatoe roho.
How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Wednesday 27 June 2012
Kumteka na kumtesa Ulimboka kuimarishe mgomo
Habari zlizotufikia ni kwamba mwenyekiti wa Jumuia ya Madaktari Dk Steven Ulimboka alitekwa na watu wa serikali na kumpeleka sehemu isiyojulikana ambako walimdhalilisha, kumtesa hata kujaribu kumuua. Ulimboka alikutwa na yote hayo kutokana na kusimamia haki za madaktari. Je kama serikali inatumia uhuni kama huu wahuni wa mitaani wafanye nini? Je kumuua Ulimboka ndilo jibu la migomo ya madaktari? Je huu si ugaidi unaotendwa na watu wanaopaswa kuuzuia? Tunalaamini uhuni na unyama huu unaofanywa na watu wanaokula la kulala kwa pesa ya umma na walioko kwenye ofisi za umma. Kwa tabia zilizoonyeshwa na serikali madaktari hawana haja kuiamini tena. Kadhalika madaktari waache tabia ya kuwaamini wanasiasa maana hawaaminiki na hawana maana. Ni juzi tu Ulimboka alipiga picha na rais Jakaya Kikwete alipoitwa pamoja na wenzake. Bahati mbaya madaktari walimchukulia serious Kikwete wasijue nyuma ya pazia Kikwete waliyekuwa wakicheka naye kulikuwa na yule ambaye yuko tayari kutuma watu wawatoe roho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
6 comments:
hao sio madaktari ni wahuni wenye shahada za kuiba kweli hivi sasa tuimarishe mgoma ili na yeye apate kujuwa kuwa walalahoi wanateseka na yeye yupo leaders club anakula bata.
walalahoi wanaoteseka mahospitalini wanaomtegemea yeye na wauaji wenzie je si ni wakuhurumiwa pia?
hao walomteka kutoka leaders club
wangelimkata shikio moja ili iwe funzo kwa madaktari uchwara kama yeye
Mtu kama huyu ni shetani kabisa, tafakri angekuwa ni rais wa nchi, kwa wale mnaotaka madikteta huyu angefit. Huwezikuwa na akili timamu utese wanadamu wenzio kwa taaluma yako inayogusa 1 kwa 1 afya na maisha yao halafu ukale bata bar. Ana ganzi ya moyo au ni vp? Yaani nna hasira!! angegoma basi akajifungia ndani mwake, kaenda kustarehe!! Basi kumbe pesa za kustarehe anazo, ina maana ana ziada, yaani nitatukana bure ya nguoni.
na wewe unaitisha mgomo?
well said na alipofikishwa hosp huo mgomo anaouimba ulitakiwa uanzie kwake nae asikie hali waliyo nayo wagonjwa. Angeachwa alale sakafuni bila huduma
Ningekuwa na uwezo ningeenda kusimama nje ya mlango wa ICU kuzuia daktari yoyote asiingie kumtibu na waendelee na mgomo wao ili na yeye ndugu zake wajisikie hopeless kama anavyotufanya sie makapuku tujisikie!!
Anon nyote hapo juu kama ni tofauti mmeongea utumbo. Nina wasi wasi haya ni mawazo ya mtu mmoja kibaraka wa CCM ambaye ananenepa kwa makombo ya akina Kikwete. Kugoma ni haki ya mtu ila kuzembea si haki. Kwanini muangalie maisha ya watu kupitia mgomo wa madaktari lakini mnashindwa kuuona upande wa pili. Ama kweli Tanzania ina miaka mingi kusonga mbele kutokana na kujaa wasaliti kama Anno wote hapo juu.
Kwani hapa hakuna maoni mbadala
lazima watu wote wa ku support wewe
na wewe ushaanza kula makombo ya chadema?
na wewe kwanini unashidwa kuangalia upande wa pili
well said na alipofikishwa hosp huo mgomo anaouimba ulitakiwa uanzie kwake nae asikie hali waliyo nayo wagonjwa. Angeachwa alale sakafuni bila huduma
Post a Comment