The Chant of Savant

Friday 5 July 2013

Kipanya na watawala mapanya walivyonufaika na ziara ya Obama

Kwa utani na uoni wa karibu kibonzo hiki kinaweza kuchukuliwa kama utani, kina ukweli usiopingika. Hebu fikiri kwa mfano kitendo cha Richmond-Dowans kubatizwa na kuitwa Symbion Tanzania tena ikazinduliwa na Obama. Hebu fikiria majizi kama Rostam Aziz eti naye kuwa miongoni mwa 'mabilionea' wa Tanzania waliokutana na Obama. Kituko zaidi eti na wezi kama Dewji nao walikuwamo. Kweli kwenye msafara wa mamba kobe wamo.

3 comments:

Jaribu said...

Wakati mwingine na hawa Wamarekani nao wana vijimambo. Hiyo Dowans ikauza mitamba yao mikweche Symbion ambayo mmoja wa waanzilishi wao ni aliyekuwa Balozi wa Marekani na ikapata baraka za Hilary Clinton alipokuja kutembea huko. Sasa hiyo Symbion nayo imesafishwa mpaka Obama kuitambua? Unless wana channel hela za CIA kwa sababu sitaki kuamini Marekani wanaweza kubariki wizi wa mali ya nchi wanazozipa misaada.

Hao "mabilionea" wa Tanzania sidhani hata kuna mmoja aliyepata hela zisizokuwa za wizi; labda Bakhresa ambaye wanamkejeli kuwa ni muuza maandazi.

Mtwangio said...

Mhango naamini na kudai kwamba tangu kuondoka duniani kwa Mwalimu Nyerere nchi yetu imegeuka kuwa kama myama mwenye manufuaa makubwa ambaye alikuwa akiwindwa kwa tamaa kubwa na wawindaji wa nyumbani na wa kimatifa na wawindaji hao wamefanikiwa kumuungusha mnyama huyo na sasa wamekuwa kama VULTURES wamemwangukia na kuuvamia mzoga wake na kuugombea kama tabia ya VULTURES walivyo kila mmoja wao anataka kuwahi kuchukua pande lake na kuna VULTURES wa nyumbani ambao walianza kuonekana tu mapema hata kabla ya Mwalimu Nyrere hajaondoka duniani na katika awamu ya pili walianza taratibu ilipokuja awamu ya tatu wakapamba kasi na hii ya nne wameshika kasi zaidi kama treni ya speed kali na kwa kushirikiana na VULTURES wa nje baada ya miaka kadhaa watausafisha mzoga wote na kuaacha ardhikavu.Nakumbuka mwalimu Nyerere alilamika kwa kuchimba madini ovyo ovyo bila ya kujali kwamba wajao tunawaachia mashimo matupu.

Taifa kama la marekani ambalo mpaka sasa hivi ndio bado ni super power linaongozwa na masilahi ya kulenga popote pale duniani na rais wa marekani anapigania masilahi hayo kwa kuyaridhisha mashirika makubwa ya kibiashara ambayo yanalenga na yana ramani ya utajiri wote wa nchi zote changa duniani kwa hiyo kwa ramani hizo ndipo rais wa marekani anazozitekeleza anapokuja madarakani kama vile wanapotekeleza matakwa ya viwanda vya kutengeza silaha kwa kusababisha migogoro ya kisiasa na kuanzisha vita kila nafasi inapopatikana ili wauze silaha zao na kufaidika na mali ghafi za nchi hizo kama yanavyoendelea maafa nchini Congo.

Kwa hiyo Obama hakuja kwa masilahi ya Tanzania wala wananchi wa Tanzania amekuja kwanza kabisa kwa masilahi ya nchi yake na yeye mwenyewe na kama ilivyo kawaida ya ufisadi wa nchi changa kwamba wanasiasa na wafanya biashara wakubwa wakubwa wanashirikiana kwa kuifisidi nchi kwa hiyo kuwepo kwa akina Rostam Aziz na akina Dewji ni maswala ya business as usual.Na hatujui nini Obama alichonunua au kupewa na serikali ya CCM mpaka atakapomaliza muda wake.tumeelewa umilikiji wa ardhi lukuki wa akina Carters,Clintons na Bushes sasa yeye hatujuia kafaidika na nini na nchi yetu bila ya wananchi wa Tanzania kufaidika nae kwa chochote kile au hata kujua kwa wakati huu.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Jaribu na Mtwangio mna hoja. Ni kweli Obama hakuja kwa maslahi ya watanzania wala si kwamba Marekani haijui kuwa Symbion Tanzania ni Richmonduli-Dowans. Wajua sana. Ila kwa vile taifa letu sasa ni kichwa cha Mwendawazimu mlevi kujifunzia kunyoa, wanabamiza na kuzoa bila kujali iwapo mataahira wetu hawastuki. Wanatanguliza chao cha mbele wasijue mbele yanaweza kuwa mauti. Nyerere alilinda raslimali zetu ili zitufae. Maskini hakujua kuwa watakuja wezi na majambazi wazigawe na kupewa chao ili wengine wajijue. Hapa wa kulaumu ni watanzania wenyewe kukosa msimamo na kutokuamua kusimamia mali zao. Nadhani hali ikiendelea hivi msishangae siku moja kusikia Ikulu imebinafsishwa mkawa na rais ina mhindi au mswahili kama Kikwete anayeamrishwa na kila kinyamkera. Kuna haja ya wenye uchungu na taifa letu kuvaa magunia na kujipaka majivu na kuanza kuomboleza. We are the nation of goons and buffoons so to speak shall this go on as it has always been.
Nawatakieni wikendi njema ndugu na marafiki zanguni.