Jana Kamanda Nkwazi Jr. alisherehekea mwaka wake wa kwanza. Si haba tulijumuika na kumkaribisha kwenye jamii ya kuhesabu miaka badala ya miezi. Taratibu ataanza kuachana na diapers na kufikiri kwenda kujiunga na vidudu wenzake. Happy Birthday Nkwazi Jr.
4 comments:
Hongera kwa kutimiza mwaka mmoja na mungu akujalie yote mema na uwe mtii kwa wazazi/walezi wako. Ni mimi shangazi yako.
Da Yacinta salamu zako zimefika kwa mhusika. Tunashukuru kwa kututoa kimasomaso. Tumefarijika kama wazazi na Mungu akulipe kwa niaba yetu.
Kila la heri.
Mwalimu Mhango nami nachukua fursa hii kwa kuwapeni hongera kama wazazi kwa kupewa na bwana Mola kiumbe ambacho mmefikia kusheherekea kutimiza kwake kwa mwaka wake mmoja.Naomba Bwana Mola ampe afya njema na uhai mrefu ukiambatana na kheri,baraka na mafanikio ili aweze kuja kuchangia katika dunia yetu hii kile ambacho alichoandaliwa na Bwana Mola.Pia namuomba Bwana Mola kwa nyinyi wazazi wake akupeni pia afya njema na uhai mrefu ambao atakuwezesheni kumlea kwa kumpandikiza maadili ambayo mtayaona yanafaa na kustahiki kwake na kumshika mkono na kumuongoza katika safari yake ya maisha mpaka ataposimama kwa miguu yake.
Ndugu yangu Mtwangio salamu zako zimefika na tunashukuru kwa dua zako kubwa inshallah subhanna mwenyewe atatujalia tena na tena. Nasi tunakutakia mafanikio katika shughuli zako na afya tele katika maisha yako.
Post a Comment