http://www.youtube.com/watch?v=aDci72DG9D4
Kumekuwapo na chokochoko kati ya Malawi na Tanzania na hivi karibuni Rwanda. Rais Jakaya Kikwete alikuwa kimya kwa muda mrefu hadi juzi tu alipoamua kupasua jibu kuwa atakayetuchokoza au kutuchezea "atanyukwa" kama Idd Amin. Kwa wanaojua diplomasia ni kwamba ngoma inogile na atakayeshindwa kuzingatia hili ajiandae. Uzuri ni kwamba katika viinchi vinayoleta unyonyo hakuna hata moja yenye kuweza kutulazama macho. Japo hatuombi , ikitokea mojawapo au vyote vikajiingiza kijeshi vitatupa sifa nyingine ya ziada zaidi ya ile aliyotuachia Amin baada ya kumfundisha adabu. Kwa kuangalia mfano wa Amin unapata hisia kuwa kikitokea kichapo si cha kushinda tu bali kuhakikisha nchi husika zinaangushwa na kuweka mtu wetu kama tulivyofanya Uganda. Hakika matamshi makali ya Kikwete ni mtihani kwa rais Yoweri Museveni wa Uganda ambaye amekuwa akimuunga mkono protege wake Paulo Kagame. Je Kagame atajibu mapigo au kunywea ili angalau aendelee kula? Kagame alikaririwa hivi karibuni akiwa mpakani mwa Tanzania kwenye mji uitwao Mulindi akitoa vitisho vya kumshikisha adabu Kikwete. Naye Kikwete katumia njia hiyo hiyo ya kujibu akiwa Kaboya karibu na mpaka wa Rwanda. Wachambuzi wa mambo tuko msituni tukichimba na kuchimbua tuone la kutokana nalo katika sekeseke hili. kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.
1 comment:
Huyu anataka kutupumbaza tu tusahau ujuha wake. Juzi juzi ilikuwa Malawi, leo Rwanda, kesho Uganda. Ingekuwa watu wanaenda vitani kwa kuwa watu wanakusema vibaya basi Marekani wangepigana na nchi nyingi duniani. Ya kwake yamemshinda anataka akawapatanishe Wanyarwanda.
Huyu Iddi Amini mwenyewe amefufuliwa na wakina Kikwete kuwa Nyerere alimuonea kwa sababu Muislam. Leo anamponda.
Post a Comment