Hatimaye rais Jakaya Kikwete ametangaza mabadiliko katika bazara lake la mawaziri. Wengi walitegemea mabadiliko kama lilivyo jina la baraza lenyewe ingawa halina mabadiliko. Wengi walitegemea mawaziri waliotwaja na wakubwa wa Chama Cha Mapinduzi kuwa mizigo wangeachia ngazi. Lakini hili halikutokea. Cha mno kilichojitokeza ni kujenga mazingira mapya ya kashfa nyingine ya EPA hasa ukiangalia kupelekewa kwa watu kama Mwigulu Nchemba na Adam Malima ambaye anajulikana anavyotumia jina la baba yake kuendelea kukaa serikalini hata kama anafanya madudu.
Majina ya watoto wa vigogo yameendelea kuwamo kwenye baraza la mawaziri. Wamo Januari Makamba, Hussein Ali Hassan Mwinyi na Malima. Limeibuka jina jipya la ndugu wa kigogo nalo ni Mahamoud Mgimwa. Kujuana na majina mazito vinaendelea kulitafuna taifa letu.
Kimsingi alichofanya Kikwete ni kuthibitisha alivyo bingwa wa sanaa na mhimili wa sera na utawala wa kulindana.
Mwaziri waliotajwa kuwa mizigo ni Jumanne Kawambwa, Christopher Chiza, Malima, William Mgimwa (sasa marehemu) bila kusahau wengine kama Hawa Ghasia. Pia kuna mawaziri waliojitokeza kuwa mizigo kweli kweli hata kama hawakutajwa lakini wanaendelea kupeta. Hawa ni Maprofesa Jumanne Maghembe na Anna Tibaijuka, Mary Nagu, William Lukuvi, Stephen Wassira, Mathias Chikawe, Sofia Simba na wengine wengi ambao wameendelea kupeta. Kweli la kufa halisikii dawa!Sura ya baraza lenyewe inaonekana hapa chini.
- UHAMISHO NA UTEUZI WA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI
______________________________ ________________
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewahamisha na kuwateua baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:-
1. OFISI YA RAIS
Hakuna mabadiliko.
2. OFISI YA MAKAMU WA RAIS
2.1 Waziri wa Nchi (Muungano) - Hakuna mabadiliko
Mhe. Eng. Dr. Binilith Satano MAHENGE (Mb)
Waziri wa Nchi (Mazingira).
Mhe. Ummy Ali MWALIMU (Mb)
Naibu Waziri
3. OFISI YA WAZIRI MKUU
Hakuna mabadiliko
4.0 WIZARA
4.1 WIZARA YA FEDHAMhe. Saada Mkuya SALUM (Mb)
Waziri wa Fedha
Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA (Mb)
Naibu Waziri wa Fedha (Sera)
Mhe. Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb)
Naibu Waziri wa Fedha
4.2 WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Hakuna mabadiliko
4.3 WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
4.3.1 Mhe. Dkt. Asha-Rose Mtengeti MIGIRO (Mb)
Waziri wa Katiba na Sheria
Naibu Waziri - Hakuna mabadiliko
4.4 WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
Hakuna mabadiliko
4.5 WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA
4.5.1 Waziri - Hakuna mabadiliko
4.5.2 Mhe. Janet Zebedayo MBENE (Mb)
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
4.6 WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA
Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (Mb)
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
4.7 WIZARA YA UJENZI
Hakuna mabadiliko
4.8 WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
4.8.1 Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb)
Waziri wa Mambo ya Ndani
Naibu Waziri - Hakuna Mabadiliko
4.9 WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
Mhe. Dkt. Seif Seleman RASHIDI (Mb)
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
Mhe. Dkt. Kebwe Stephen KEBWE (Mb)
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
4.10 WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
4.10.1 Waziri: Hakuna mabadiliko
4.10.2 Mhe. Jenista Joakim MHAGAMA (Mb)
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
4.11 WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO
4.11.1 Waziri: Hakuna mabadiliko
4. 11.2 Mhe. Dkt. Pindi Hazara CHANA (Mb)
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
4.12 WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI
4.12.1 Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Dismas KAMANI (Mb)
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Mhe. Kaika Saning’o TELELE (Mb)
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
4.13 WIZARA YA KAZI NA AJIRA
Hakuna mabadiliko
4.14 WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Hakuna mabadiliko
4.15 WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
4.15.1 Waziri - Hakuna mabadiliko
4.15.2 Mhe. George Boniface Taguluvala SIMBACHAWENE (Mb)
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
4.16 WIZARA YA MAJI
4.16.1 Waziri - Hakuna mabadiliko
4.16.2 Mhe. Amos Gabriel MAKALLA (Mb)
Naibu Waziri wa Maji
4.17 WIZARA YA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA
4.17.1 Waziri - Hakuna mabadiliko
4.17.2 Mhe. Godfrey Weston ZAMBI (Mb)
Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
4.18 WIZARA YA UCHUKUZI
Hakuna mabadiliko
4.19 WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
4.19.1 Waziri - Hakuna mabadiliko
4.19.2 Mhe. Juma Selemani NKAMIA (Mb)
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
4.20 WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
4.20.1 Mhe. Lazaro Samuel NYALANDU (Mb)
Waziri wa Maliasili na Utalii
4.20.2 Mhe. Mahmoud Hassan MGIMWA (Mb)
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
4.21 WIZARA YA NISHATI NA MADINI
Waziri - Hakuna mabadiliko
Naibu Waziri (Madini) - Hakuna mabadiliko
4.21.3 Mhe. Charles Muhangwa KITWANGA (Mb)
Naibu Waziri (Nishati)Balozi Ombeni Y. Sefue
KATIBU MKUU KIONGOZI
Ikulu
DAR ES SALAAM
19 Januari, 2014
2 comments:
Kuna wakati nilikuwa nasikiliza nyimbo ya Bendi ya watu kutoka Kongo-Kinshasha(Mboga mbele, ugali nyuma-Keko Mahubusu wana Kibinda Nkoi) ni Mtu wa kutoka Taifa la Tuliopata uhuru karibuni sawa tuu huko Asia...
Basi huyu Bwana akaniambia hii ni kama wananchi wako na viongozi wake wote wanacheza hiyo Kibinda Nkoi.....Hii kauli inaendelea kuniumiza kila siku naposikiliza hizi nyimbo za uteuzi wa Mawaziri.
Kimsingi kutakuwa na taasisi mahususi kabisa ndiyo yenye matatizo makubwa yanayoleta shinda kupata watu/viongozi sahihi wazalendo wa taifa...
Maana hivi juzi nilikuwa nikisoma habari mitiani kidato cha pili mwaka 2012 kuhusu, hakuna hata mwanafunzi aliyefeli mitihani na matokeo yake hatutayaona. Lakini waziri husika wa wizara ya Elimu yupo kama kawaida....
Anon una maanisha kuwa hatubadiliki kiasi cha kuwa na wimbo mmoja kama wa jogoo siyo? Nakubaliana nawe kwe vile hata ukiangalia kinachoitwa baraza la mabailiko halina madiliko zaidi ya maanguko. Nangoja kusikia CCM imeiba pesa nyingine kwa ajili ya uchaguzi. Nikiona hizo sura mbili yaani Nchemba na Malima sina raha.
Post a Comment