- Wanaosema rais Jakaya Kikwete ni msanii hawakosei. Je hapa ana tofauti na marapper katika miziki ya kizazi kipya? Ukichanganya na "ujana" wake ambao ameu-maintain na kupata rangi nywele ili mvi zisionekane ndiyo usiseme. Nimependa staili yake ya kwenda na wakati ingawa si katika ofisi yake ambayo ameamua kuitelekeza akipendelea kusafiri ambao wabaya wake huita kuzurura.Wakati ukututa ukifika hugota. Pamoja na jitihada zote, hapa uzee unaanza kujitokeza hata kama haukaribishwi. Mzee hapa hajapita saluni kupigwa soap soap aonekana kijana. Gaddafi alizoea hata kupiga wigi ili aonekana wamo wakati alikuwa kibabu!Jamaa kwenye boxing yumo. Msanii lazima amudu sehemu zote. Hata kubembea ni sanaa. Au vipi?Jamaa hajasahau vikwata wakati wa udogo wake.
Je hapa nani katunga? Hata hotuba za kuandikwa zaweza kuwa kitabu cha kujisifia kutunga? Je jamaa atapata muda wa kusoma haya matabu ambayo kimsingi ni maadui zake wakubwa? Kama kawaida, msanii hapa anaonekana bonge la somi.
3 comments:
Kuhusu hayo ma-hotuba yaliyochapishwa kama inahewsabiwa kuwa na mafanikio basi ni sawa na haidithi ya Katope(Nategemea utakuwa unaikumbuka hii hadithi Dr. NN Mhango)
Kuhusu hayo ma-hotuba yaliyochapishwa kama inahewsabiwa kuwa na mafanikio basi ni sawa na haidithi ya Katope(Nategemea utakuwa unaikumbuka hii hadithi Dr. NN Mhango)
Anon
Naikumbuka sana hadithi ya Katope mtoto aliyeogopa maji akaishia kumomonyolewa na mvua. Au ni ile ya fimbo mchape mbuzi mbuzi anywe maji na maji ya mwagikie Katope....?
Angalizo, ingawa nina mpango wa kufika huko, bado sijawa Dr. Naogopa udokta wa akina Njaa Kaya.
Post a Comment