How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Thursday, 13 February 2014

Swali la leo: Iweje Faru na Tembo wauawe Bongo kampeni London?

Ivory destruction
Pesa ya wizi, ufisadi, rushwa, unga na ujangili wanaficha London.
Safari za kikazi wanafanya London.
Kampeni ya uzazi wa mpango London.
Mikutano ya uwazi London'
Kampeni ya kuangamiza ujangili London.
Je ni kwa nini au ni kwa vile hawa jamaa ndiyo waliotutawala?
Je ni roho kuwasuta wahusika ambao walirithi faru na tembo kibao toka kwa wakoloni?
Wakoloni walikuja wakatuibia lakini walikuwa na akili wakatubakishia.
Sisi tulipopata uhuru ambao umegeuka udhuru tumejitahidi kujiibia na kumaliza kana kwamba hakuna vizazi vijavyo. Sijui ndiyo huu uvivu wa kufikiri au kufikiri kivivu! Sijui ndiyo huko kuishiwa au sanaa za kuwaweka sawa wafadhili majangili ya ofisini na mbugani yakaendelea kupeta?
Nukuu ya leo ni toka kwa Mchungaji Peter Msigwa Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA).
Alikaririwa hivi karibuni akihoji,“Inakuwaje mtu anayevunja sheria za nchi hakamatwi. Waziri Nyalandu amekuwa mlalamikaji badala ya kutafuta suluhu, majibu yake na ya Serikali ya CCM yanadhihirisha kuwa mtandao huu unaogopwa unaihusisha Ikulu, wanasiasa, polisi, maofisa wanyamapori na wanajeshi.”

2 comments:

Anonymous said...

African Continent needs officially declaring that unable to lead by themselves and accepting were not yet civilized to demand for independence at that time, in which the solution is to invite back re-colonisation to the whole continent.

African leaders have not got anywhere near to start retain Good Governance.

I know it could sound to hash from the people lost their bloods during the struggle for independence but Surely we can not walk out from the fact and thruth.

Anonymous said...

Mbona mambo
Kuna Watu wamesifia hotuba ya mkuu London
Jamani Kama ulivyosema Tembo bongo mkutano London
Haya tusubiri mkutano wa winter games ufanyike bongo
Hongera mchungaji msigwa sema yote
Kwani vigogo wa CCM ndo Wauwa Tembo wetu
Kiama chenu 2015 mtaondoka na wachina wenu