How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Saturday, 31 January 2015

Well done doyen Kingunge!

          Believe me. Our hunk’s currently facing a crazier atmosphere altogether. It is bracing itself for general elections come October when Jake Kiquette’ll hit the road and allow others to come and clean his jumble. Whoever comes in has a lot to do especially at this time our hunk’s grappling with the grip of grafts and all sorts of criminalities committed by the high and the mighty. Before po-faced Kingunge Ngombale-Mwiru  dropped the bolt from the blue in his no-nonsense style, some old-school followers and fans of Chama cha Maulaji (CcM) were wee bit confused about whom they’d entrust their votes come next general elections shan't they turn to be charade aka uchakachuaji. At this time of eating, without sweating, without washing hands, and eating with hands and legs, a vote’s a precious thing. For, without it, one’s left in the cold. So, every eater wants to get a vote so as to take a dip in a gravy train. Here’s where one-upsmanship pays if those targeted aren't vigilant and gallant.
          Without mincing words, Kingunge said that all those CcM top dogs you hear hooting for presidency, are unfaithful, corrupt and use suspicious dosh to vie. If anything, this is the boldest stance ever been taken by CcM’s doyen-cum-cadre.  
          Frankly, Kingunge wants bin-Adams in the hunk to sever the nexus with CcM and look somewhere else, opposition of course, for the coming president who’ll be charged with cleaning the house after long time rule of misrule. Kingunge knows all like his palm. They’re crooks and rent-seekers he doesn't want you to goof voting for while they’re going to vend you.
          Before philosophizing even more, I must doff my hat for Kingunge for openly telling all those who want to coff presidency so that they can easily make dosh without doing anything.
          Kingunge added, “Frankly, when we look at all those making announcements, there is no even a single clean person… we can’t elect president as if we looking for footballer. It’s impossible,” In a simple parlance, as Mwl Mchonga once quipped, all those you see buying votes are bought. According to Mchonga, all these dudes you see making noises have already been bought by their masters who’ll use them after you commit sacrilege and hand ulaji over to them. Beware then. If their inventors and minders have already lost faith in them, then what are you looking for to vote for them?  Ogopa yeye kama ukoma. If we go by Kingunge and Mchonga’s tipoffs, the truth’s likely to be that most of those you see trying to dupe you may be spending dosh obtained from drugs, escrow, and all sorts of criminalities.
          Given that Kingunge, just like mzee Jose Warioba, wants to leave behind a very good legacy, it isn't easy to state if it’s the end or the beginning of reigning in even more shall those hard-heard creatures persist to see to it that they dupe boozers. Mzee, Kingunge, please don’t stop giving them their awesome pills. Boozers have already vowed to kibble them. No quibble about that. Given that the ulaji season is approaching, we’ll witness many fission and fusion in the old order whereby horse and insult trading will be the in-thing. Books will be written, some stating nothing but praise singing. Hired pen and hit-pen will be at work to see to it that dosh is made and power is grabbed. It is upon boozers to weigh and even things making sure they know what’s right and what’s wrong for them.
          Now that the ulaji seekers are pulling strings and pushing buttons to see to it that they land ulaji and eat gluttonously there after. Once this happens, all those who enabled them are forgotten. Shall they try; they face what the Geita boys faced. You see. Some have already put a spin on things so as to commission some people to author books singing praise of them. Given that Bongolalalanders are good imitators, soon you’ll see many logical and illogical books in shelves even if there’s nobody to buy them.  Remember Tumaini lililorejea and then likapotea? Where’s the dude that wasted honour and time to author such a nugatory book?  Some boozers told me that the guy’s promised a post of envoi to a certain hunk that’s why he dressed himself down. Again, after being punched under the belt, he ended up being disenchanted blaming his myopia and greed. Dosh makers like tomatoes are on the hunt to eat money from those who eat them. It is a dog-eat-dog thing.
          Time for con men to reap where they didn't sow is now. All in all and above all, all this biz is about using you as a step to ulaji. So, too, you need to know that the said ulaji is that of eating you. I’m hoping they’ll continue their visits throughout the winter-for our pleasure,” this quotes comes from the book Birds of a feather-Mary Krueger. The birds I mean here are politicians and the winter, campaigns. Will they? Forget. The jig is up.
Source: Guardian Feb., 1, 2015.

Mlevi aonya: Mwaogelea vinyesini mwajiona!

          Shalom le kulam,
Kila mvua zikinyesha kwenye jiji la Bongosisalama wataalamu wa ushenzi nao huonyesha sayansi yao ya kufungulia maji ya vyooni na kuchanganyikana na ya mvua ili kukwepa gharama ya kunyonya vyoo. Ni bahati mbaya kuwa huu mchezo umekuwa ukiendelea pamoja na madhara yake kiafya kwa walevi. Sijui hili nalo linahitaji wafadhili au wataalamu wa jinai kulitambua ili wahusika wachuke hatua? Je hawa wanaonyamazia maangamizi haya kwa walevi wanafaidika vipi kutokana na jinai hii au ni uzembe tu na ujinga n ahata upumbavu wa kutotambua kuwa magonjwa huvuruga mipango ya kaya ya maendeleo? Hata hivyo nani anajali iwapo maendeleo kwa wakubwa walio wengi ni wao kupata hata kama ni kwa kuwauza walevi na raslimali zao kama ilivyo?
Siku moja mlevi mwenzangu, baada ya kupiga mibangi aliniacha hoi nilipokuwa nikilalamika baada ya kurejea Uswekeni toka Kariakoo baada ya kuogelea kwenye mavi yaitwayo maji ya mvua. Baada ya kufika zangu kwenye baa ya Mama Coltide na kupata kanywaji, nilipoanza kunywa nikasikia kama harufu ya kinyesi vile. Nilidhani mwenzangu alikuwa ameachia hewa mbaya. Baada ya kumvaa nikimtaka aache kuachia hewa mbaya kwenye kadamnasi, naye alinikaba akisema alidhani mie ndiye nilikuwa nimeshua (kwa kisambaa) yaani kutoa hewa mbaya.  Kwa vile tunapendana na kuheshimiana na huyu mlevi mvuta bangi, ilibidi tutafute chanzo cha tatizo la harufu mbaya.
Jamaa aliniuliza kama nilikuwa nimekwenda Kariakoo siku hiyo. Baada ya kumwambia kuwa nilikuwa natokea kule, alisema, “Hakuna haja ya kukamatana uchawi wala kutoana macho. Kumbe hujui kuwa mvua imenyesha leo na umeogelea kwenye maji ya chooni!”
Ugomvi wetu uliishia pale jamaa alipojisemea, “Lisirikali linaona lakini haioni.” Nilipomuuliza alimaanisha nini kusema kuwa lisirikali linaona lakini halioni, alijibu kuwa tatizo linajulikana sema wakubwa hawataki kulifanyia kazi tokana na kuwa bize kwenye kupiga dili kuanzia escrow hadi bomba la gesi.
 Hivyo, tuligundua kuwa tatizo linajulikana lakini kila anayehusina anajifanya kutojua kuwa lipo.
Ukiangalia wakazi wenyewe wa katikati ya jiji na mambo yao ya kutia shaka, unashindwa kuelewa uanzie na kuishia wapi. Mambo fanyika kama iko Bombei! Veve iko soma Mahabharata? Iko jua Ugrasrava Sauti au Bhagavad Gita?  Basi kama iko jua sunskrit basi tafsiri hii Theudorena meridarkhena pratithavida ime sarira sakamunisa bhagavato bahu-jana-stitiye. Hebu tuache hindi. Mijitu kwa ubinafsi na ujinga hata ukatili linafungulia maji ya chooni lisijue kuwa magonjwa hayachagui. Nalo laweza kuugua hata kunyotoka roho. Je ni wangapi wanaliona tatizo hivi? Hata hivyo, tusishangae. Kama watu wananywesha maji ya chooni kwa kuhadaiwa kuwa ni ya kisima, unategemea nini?  Anayebisha kuwa hanywi maji ya chooni hasa kwa wakazi wa jiji wanaotumia ima maji ya visima au mizega ajitokeze nimuelimishe.  Hebu nikuulize japo kilevi. Je unajua hawa vijana wanaouza maji kwenye mizega wanapoyachota? Usiniambie kuwa wanayachota kwenye mito iliyotapakaa Dar ambayo mingi yake imejaa uchafu wa viwandani na majumbani bila kusahau kinyesi. Kama wanachota huko basi wewe unayenunua jua unakula uchafu tu taka usitake. Juzi juzi nilizurura kwenye kaya jirani kuanzia kwa kaya ya Nyayo hadi kule walikonyongana kwa mapanga. Guess what. Nilikuta miji yao mikuu ina maji ya uhakika safi na salama. Je sisi tulirogwa na nani ambao pamoja na kuwatangulia wenzetu kuunyaka uhuru kutokuwa na maji ya uhakika? Je wajua kuwa katika kaya hizi hata umeme si aghali wala wa mgao kama kwetu? Ajabu ya maajabu wenzetu hawana vyanzo vya umeme kama vyetu tunavyotukana kwa kutovitumia! Umeipata hiyo? Kama hujatosheka sema nikupe dozi nyingine.
Turejee kunywa, kufulia, kuogea na kuogelea kwenye vinyesi.FYI kama unategemea kunywa, kufulia, kupikia hata kuogea ujue huna tofauti na inzi. Tofauti ni kwamba inzi ni mdudu. Hana akili wala nguvu ya kujikomboa na kujiondoa kwenye kadhia hii tofauti na wewe unayetenzwa kama mdudu wakati u mja. Tunazidiwa na mijuzi ambao hunywa maji ya mvua na si ya vinyesi! Ni ajabu kuwa mvuta bangi na mlevi anaweza kuliona hili wakati wale wanaojifanya wazima hawalioni! Mtaendelea kunywa maji ya chooni hadi lini kwenye karne ya 21 au ndiyo maisha bien yenyewe mliyoahidiwa?

Usitake kunitapisha kusema eti hayo ndiyo maisha poa na mswano mliyoahidiwa na wasanii wenu. Yangekuwa hivyo, wengine wangeishi kwa kuiba maji na umeme? Kwani hatuwajui? Sijui na zoezi la kunyaka vishoka wa umeme na maji nalo limeishia wapi. Hata hivyo, kama tutasema ukweli, nani amkamate nani wakati naambwa kuwa lisirikali ndilo linaongoza kwa kutolipa ankara za umeme na ma-water? Ama kweli jogoo aliwafundisha vifaranga kunya ndani! Unategemea nini toka kwa lisirikali ambalo waingereza huita sitting duck au bata aatamiaye? Ikizidi ikipungua wale wanene wanaokalia uchumi huitwa lame duck, kwa kisambaa. Hakuna kilionikera kama kusikia kuwa kuna wadhiri mzima wa Ma-water wakati hakuna ma-water kayani. Je huyu analipwa kwa kazi ipi iwapo walevi wanaogelea kwenye vinyesi kama inzi?  Ajabu waziri mwenye eti ni prof. Prof au porofedha kama siyo profedheha kama wale wa escrew au yule aliyejificha nyuma ya kampuni jambizi la Uda huku akiwatangulia matapeli wasio na hata nduru wakijifanya ndio wenye mali wakati wenye mali hii ya ufisadi wanajulikana. Hayo tuyaache. Nadhani huyu angeitwa wadhiri wa, vinyesi, sorry, mabomba yasiyotoa maji. Au tuseme waziri wa kukusanya malipo bila kutoa maji.
Chanzo:Nipashe Januari 31, 2015.

Vasco da Gama anapokula buku!

Jamaa anasoma au mkwara na kutaka apigwe picha? Kwa wanaomjua huyu jamaa, hakuna kitu asichopenda kama kusoma. Hata kabla ya kuwa rais alisifika kwenda kwenye kumbi za muziki na mambo mengine kama hayo. Alijua kukaa kwenye vijiwe vya mpira na kusogoa zaidi ya kujisomea hata kujiendeleza.  Ukitaka kujua hofu inatoka wapi, jiulize swali rahisi. Mbona walio karibu naye wote hakuna anayesoma isipokuwa yeye? Kitu kingine, angalia wingi wa walaji alioandamana nao. Hao ni wale wanaoweza kupewa viti. Bado wapiga picha uchwara na wasaka sifa ambao wamegeuka fisi  wasiobanduka kila alipo simba. Fedha ya umma inafujwa kwenye upuuzi kama huu kila uchao. 

Tuesday, 27 January 2015

Letter to Mayardit and Machar

          Dear your Excellency Salva Kiir Mayardit the president of the republic of South Sudan (RSS),
Dear Dr Riek Machal leader of rebels,
          I hope you are fine, and now you can sleep peacefully after signing a peace agreement in Ngurdoto Tanzania. I salute you. True, the whole region welcomes this breakthrough. May God add grandeur and blessings.  Reaching such a juncture after fighting for a long time is recommendable and welcome, especially, for the people of South Sudan. I understand. You both, hand-in-hand, fought for the emancipation of your esteemed nation referred to as the youngest nation of the world which it is. Again, you country is young but you are not.  This being the case, your maturity is an asset for the young nation shall you respect those signatures you appended on the agreement recently. Please, live up to your words.
          Ngurdoto accord is the third. Prior you signed two accords you ended up breaking. I implore you.  Please, no failure of the accord should be repeated. Africans have it that strong evidence stands three times. Three times becomes a good number in order to give a person the atmosphere of learning from his mistakes. I hope this applies to you. Therefore, this last or third time you appended your signatures, shall be violated, it means, you'll be sending your noble and young nation to purgatory wantonly and pointlessly. It should nary happen. The blood you shed during fighting for your nation wasn't in vain. But the blood shed due to your difference, if bloodletting isn't stopped, will haunt all of you so much so that whatever any of you aspires for in power won’t become meaningful or successful. Human blood is different from the blood of animal's. It is sacred and blessed. It is not supposed to be spilled without any necessity or reason.
          Gentlemen, when you gained your independence through separation after fighting for decades, we, your brothers and sisters were happy. We knew the lengthier and tougher thoroughfare you journeyed to reach at the point of breaking away. We evidenced your torments, ire, angst and predicaments. We were thrilled when you fulfilled your dream of becoming a nation. Again, when you turned noble guns you used to fight for the nation against one another, those who tortured you and despised us for celebrating your rebirth, were happy some telling , “You see, these guys can`t do anything for themselves.”   They kept singing the same song of calling others slaves and many more bad names. Please, stay put in the vision of making a peaceful nation by avoiding warring pointlessly.
          Gentlemen, I full understand the responsibility you have on your shoulders for both sides. Please don’t allow trivial and tribal sentimentalities drift you away for the peril of the nation. Those brothers and sisters, who, for three times, offered to mediate, have a lot of things to do. They won’t get time every time you fight. Don’t make them become tired of you. Use them to forge ahead instead of wasting time fighting and causing mayhem pointlessly. The world will laugh at you when your people starve and face stagnation economically, politically and socially. Please sit together and devise how to utilize the gifts of resources God gave you. Please show your patriotism and the lesson you got from past mistakes. Reinvent your image as people and a nation by shunning tribalism, regionalism, cynicism and other trivial things. Time will nary wait for you especially at this time the world is running while you butchering one another. Wars have nary built any empire save to bring it to its knees. This is not the way to go for wise and courageous people like you.
          Gentlemen, the women of South Sudan are tired of burying their children and husbands. Children are tired of burying their fathers. People are tired of burying their kinship. Even birds and other wild animals are tired of hearing gun shots. South Sudan is crying wanting you to heal her from megalomania of in-fighting and greed for power. South Sudan is whining and shrieking for her children. She is bleeding to death due to the injuries inflicted by her own children. Who bewitched you brothers? God created one South Sudan for all of you equally. Therefore there won’t be any South Sudan for some of you by excluding others. God doesn't apply  Exclusionary edict or apartheid. South Sudan is for all Shuluk, Kakwa, Dinka, Didinga, Nuer, Luo, Toposa, Lotuho and all other communities equally regardless the size of the  population of one community compared to another or others. You fought for the nation as one people. You will always live as one people.  Your motto should be:  South Sudan, One people instead of South Sudan, Many People or Divided Communities. It doesn't work and it can’t work.  The leitmotif of war doesn't help anything except dressing you down.
Gentlemen,
          Allow me to end up here saying, enough is enough. This time prove your detractors wrong as you make your people happy and safe in a peaceful country.
Long Live South Sudan
South Sudan, One People
South Sudan, One Spirit
South Sudan, One Body
South Sudan, One Mission
South Sudan, One Destiny

That is my contribution.
African Executive Magazine Jan., 2015.

Mfumo fisadi usiwatoe kafara askari wetu

Wakuu wa Jeshi la Polisi wakikenua baada ya kutupia cheki na fisadi Harbinder Sethi Singh mwizi wa escrow

         

          Tanzania sasa iko msambweni. Inatenzwa kana kwamba haina viongozi, na kama wapo, hawaoni wala hawasikii, ukiachia mbali kutofaa wala kujihangaisha kupambana na majanga yanayowakabili umma ambao sasa ni yatima.     Kuvamiwa kituo cha polisi cha Ikwiriri, Pwani hivi karibuni na wanaosemekana kuwa majambazi ni kiashiria cha uoza wa mfumo fisadi. Askari wawili wanaofanya kazi kwenye mazingira magumu waliripotiwa kufa huku bunduki saba na risasi 60 ambazo, bila shaka, madhara yake yatakuwa makubwa baadaye zikiibiwa. Inashangaza polisi wanaopaswa kulinda usalama wetu nao si salama. Je hapa nchi ni salama? Ajabu hata kadhia hii ilipotokea, serikali haikuja na tamko stahiki lau kuonyesha kuwa kuna serikali. Je kuna magenge ya watu yanayotaka kuingia msituni kama ilivyowahi kudaiwa na baadhi ya vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa bunge la katiba wakisema kuwa kama rasimu ya jaji Warioba ingepita wangeenda msituni? Je hawa siyo sehemu nzuri ya kuanzia upelelezi? Je kuna kitu watu hawa wamenusa kiasi cha kuanza kujiandaa au ni matukio tofauti? Jikumbushe kauli za John Komba, mbunge wa Mbinga na William Lukuvi (Ismani)? Ni bahati mbaya. Hata waheshimiwa hawa walipotoa madai hatari kama haya, hawakuhojiwa kwa vile ni vigogo wa chama na serikali.

          Ifahamike kuwa Ikwiriri si kituo cha kwanza wala mwisho cha polisi kuvamiwa. Ilishatokea kule Mkamba Kimanzichana na Bukombe Geita. Kinachogomba ni kwanini serikali, hata baada ya kuvamiwa kituo cha kwanza, haikuchukua hatua kuzuia kurudiwa kwa jinai hii kama hakuna namna? Unaweza kutoa hitimisho lolote hasa ukizingatia kinachofanyika kwenye kushughulikia kashfa za wizi wa mabilioni ambapo baadhi ya wezi wanaonekana kutoguswa hata wakitenda jinai kiasi gani. Hawa wanashindwa kuanza kuanzisha majeshi yao?

          Ukivuka mpaka ukajielekeza kwa kinachofanyika Nigeria ambako kundi la Boko Haram linaihenyesha serikali au Somalia ambapo al-Shabbaab wanaipa hali ngumu serikali nchini humo na nchi jirani ya Kenya, unaweza kujua ninachomaanisha hapa. Hata haya makundi kama al-Houthi kule Yemeni, al Qaeda Maghreb na mengine mengi yalianza hivi hivi.  Je wizi huu wa silaha toka vituo vya polisi unaashiria nini kwa taifa ambalo liko msambweni kutokana na kukosa uongozi makini na wenye visheni?

           Zama za awamu ya kwanza, kitu kama hiki kingetokea, mipaka yote ingefungwa na wahalifu hawa wangesakwa na kutiwa adabu. Lakini sasa nani afunge mipaka wakati watu wameziba masikio wakihangaishwa na wizi wa fedha za umma na kuusaka ukuu bila kuwa na ajenda yoyote ya kuufayia umma zaidi ya kuibia na kuutumia watakavyo kama ambavyo imezoeleka kuwa urais kwa sasa ni kijiko kikubwa cha kuchotea utajiri kwa mwenye kuwa nao pamoja na familia, marafiki, hata waramba viatu wake?

          Kwa matukio haya matatu ya kuvamia, kuua askari, kupora silaha, kuharibu mali ya umma, kuruvuga amani, kutenda jinai, kumilki na kutumia silaha kinyume cha sheria na kutishia usalama wa taifa, ni ushahidi kuwa taifa letu si salama tena. Kama tunashindwa na magenge ya wahalifu wawe wanatumwa na wakubwa wanaotishia kwenye msituni au wanasukumwa na jinai yao, je tukivamiwa na taifa jingine tutafurukuta kweli? Inakuwaje tunapata polisi wengi wa kuwapiga wapinzani na waandamanaji lakini tunakosa hata polisi wa kujilinda?

          Uvamizi wa vituo vya polisi licha ya kulidhalilisha jeshi la polisi, unatishia maisha ya askari wetu ambao hawakwepi lawama kwa kujiruhusu kutumika kisiasa huku maslahi na usalama wao vikiwa hatarini.  Ili kuwa salama askari wetu wanapaswa kuasi na kuacha kutumiwa kisiasa kama walivyofanya wenzao wa Tunisia, Burkina Faso na kwingineko ambako serikali zilizokuwa zimelala kwenye usukani zilifurushwa baada ya askari polisi na jeshi kukataa kutii amri za kuzuia waandamanaji waliolenga kukomboa nchi zao.

           Polisi wetu wanafanya kazi katika mazingira magumu. Wana mishahara na marupurupu kidogo sawa na watanzania wengine ikilinganishwa na wanasiasa. Pia wanaisha maisha ya chini sana. Ukienda kwenye Kota zao, nyingi zinatia aibu. Wengine hata sare zao zinaonyesha ugumu na uhovyo wa maisha wanayoishi. Hapa hujaongelea udhalilishaji na chuki wanavyopambana navyo baada ya kutumiwa kisiasa kuwapiga na kuwaumiza watu wasio na hatia waliopaswa kuwalinda. Je kuvamiwa kwa vituo vya polisi ni jinai ya kawaida au chuki za wananchi dhidi yao? Tunapaswa kuzama zaidi.

          Japo lolote lawezekana, mazingira ya ukosefu wa maadili yaliyojengwa tangu kuondoka serikali ya awamu ya kwanza ni ya kulaumiwa kwa matukio haya. Watu wanataka bunduki ili wafanya ujambazi na kuwa matajiri wakijua fika mfumo wetu haumbani mtu kueleza alivyopata utajiri wake. Huu ni motisha mkubwa kwa wanasiasa na wahaloifu bila shaka.

          Wakati umefika wa kuwataka watawala wetu wahakikishe usalama wa watanzania wote wakiwamo polisi wanaoshughulikia usalama huu. Pia umefika wakati wa polisi kuuhoji mfumo na mamlaka zinazowajengea mazingira ya kufanya kazi na kuuawa katika mazingira magumu kirahisi hivi.  Wavunje ndoa na wanasiasa na mafisadi na kufunga ndoa na umma.Tunatuma salamu za rambirambi kwa jeshi la polisi tukishauri IGP ajiuzulu kwa vile ameshindwa.

 Chanzo; Tanzania Daima Januari 28, 2015.

Kijiwe chaomboleza ndata



 Pamoja na kwamba ndata huwa wanatughasi hata kutubambikizia kesi wanapotudaka, hatuna kinyongo nao zaidi ya kuwaonea huruma kwa wanavyotumiwa wakijiona hadi kuhatarisha maisha yao. Baada ya kutokea mashambulio mengi kubwa likiwa la hivi karibuni pale Ikwiriri, kijiwe kimekaa kama kamati kutoa rambirambi na tamko. Kinatoa shule kwa ndata wajitambue na kuchukua hatua kabla hawajamalizwa.
Mgosi Machungi siku hizi anajilawa kweli kweli. Leo kamuwahi hata muuza kahawa utadhani kuna upupu kitandani mwake. Nani anajua? Huenda bi mkubwa kamwekea mgomo. Hayo tuyaache.

Mgosi baada ya kuridhika kuwa  yakama au korum imetimia, anatafuna mic, “Tilishawambia kuwa wanatumika kishiasha lakini walitidhaau. Unaona sasa majambazi yanawaua kama swaa na kuchukua vya moto vyao kiahisi kana kwamba ni vichanga?”

“Mgosi nawe kwa kuanzia stori katikati huna mfano! Kumbe unaongelea mauaji ya ndata kule Ikwiriri siyo?” anauliza Mchunguliaji huku akijiweka vizuri kwenye benchi.

Mpemba aliyekuwa ndiyo amemaliza kuagiza kahawa anakwea mic “Yakhe hii yantisha sana hadi nataka nirejee zangu Pemba. Yawezekanaje hawa wanioitwa majambazi wavamia vituo na kupora silaha kirahisi hivi kama hakuna namna hata baada ya kuwa hii ishatokea kule Mwanza na kwingineko?”

Kapende hangoji Mpemba aendelee. Anakula mic kinomi, “Kwani ukienda Pemba unadhani utanusurika wakati kaya ni moja Ami? Hapa dawa si kufanya kama akina Kanji ambao wakisikia tatizo hukimbilia kaya jirani hadi mambo yapoe. Tunapaswa kusimama na kuwatetea hawa jamaa wanaoonekana kushindwa kujitetea hata wanapohujumiwa kwa kutumiwa vibaya na watafuta ulaji,” Kanji anamkata jicho la hasira kusikia akitaja magabacholi lakini hasemi kitu.

Mijjinga huku akiweka vizuri mavazi yake tokana na kupenda kuulamba na kuonekana kama Peedeejee, anapoka mic, “Hivi kama hawawezi kujilinda wataweza kutulinda kweli au ni kutumia kodi zetu kuwaneemesha wakati tukihangaishwa na wahalifu?”

“Kumbe wewe huwa wanakulinda! Kama kuna wanachonifanyia sikingine bali kutudunda tunapoandamana kupinga ujambazi uwe wa bunduki au kalamu. Kwa vile umewalenga, huenda wakaelewa somo,” Mipawa anajibu huku akitabasamu.

“Usemayo ni kweli. Wenye kulindwa ni wanono wanaoweza kuamuru ndata hata kuwakomesha wabaya wao binafsi. Mnaojidanganya kulindwa mmeliwa na mtaliwa sana,” Mbwamwitu anachomekea huku akimtazama Mgosi kwa chati akijua fika asivyopenda neno kuliwa.

Mzee Maneno anaamua kumpa sapoti Mbwamwitu japo huwa wanakosana mara kwa mara kutokana na maneno yake ya kufyatua. Anasema, “Kweli, wangekuwa wanatulinda si wangewakamata majizi na mafisadi yanayotuibia kila uchao. Si wangewakamata hata hawa wadokozi wa kura zetu wachakachuaji.”

“Yakhe usemayo nkweli. Wangekuwa wanatulinda si wengeenda kamata wale walokataa hata kuapisha viongozi kwa vile eti waloshinda upinzani.”

“Wankamate nani wakati wote chama moja dugu yangu. Usinikumbushe nshike nshike wa Segerea wa kuapishana kwa kutumia mawakili baada ya wachakachuaji kuzidiwa ujanja na people power,” Anachomekea  Kapende.

Mheshimiwa Bwege anaamua kutia guu,“Hapa halindwi mtu. Tunalindwa na Mungu vinginevyo, naona ndata kama wanyanyasaji wanaotumiwa na wanono, finish. Nadhani hawana haja ya kunung’unika wala kuonewa huruma hasa ikizingatiwa kuwa wao ndiyo wamewalea majambazi n ahata wengine kushirikiana nao wasijue hawa jama hawana dini.”

Baada ya Msomi Mkatatamaa kumaliza kusoma gazeti lake la kitasha anaamua kutia guu huku kila mtu akiwa na hamu ya kusikia atasemaje. Anakohoa kidogo na kubwia kahawa yake na kusema, “Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Hawa ndata waliwalea majambazi hata baadhi yao kufikia kushirikiana nao wasijue kuwa hawa hawana dini kama alivyosema msemaji mmoja aliyepita. Kimsingi, huu si wakati wa kuwalaumu ndata bali kuwasikitikia na kuwapa darasa wajue kuwa nao wanaliwa kama wale wanaodhani wananyanyasa kwa vipigo kila siku.”

Anabwia kahawa na kuendelea, “Kwa waliosoma mambo ya kiutawala tunajua fika nani wa kulaumiwa. Ulitegemea nini kwenye kaya ambapo kila mtu  anaruhusiwa kujiibia bila kushughulikiwa? Unategemea nini kwenye kaya ambapo kila mja anaruhusiwa kutajirika bila kutoa maelezo ya alivyopata huo ukwasi? Kama kuna kitachowamaliza ndata si kingine ni hiki. Pia kile kitendo cha kujiruhusu kutumika kuwa kikwazo cha ukombozi lazima kitawagharimu hata maisha yao kama ilivyotokea. Na huu si mwisho wa filamu yenyewe. Watanyotolewa roho wengi tu.”

“Kumbe tatizo ni kubwa kuiko tinavyoiona!” anashangaa Mgosi Machungi.

Msomi anaendelea kudema, “Hivi mlitegemea nini wanene kufunga ndoa na mafisadi na wezi? Kufanya hivi ni kuweka kaya kwenye autopilot. Kwa wale tuliopanda ndege autopilot ni mfumo wa kuendesha ndege bila rubani au rubani kuifanya ndege ijiendeshe yenyewe.”

Kabla ya kuendelea, Sofia Lion Kanungaembe anauliza, “Kweli ndege inaweza kupaa bila rubani jamani?”

Msomi anajibu, “Nilitegemea swali hilo. Usingeuliza ningeshangaa. Ukweli ni kwamba si ndege tu. Siku hizi kuna hata magari yanaweza kukatisha mitaa bila dereva. Hilo si muhimu leo. Muhimu ni kwamba tangu wanene walipojiingiza kwenye mashindano ya kuibia kaya, basi imebaki kama haina mwenyewe. Kwanini majambazi wa mitutu wasiichukue iwapo wanaona wenzao wa kalamu wameishafanya hivyo? Umemsikia mnene akilaani jinai hii au kueleza atakavyopambana nayo? Kimsingi, ndata wasipogutuka watatolewa kafara na wataliwa wakijiona kama wale wanaowanyanyasa.”

Kijiwe kikiwa kinanoga si mvua ikaaza kunyesha!
Chanzo: Tanzania Daima Januari 28, 2015.

Sunday, 25 January 2015

Kikwete sijui ni kupenda misiba, misifa, uzururaji, ugonjwa au ujinga?

unnamed1jk
Alipokufa baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere sikuona wala kusikia ujumbe toka Saudia. Rais Jakaya Kikwete sijui kwa kujikomba au kwa uhusiano wa siri eti ameunguza mafuta kwenda kuhani msiba. Kama alikuwa anamthamini sana mfalme Abdullah si angehudhuria mazishi ambayo nayo nijuavyo sijui kama angeruhusiwa kuhudhuria hasa ikizingatiwa kuwa wenzetu wanazika kirahisi na si kwa ushaufu kama waswahili maskini. Kikwete amebaki na miezi michache kuondoka madarakani bila kufanya kazi yoyote isipokuwa kuwatetea mafisadi na kuzurura. Heri amalize muda wake lau nchi ipumue kutokana na kuwa na rais asiyekaa ofisini wala mwenye kutumia busara katika maamuzi na matendo yake.

Despite our goodies we've our evils


Although we've a lot to be proud of, we, too, have a lot to be ashamed of. Nothing tarnishes Canada imago at home and abroad like this abhorring and horrible mistreatment of aboriginal people. Racism as you may call it, our brethren have suffered more words can express. Genocide committed on them for generations not to mention apartheid system lorded over them since the inception of colonialism. guests if not refugees in their own country! 
Time for addressing this anomaly making all of us uncomfortable seem to have approached. Let's seize it and redress our brethren as we move ahead as one country and one people.

We’re rich save we lack common sense

          The other day I was reading the story about the expansion of Jomo Kenyatta International Airport hyped as Green Field Terminal. However, soaked as I was, it baffled me to find that the total cost of the project is just $ 654 million. The terminal will enable JKIA that serves between two and six million passengers annually to approximately 20 million passengers. What a sound investment!
          After I was done with Green Field Terminal, I tried to revisit the map of corruption in the hunk. What came first was of EPA that sank 116 Richmonduli more than that and escrow 200. Wait. There is another coming known as Gas Pipe scam (GPS) I’m told it has already swallowed over $ 600 equivalent with the cost of expanding JKIA. What of our JNKIA? How many passengers it handles annually? According to president Uhuru Kenyatta after GFT is completed, it will propel Kenya into a middle income country. It’ll have 50 international and 10 local checkings, a railway and other facilities. The news of GFT sounds as haiku for Kenyans while a bitter pill for Bongolalalanders as they depend on cock-a-doodle-doo to get the answer in vain.
          To put it in our home context this means, we’re able to build more than two GTF shall we just use common sense. If you take $ 116M we lost to EPA without touching on Richmonduli then add $200M lost to escrow and $ 600M allegedly lost in Gas Pipeline minus over $ 500M we lost to corruption in local govts, you can see what I mean. We’re talking about roughly $1.5B. Had we “restrained” ourselves, as CCM would put it, from committing burglary to our hunk, we’re able to move over 1/3 of our paupers from stinking poverty. Again, where does this dosh go? To Swiss accounts or to the countries were many finks use as agents hail? Who knows? You know where our dosh goes. Feel the same shame you feel when you’re taken for a ride.
          Let me break a code of silence and say it. While our neighbours are boasting of being the hub of East and Central Africa, we’re busy in our bunga bunga biz of plundering! Interestingly, when it comes to corruption index, Kenya is worse than we are. Ironically, they’re ahead of the game albeit.  Everybody must ask. What’s always been wrong with our rulers? Are they real sane or something? I remember the story of two corrupt ministers one from Bongo and another from Singapore. When the Singaporean minister visited his counterpart in Bongo, he’s shocked to see the mansion the chinch was living in.  He jokingly asked him: How did you manage to build such an expensive castle? The dude replied, “Do you see that road project there? The cut I got from it enabled me to build this small house of mine. The Singaporean fella was fumbling and fluffing to see the road the swindler was talking about but ended up seeing nothing. He finally asked: Where's the road project you are talking about? The response was: What have you seen? The answer was: Nothing. The host quipped: That’s that.
          More than anything else, our helter-skelter polities, politics and policy are pregnant with corruption, nihilism and theft despite rulers’ braggadocios of umoja na ushikamano. How can we shikamana while others are robbing us pointlessly and wantonly?  To get into public office, one’s to bribe voters who shamelessly complain after goofing by selling their votes willy-nilly.
          Another gem, the world evidenced the drop of fuel price in the world market. Again, Tanzanians didn't enjoy this free fall. They’re still being robbed pointlessly as the govt sits and looks as if it has no biz with this rip off. Methinks. Consumers have to blame this logjam on the corrupt government that is in bed with swindlers raising monies for coming elections by allowing the thieves to rob our people. If anything, this must be one of the reasons why Tanzanians should vote CCM out. This needs no prefiguring or configuring. If Bongolalalanders would be true to themselves like boozers, we’d have had new faces in ulaji. It is as if Bongolalalanders are insane thanks to doing the same thing over and over again expecting different results. To avoid being chortled, Bongolalalanders need to pigeonhole CcM if it goes on with its wishy washy headship.
          If those suffering fail to do something to see to it that the kit and caboodle of swindlers is not made to pack and jump into water, I won’t wonder to hear people calling them names such as dimwits, halfwits and nitwits. Change can find its home through interrogating and rebelling against the status quo. Boozers have though singlehandedly doing this. Are the Bongolalalander ready?

          In sum, what Bongolalalanders need to ask themselves and their honchos is: Why are we endowed with all these resources and yet we’re shockingly poor? Is it lack of will to change the status quo for bongolalalanders or the lack of common sense for their honchos? Au revoir pour aujourd’hui.

Saturday, 24 January 2015

Hizi shahada za Tunu Pinda za kweli au?

Hii Master ya Tunu ni feki piga ua. Haiwezekani Chuo Huria mtu kufanya shahada ya Uzamili ndani ya miaka miwili.
Hi
Mke wa waziri mkuu Tunu Pinda akitoka kupokea shahada ya Uzamili toka Chuo Kikuu Huria Januari 2015.
Mke wa Waziri Mkuu Tunu Pinda akipokea shahada ya kwanza toka Chuo Kikuu Huria Oktoba  2012.

Kwa nchi ambapo kughushi kumehalalishwa, wakubwa, wake, watoto hata marafiki zao hutumia kila fursa ima kujipatia fedha kwa njia ya kuanzisha biashara mbali mbali kuanzia NGOs hadi kuchukua mikopo kwenye mabenki mbali mbali, kupewa upendeleo katika biashara na kukwepa kodi. Kwa upande wa ujiko wa elimu hujiandikisha kwenye vyuo huku ima wakiwalipa watu kuwafanyia mitihani au kupitishwa kinamna. Kutokana na mchezo huu mchafu ndiyo maana tunalzimika kuuliza kunani kati ya Tunu Pinda mke waziri mkuu na Chuo kikuu huria? Je amewezaje kufanya shahada ya Uzamili kwa miaka miwili  tena akiwa chuo huria ambako hakuna madarasa? Kwa wanaojua shahada ya pili, kwa watu wanaosoma full time hupewa kuanzia miaka miwili hadi minne kumaliza masomo wakati wanaosoma part time hupewa hadi miaka sita. Hapa lazima kutakuwa na namna.

Mlevi apanga kubadili jina

Japo sera ya uga huu ni kuepuka kadri iwezakanavyo kutaja majina ya ngurumbili. Hata hivyo, tokana na uzito na umuhimu wa suala la leo tutavunja huu mwiko wa kutaja majina hata kama siyo ya watu wanaoishi hata kufanana nayo. Hivyo, atakayeingia mkenge akadhani majina yatakayotumika hapa ni yake atakuwa na kibarua cha kuthibitishia mahakama kuwa kweli majina ni yake bila kukosea hata nukta. Hata hivyo sheria husema: To every general rule there is an exception to it.
          Kuna majina matatu au manne yaninyima usingizi.  Majina haya yanifanya nikonde. Nimejaribu kuvuta mibangi na kupiga ulabu ili kujisahaulisha majina haya bila mafanikio, majina haya yamegeuka majini kwangu. Kwani yanaanza kuninyonya damu akili na mawazo.
          Kwa vile nina usongo, tuseme hata uroho wa ulaji, kuanzia wa kisiasa hata kiwekezaji na hata kutorohsa nyara za taifa la shamba la bibi la Danganyika. Ili kutengeza njuluku ya kuweza kuwahonga wapika kura ya kula wapumbavu, sorry, wajanja, lazima niwe na njuluku sawa na mafisadi wanaotumia njuluku kutaka kuukwaa ukuu. Siku hizi bila kuwa na kufuru ya njuluku hupati ulaji hata kama ni wa nyumba kumi. Tangu utumishi wa umma ugeuke utumiaji umma, lazima mwenye kuutaka uwe na mshiko wa kuwashikisha wauza kura ya kula.
          Kama nataka kugombea uhishimiwa na kuupata kirahi lazima nibadili jina na kuwa Riz Kitegemezi badala ya mlevi. Hivyo, tukikutana mitaani siku zijazo sitaki nisikie jina langu la Mlevi Mkuu bali mwana wa mkuu Riz au ikipungua ikazidi basi niite Jan Makambale kama siyo God Mgimua au Imma Nchimbvi kama siyo Hussein Muinyi au Adam Milima ya Kigoma.
          Kwa vile nataka nipate dili za kuwa-srew walevi lazima nibadili jina na kuitwa Jimmy Rugemalayer. Najua nikiwa na jina hili nitavutia wakubwa wanaotafuta makuwadi wa kusimamia biashara yao fichi ya nyuma ya pazia kama ambayo wajina wangu amekuwa akifanya kwa takribani kwa miaka 20. Mungu akupe nini zaidi ya jina tamu linalovutia na kuwahamasisha wakubwa wakutumie au, tuseme, mtumiane kuwaibia walevi?
          Kwa vile huyu jamaa ameishachafuka sana na pia akiamua kushupaa hakuna pa kumbwaga, nina wasiwasi. Wakubwa wanaweza kuachana naye akabaki na akina Anna Kajuamlo, Jaji Mujuulizi na Ruhangaisa na nshomile wengine. Hivyo basi napanga kujiita Harbinger Seti Sing Song of screwing boozers. Ukiwa na jina kama hili unakuwa na uwezo wa kuwaweka wanene mfukoni mwako na kufanya utakavyo hata ukiamua kudhalilisha kaya kama wenye majina haya wanavyofanya kila uchao bila kuguswa. Ukiwa na jina hili , hata wafwadhili waking’akia dili zako wenye kaya wanajifanya kutojali wala kusikia kwa vile unayefanya mambo ni wewe mwenye jina tukufu duniani.
          Kwa vile kusafirisha wanyama nje kunalipa, napanga kubadili jina niitwe Kamran Ahmed ili nami nipate wakubwa wa kunitumia kusafirisha wanyama hai kwenda Qatar. Najua dili italipa hasa ikizingatiwa kuwa nikikamatwa watanitoa korokoroni na kunitafutia hati ya kusafiria na kutokomea ili nisiwataje.
          Ili kusafirisha pembe za ndovu bila kushughulikiwa, napanga kubadili jina na kujiita Abdul Kinamna au Ivory Kang Xi Pingpong Dong Kong ili nisafirishe vipusa na kuukata haraka kama siyo kupewa ulaji kwenye chama twawala kama Abdul Kinamna ambaye anaendelea kutesa huku kashfa yake ikisukumizwa chini ya busati. Hii Bongo usicheke wala kudhani hii ni mipango ya kibangi bangi au ulabu. I am dead serious guys. Nikishaitwa Ivory Kang Xi Pingpong Dong Kong nitaweza kupanga jumba la bei mbaya maeneo ya Msasani na kukusanya kago bila kubughudhiwa na ndata wala mashushu uchwara kama Rama Igondhuz wanaoaminika kutumika kuwapiga akina dk Steve Ulimboka na Absalim Kibanda.
          Ili kusafirisha miunga bila kusumbuliwa lazima nibadilishe jina niitwe Masogangege. Najua nikishaanza kuitwa mr Angie Masogange nikitia timu pale Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa mzee Mchonga washikaji zangu walioajiriwa pale kuruhusu miunga ipite hawatanisumbua zaidi ya kutaka niwakatie chao na kila mmoja achukue hamsini zake. Nitapita utadhani napitisha bidhaa halali au vitu vya maana. Kama twiga wanapita itakuwaje midawa isipite?
          Ni raha na ujiko kuwa na majina matakatifu kama vile Rugemalayer, Singasinga Harbinger, Dong Kong, Riz na mwengine mengi. Uwiiii! Nitaukata kama sina akili nzuri. Ngoja kwanza nisokote bangi inibangue nipange mipango mingine mikuu ya kuwa bilionea ghafla bin vu kwenye kaya hii ambako wizi umehalalishwa na utajiri wa haraka ni halali.
          Ikizidi ikapungua najiita  Malegelesi au Lukaza kama wale jamaa zangu wa EPA kama siyo Roasttamu la Aziz wa Kagoda ili nichonge dili jingine na HEPA niwahepe wachovu na kufaidi njuluku zao kama hawa jamaa wanavyoendelea kuzila huku wengine wakitangazwa kuwa mabilionea wakati ni wezi watupu. Kwani hatujui wala kuona?

          Ukihomola fedha za HEPA unaambiwa na mkuu urejeshe utadhani ulikopa wakati ulikwiba tu. Hii ndiyo Bongolalaland ambapo ubongo huwa hauna matumizi zaidi ya utumbo.
Chanzo: Nipashe Januari 24, 2015.

I bet Hakainde Hachilema will become Zambia's President

Although this time around the ruling Party in Zambia may use its incumbency to win  presidential by-election, if it happens, Mr H H or Hakainde Hachilema won't lose anything. If Edgar Lungu wins, it is the matter of being in power for one year. Come next year, HH will carry the day. So, either way the elections goes, HH is unstoppable. Looking at  his trajectory since he started running, HH is unstoppable. He might be stopped this time around, next elections he will win. If Lungu wins this time around, he will mess and re-run and lose. This is my bet based on the probability offered above. Who ever wins will do with a knife-edge win. So Zambians need to maintain peace given that there is no loser in this election shall HH lose so as to win next year.

Nenda Muongo na uongo wako



Nenda Sospeter Muongo profesa wa hovyo,
Nenda kaongee uongo wako na profesa Anna Tibaijuka
Nenda usiangalie nyuma 
Nenda kwa James Rugemalayer na Tibaijuka
Nenda mpange dili jingine
Au nenda kaongee na Kikwete mshirika wako
Nenda atakupa kazi huenda ubalozi Umoja wa Mataifa
Nenda Muongo Nenda
Tokomea mwana kutokomea
Ila wakati ukienda na kutokomea
Usikose kukumbuka
Siku moja wewe na wenzako mtanyea debe

Wednesday, 21 January 2015

Rais ajitoe kwenye makucha ya mafisadi

          Hali ilivyo, rais Jakaya Kikwete ametekwa na mafisadi kiasi cha kutofurukuta hata baada ya wananchi kulalamika na kupiga kelele. Inavyoonekana, Kikwete hasikii wala haoni. Ametekwa kiasi cha kuacha maswali mengi kuliko majibu. Wengi bado wanashindwa kuelewa ni kwanini Kikwete amejiruhusu kuonekana mhimili wa mafisadi dhidi ya umma. Wanashindwa wamuweke upande gani.
          Baada ya kuibuliwa kashfa ya wizi wa mabilioni ya fedha za umma toka kwenye mfuko wa escrow, mengi yamefichuka pia. Mafisadi watawala wakishirikiana na maajenti wao, waliliibia taifa kiasi kikubwa cha fedha ambacho hadi sasa hakijulikani. Mwanzoni tuliambiwa zilikuwa zimeibiwa bilioni 200. Baadaye tukaambiwa kumbe zilizoibiwa zilikuwa shilingi bilioni 300 na ushei. Taarifa za mwisho ni kwamba tuliibiwa shilingi bilioni 400. Je kutaibuka ukweli na namba nyingine?
          Pamoja na utata kuhusiana na kiasi cha fedha kilichoibwa, serikali imeendelea kukaa kimya ikionyesha kila dalili za kulalia upande wa pili. Rejea maazimio ya bunge kuwa Kikwete awawajibishe watuhumiwa walioonekana kutenda kosa asifanye hivyo. Ajabu mtuhumiwa mkuu, waziri wa Nishati na Madini profesa Sospeter Muhongo anaendelea kutesa huku umma ukiteseka. Kitendo cha Kikwete kumkingia kifua Muhongo kimeacha maswali mengi kuliko majibu. Je lao ni moja au ni woga tu? Je anatoa picha gani kwa umma uliomchagua akiuaminisha kuwa angeulinda pamoja na mali na fedha zake?  Kwanini Kikwete anasitasita kumchukulia hatua Muhongo wakati ukweli uko wazi, alitenda kosa?
          Kinachotatizo zaidi ni mantiki ya Kikwete kumfukuza waziri wa zamani wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi profesa Anna Tibaijuka kwa kosa si la kusaidia au kushiriki kuibiwa fedha husika bali kupokea pesa kiduchu. Je alimtoa kafara kuuridhisha umma na wafadhili kutaka mambo yapoe Muhongo na wenzake waendelee? Ionekanavyo kwa mizania ya Kikwete, kupokea fedha za wizi ni kosa kubwa kuliko kuiba fedha yenyewe. Isingekuwa hivyo, watuhumiwa kama Harbinder Sethi Singh na James Rugemalira wangekuwa korokoroni wakingoja kupewa haki yao. Ilavkwa Kikwete si hivyo. Kama ilivyo kwenye kitabu cha Shamba la Wanyama cha George Orwell, wanyama wote ni sawa  ila wengine ni sawa zaidi. Haiingii akilini. Watu waliopokea kuadhibiwa kabla ya waliowapa hiyo fedha ya wizi. Je Tibaijuka akisema ameonewa au kutolewa kafara ataonekana kituko kama alivyokuwa aking’ang’ania wakati dalili zote zilikuwa wazi kuwa alikuwa amekalia kuti kavu? Je kwanini Kikwete anatenda kinyume na fikra na akili za kawaida?
          Wapo wanaoona kama rais ametekwa na mafisadi. Pia wapo wanaoona kama rais aliagiza fedha husika zikwapuliwe kutokana na jinsi alivyoshughulikia wizi mzima. Ikumbukwe. Hii si mara ya kwanza kwa Kikwete kuwanusuru mafisadi kwenye kashfa nyingine ya mabilioni EPA ambayo hadi kesho haijawahi kukanushwa wala kutolewa na maelezo na Kikwete baada ya kutuhumiwa kuwa alikuwa nyuma ya jinai hii ili kupata mtaji wa kushindia urais. Rejea jinsi watuhumiwa wakuu wa ufisadi kama Rostam Aziz walivyookolewa na Kikwete kiasi cha sasa kuambiwa eti ndiyo mabilionea wanoongoza kwa utajiri nchini na si wizi wa fedha za umma.
          Hali ilivyo ni kwamba umma umekata tamaa kiasi cha kuwa watazamaji. Baada ya Kikwete kufanya kile waingereza huita leap service inaonekana hata wafadhili wamenyamaza kiasi cha kupoteza matumaini ya watanzania. Wengi wanashangaa mantiki ya Kikwete kuwataka wezi wa EPA kurejesha fedha lakini asifanye hivyo angalau dhidi ya wezi wa escrow. Je hii ndiyo lala salama ambapo wahusika, kama walivyokusanya mtaji wa kuingilia, wanakusanya mtaji wa kuondokea? Je hii ni stahiki na haki kwa watanzania? Je mtu aliyefanya hivi atashindwa kuhakikisha kuwa atakapoondoka madarakani anaacha kibaraka wake wa kumlinda kama alivyofanya Benjamin Mkapa baada ya kutuhumiwa kwa kashfa mbali mbali ikiwemo ya EPA ambapo mwanasheria aliyesimamia uhamishaji wa fedha za EPA aliwataja vigogo wa serikali na wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)?
          Kama upuuzi uliofanyika 2005, hakuna shaka. Rais ajaye atakuwa mateka wa mafisadi kama ilivyo kwa Kikwete ambaye ameonyesha wazi kuwa tayari kulaumiwa kwa kuwalinda mafisadi. Ameziba masikio na midomo. Amewadharau watanzania kuwapuuzia. Amedharau na kulipuuzia Bunge na hata wafadhili ili kunusuru watu wake. Je ni kwanini kama hakuna jinsi anavyonufaika na watu hawa? Imefikia mahali Muhongo na wezi wa escrow wanaonekana kama serikali ndani ya serikali. Kulikoni? Je kwa namna hii Kikwete, serikali yake na chama chake hawajetekwa na mafisadi kama si kuwa sehemu yao? Je kigugumizi cha Kikwete kinatokana na nahau kuwa waarabu wa Pemba hujuana kwa viremba? Je kwa muda mfupi uliobaki kwa Kikwete kuondoka ofisini, kama ataendelea na msimamo wa sasa wa kuwalinda mafisadi, watanzania wamejiandaa kufanya nini kuhakikisha haki yao haipotei? Je watawaachia kila kitu wanasiasa na wafadhili au kuchukua hatua mujarabu ili kutoa onyo kwa watawala wajao kutowatenza kama shamba la bibi? Je wataendelea kunywea na kugeuka kondoo wa kafara arariwaye bila kujitetea? Je ukimya, au tuseme kutojali au woge huu utalifikisha wapi taifa?
Tumalizie kwa kumtaka Kikwete ajiondoke kwenye makucha ya mafisadi. Alichaguliwa na watanzania na si mafisadi. Asikubali watanzania wamkumbuke kama rais aliyesimamia na kuwezesha ufisadi. Kuna maisha baada ya urais.
 Chanzo: Tanzania Daima Januari 21, 2015.

Kijiwe chajadili uzabazabina wa escrew


 
          Baada ya kuanza kushuhudia mazingaombwe juu ya kuwafikisha wa pilato majembuzi ya esrew, Kijiwe kimekaa kama kamati kujaribu kupitia nini kifanyike na nini kimepungua. Kijiwe kinatamka wazi kuwa waishiwa walikosea kukilinda kigenge chao na lisirikali lake. Maana kwa mchoro ulivyo, hata huyu dingi mwenyewe, kama ukweli utawekwa wazi hanusuriki.
          Kapende anaingia akiwa ameshika gazeti la Tell It Today. Anaonyesha kichwa cha habari kisemacho kuwa mafisadi wa escrow wamefikishwa kwa pilato.
           Anasema, “Mnaichukuliaje hii ya kuwapeleka wapokeaji tena vidagaa kwa pilato wakati mapapa yakiendelea kukata maji?”
          “Wallahi mie naona huu ka usanii ntupu. Yawezekanaje walopokea njuluku waonekane wakosefu kuliko walioiba na kuwakati huo nshiko yarabi? Hakuna waliponchosha kama kusema eti na Mizengwe iliyopinda hajatenda kosa wakati alitaka hata kuwasafisha hawa wenzake.” Mpemba anajibu kwa hasira na mstuko.
          Kabla ya Mpemba kuendelea Mijjinga anapoka mic na kuzoza, “Kuna jamaa yangu anayefanya kazi benki amenitonya kuwa alimuona Rugamalayer akiweka njuluku nyingine kwa ajili ya mkuu fulani ili atumie kwenye uchakachuaji.”
          “Si useme tu kuwa huyu mdingi ni wa Mizengwe aliyeonekana kufumbia macho ujambazi huu wa mchana kwa vile anafaidika nao kibinafsi na kichama,” anazoza mzee Maneno huku akibwia kahawa yake.
          Anaangalia huku na kule na kuendelea, “Jamaa yangu amesema kuwa watu wa karibu na habithi huyu walintonya kuwa huwa anawasiliana kwa email na Njaa Kaya kiasi cha kumuamuru la kufanya na la kuacha.” Mpemba anazidi kumwaga tama.
          Tunaangalia tukishuku kidogo, maana kijiweni wakati mwingine hata kamba hupita ilmradi kunogesha maongezi.
          Mipawa anakula mic, “Mie hili la kuwa na email ya Njaa Kaya au la halinishughulishi. Kinachonishangaza ni kuona wanashitakiwa vidagaa tu.”
          Sofia Lion Kanungaembe leo anaingia mapema. Anakula mic, “Hivi nyie watu mfanyiwe nini mridhike? Mbona mtukufu keshaamuru Takokuu wawafikishe hawa watuhumiwa kwa pilato? Ushahidi unao kwenye gazeti lako.” Anaongea huku akimtazama Kapende anayeamua kumuingilia Sofia na kusema, “Urongo mtupu.  Mbona hakumuokoa nshomile mwenzake porofweza Anne Tiba?”
          Kabla ya Kapende kuendelea, Profesa Msomi Mkatatamaa anakwanyua mic, “Umenikumbusha haya mambo ya ukabila uchwara. Umeona kuwa wengi wa waliosuka na kupokea njuluku hizi ni nshomile watupu? Yupo KyaBK, Bakwekwea, Tiba, Ki-Soft, Luang-isha, Mujuliiizi and others.” Anapiga chafya kuonyesha kuwa hii si halali na kuendelea, “Bado tunangoja kujua magabacholi waliokatiwa na Harbinder. Maana inavyoonekana wizi huu unawanufaisha watu wa chama kimoja, kabila moja na dugu moja kama sikosei.”
          Kanji anamkata jicho Kapende na kunong’ona kitu na Sofi na kusema, “Dugu yangu veve chukia hindi sana hadi nahusisha kila baya natendeka hapa. Kama Harbinger Napata juluku basi ni yake na mke na toto yake lakini si ya hindi yote. Yeye siyo kama haya nagawa juluku hovyo hovyo.”
          “Kanji usemayo kweli. Hindi hapana gawa pesa hovyo hovyo kwa Swahili bali yeye chukua pesa yake weka Bombei kusaidia dugu yake na siyo Swahili.” Anachangia Mchunguliaji.
          “Mie nadhani gabacholi aihitaji kutembeza njuluku hasa ikizingatiwa kuwa anaombwa na wakubwa asimamie jinai yao. Mara hii mmesahau skandali ya Chavda! Hawa jamaa wanaletwa na wakubwa wasiotaka kujulikana. Maana wanajua wakiwashikirika waswahili wanaweza kuwachoma au kuwataja mambo yakizidi wakati gabacholi anachukua pasi yake na kurejea zake kwao au kwa Mama na mambo kwisha.” Anasema Msomi huku akibonyeza kisimu chake.
          Mgosi Machungi na mheshimiwa Bwege leo wamechelewa. Ndiyo wametia timu kitambo na hivyo hawajaronga. Wana unywaunywa wa kuronga.
          Mgosi Machungi anakamata mic na kumwaga uchungu, “Kwei usemayo Msomi. Hizi dii hapa kayani inaonekana zinachongwa na dugu moja yaani nshomie. Usitikumbushe wezi wengine akina Kyomuhendoo, lukazakaza, Mwesigwa, Maegesi na wengine wengi toka kanda hiyo hiyo.”
          Mheshimiwa Bwege anampoka Mgosi mic na kuongeza orodha ya majembuzi wetu wa escrew.
          “Nakubaliana nawe Mgosi. Hii mijizi inaonekana kutoka sehemu moja. Inafaa ichomwe moto kama siyo kutundikwa shamba mchana kweupe ili liwe somo kwa wengine. Hata hivyo nani amhukumu nani wakati hawa tunaowalilia nao ni washirika na washikaji wa mibaka hii? Unadhani ni kwanini munene anajifanya kutomhusu hadi anatuwekea viporo vya ufisadi. Anajua akiwawasha nao wanamuwasha na ngoma inakuwa droo au vipi?”
          Mijjinga anakatua mic na kuongeza orodha, “Umesahau nshomiee mwingine Porofedheha Sossi Muongo, Maswiswi na wengine nawahifadhi.”
          Kapende anamkosoa Mijjinga kwa kusema, “Hao siyo nshomile bali mura kaka japo wote wanatoka kumoja tena ni watani.”
          “Kwangu wote ni wale wale. Kwani kuna tofauti gani kati ya mura na murangila? Yote toto ya baba na mama moja bwana.” Anajibu Mijjinga.
          Msomi haridhishwi na mchango wa Mijjinga. Hivyo anaamua kurejea kwa upya. Anakamua mic, “Japo majina na sura zinaonyesha ni watu wa kanda moja, hakuna haja ya kuwaweka kwenye kapu moja. Hata hivyo, nakubaliana nawe kuwa kuna patern ya ukabila hapa. Maana ukiona Were-ma na hata Nkwingwa Ngereja na Chengee wote wanatoka kanda hiyo hiyo. Sijui kuna tatizo gani hapa.”

Kijiwe kikiwa kinango si ukapita msafara wa mdingi. Acha tuurushie mawe na matusi kabla ya kutawanyika kuepuka kuwaumiza ndata ambao wangejipendekeza kuja kututia adabu!
Chanzo: Tanzania Daima Januari 21, 2015.