How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Saturday, 24 January 2015

Hizi shahada za Tunu Pinda za kweli au?

Hii Master ya Tunu ni feki piga ua. Haiwezekani Chuo Huria mtu kufanya shahada ya Uzamili ndani ya miaka miwili.
Hi
Mke wa waziri mkuu Tunu Pinda akitoka kupokea shahada ya Uzamili toka Chuo Kikuu Huria Januari 2015.
Mke wa Waziri Mkuu Tunu Pinda akipokea shahada ya kwanza toka Chuo Kikuu Huria Oktoba  2012.

Kwa nchi ambapo kughushi kumehalalishwa, wakubwa, wake, watoto hata marafiki zao hutumia kila fursa ima kujipatia fedha kwa njia ya kuanzisha biashara mbali mbali kuanzia NGOs hadi kuchukua mikopo kwenye mabenki mbali mbali, kupewa upendeleo katika biashara na kukwepa kodi. Kwa upande wa ujiko wa elimu hujiandikisha kwenye vyuo huku ima wakiwalipa watu kuwafanyia mitihani au kupitishwa kinamna. Kutokana na mchezo huu mchafu ndiyo maana tunalzimika kuuliza kunani kati ya Tunu Pinda mke waziri mkuu na Chuo kikuu huria? Je amewezaje kufanya shahada ya Uzamili kwa miaka miwili  tena akiwa chuo huria ambako hakuna madarasa? Kwa wanaojua shahada ya pili, kwa watu wanaosoma full time hupewa kuanzia miaka miwili hadi minne kumaliza masomo wakati wanaosoma part time hupewa hadi miaka sita. Hapa lazima kutakuwa na namna.

2 comments:

Anonymous said...

Msicheke bi Tunu
Mbona rais mwenye PHD duniani hakuna
Bongo hiyo
Ndo maana hata ughaibuni ukiwa na defree ya bongo
Wazungu hawaamani
Fuck unatuponza hata sisi wasomi wa kweli

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon usemayo kweli tupu. Hawa vihiyo wanatuponza sana. Rais wenu kuwa na PhD ya kugawiwa wala isikupe taabu. Kwani hata yeye mwenyewe anajijua alivyo mtupu na kihiyo. Hata hiyo bachelor ya siasa nayo ni mashaka matupu.