Japo sera ya uga huu ni kuepuka kadri
iwezakanavyo kutaja majina ya ngurumbili. Hata hivyo, tokana na uzito na
umuhimu wa suala la leo tutavunja huu mwiko wa kutaja majina hata kama siyo ya
watu wanaoishi hata kufanana nayo. Hivyo, atakayeingia mkenge akadhani majina
yatakayotumika hapa ni yake atakuwa na kibarua cha kuthibitishia mahakama kuwa
kweli majina ni yake bila kukosea hata nukta. Hata hivyo sheria husema: To
every general rule there is an exception to it.
Kuna majina matatu au manne yaninyima
usingizi. Majina haya yanifanya nikonde.
Nimejaribu kuvuta mibangi na kupiga ulabu ili kujisahaulisha majina haya bila
mafanikio, majina haya yamegeuka majini kwangu. Kwani yanaanza kuninyonya damu akili
na mawazo.
Kwa vile nina usongo, tuseme hata
uroho wa ulaji, kuanzia wa kisiasa hata kiwekezaji na hata kutorohsa nyara za
taifa la shamba la bibi la Danganyika. Ili kutengeza njuluku ya kuweza
kuwahonga wapika kura ya kula wapumbavu, sorry, wajanja, lazima niwe na njuluku
sawa na mafisadi wanaotumia njuluku kutaka kuukwaa ukuu. Siku hizi bila kuwa na
kufuru ya njuluku hupati ulaji hata kama ni wa nyumba kumi. Tangu utumishi wa
umma ugeuke utumiaji umma, lazima mwenye kuutaka uwe na mshiko wa kuwashikisha
wauza kura ya kula.
Kama nataka kugombea uhishimiwa na
kuupata kirahi lazima nibadili jina na kuwa Riz Kitegemezi badala ya mlevi.
Hivyo, tukikutana mitaani siku zijazo sitaki nisikie jina langu la Mlevi Mkuu
bali mwana wa mkuu Riz au ikipungua ikazidi basi niite Jan Makambale kama siyo
God Mgimua au Imma Nchimbvi kama siyo Hussein Muinyi au Adam Milima ya Kigoma.
Kwa vile nataka nipate dili za
kuwa-srew walevi lazima nibadili jina na kuitwa Jimmy Rugemalayer. Najua nikiwa
na jina hili nitavutia wakubwa wanaotafuta makuwadi wa kusimamia biashara yao
fichi ya nyuma ya pazia kama ambayo wajina wangu amekuwa akifanya kwa takribani
kwa miaka 20. Mungu akupe nini zaidi ya jina tamu linalovutia na kuwahamasisha
wakubwa wakutumie au, tuseme, mtumiane kuwaibia walevi?
Kwa vile huyu jamaa ameishachafuka
sana na pia akiamua kushupaa hakuna pa kumbwaga, nina wasiwasi. Wakubwa
wanaweza kuachana naye akabaki na akina Anna Kajuamlo, Jaji Mujuulizi na
Ruhangaisa na nshomile wengine. Hivyo basi napanga kujiita Harbinger Seti Sing
Song of screwing boozers. Ukiwa na jina kama hili unakuwa na uwezo wa kuwaweka
wanene mfukoni mwako na kufanya utakavyo hata ukiamua kudhalilisha kaya kama
wenye majina haya wanavyofanya kila uchao bila kuguswa. Ukiwa na jina hili ,
hata wafwadhili waking’akia dili zako wenye kaya wanajifanya kutojali wala
kusikia kwa vile unayefanya mambo ni wewe mwenye jina tukufu duniani.
Kwa vile kusafirisha wanyama nje
kunalipa, napanga kubadili jina niitwe Kamran Ahmed ili nami nipate wakubwa wa
kunitumia kusafirisha wanyama hai kwenda Qatar. Najua dili italipa hasa
ikizingatiwa kuwa nikikamatwa watanitoa korokoroni na kunitafutia hati ya
kusafiria na kutokomea ili nisiwataje.
Ili kusafirisha pembe za ndovu bila
kushughulikiwa, napanga kubadili jina na kujiita Abdul Kinamna au Ivory Kang Xi
Pingpong Dong Kong ili nisafirishe vipusa na kuukata haraka kama siyo kupewa
ulaji kwenye chama twawala kama Abdul Kinamna ambaye anaendelea kutesa huku
kashfa yake ikisukumizwa chini ya busati. Hii Bongo usicheke wala kudhani hii
ni mipango ya kibangi bangi au ulabu. I am dead serious guys. Nikishaitwa Ivory
Kang Xi Pingpong Dong Kong nitaweza kupanga jumba la bei mbaya maeneo ya
Msasani na kukusanya kago bila kubughudhiwa na ndata wala mashushu uchwara kama
Rama Igondhuz wanaoaminika kutumika kuwapiga akina dk Steve Ulimboka na Absalim
Kibanda.
Ili kusafirisha miunga bila
kusumbuliwa lazima nibadilishe jina niitwe Masogangege. Najua nikishaanza
kuitwa mr Angie Masogange nikitia timu pale Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
mzee Mchonga washikaji zangu walioajiriwa pale kuruhusu miunga ipite
hawatanisumbua zaidi ya kutaka niwakatie chao na kila mmoja achukue hamsini
zake. Nitapita utadhani napitisha bidhaa halali au vitu vya maana. Kama twiga
wanapita itakuwaje midawa isipite?
Ni raha na ujiko kuwa na majina
matakatifu kama vile Rugemalayer, Singasinga Harbinger, Dong Kong, Riz na
mwengine mengi. Uwiiii! Nitaukata kama sina akili nzuri. Ngoja kwanza nisokote
bangi inibangue nipange mipango mingine mikuu ya kuwa bilionea ghafla bin vu
kwenye kaya hii ambako wizi umehalalishwa na utajiri wa haraka ni halali.
Ikizidi ikapungua najiita Malegelesi au Lukaza kama wale jamaa zangu wa
EPA kama siyo Roasttamu la Aziz wa Kagoda ili nichonge dili jingine na HEPA
niwahepe wachovu na kufaidi njuluku zao kama hawa jamaa wanavyoendelea kuzila
huku wengine wakitangazwa kuwa mabilionea wakati ni wezi watupu. Kwani hatujui
wala kuona?
Ukihomola fedha za HEPA unaambiwa na
mkuu urejeshe utadhani ulikopa wakati ulikwiba tu. Hii ndiyo Bongolalaland
ambapo ubongo huwa hauna matumizi zaidi ya utumbo.
Chanzo: Nipashe Januari 24, 2015.
No comments:
Post a Comment