Heko Rais Magufuli

Wednesday, 18 October 2017

Kijiwe chatamani Tunduni angekuwa mgeshi

           Baada ya kungoja kwa muda mrefu kusikia kuwa washenzi waliotaka kumnyotoa roho mhishimiwa totoTunduni Lissu bila majibu, kijiwe kimeamua kutoa angalizo.
            Mgoshi Machungi anaingia akiwa anaonyesha wazi ana jambo linalomkera. Anaamkua, kuagiza kahawa yake na kusema “hivi inakuwaje hatisikii wae waiotaka kumnyotoa roho totoTunduni Issu wanageuka inshu kiasi cha kutonyakwa pamoja na unyama wao?  Hakuna kimetishangaza kama Munene na timu yake waivoitikia. Je tifanye nini au kunani jamani?”
            Kapende anakula mic “hata mimi nashangaa kuona namna alivyojihimu na kujilawa pale mgeshi mstaafu alivyopiga shaba. Huenda huyu Tunduni angelipata top priority kama ilivyotokea kwa mgeshi husika. Hata hivyo, sijaelewi namna mgeshi anavyoweza kuwa muhimu kuliko muishiwa.  Unadhani angekuwa ndata, wenzake wangelishindwa kuwanyaka wale waliomfanyia kitu mbaya. Na kama angekuwa munene, wote wangemwabudia na kumuogopa hata kama ni kinafiki na kwa woga.”
           Mijjinga  anaamua kutia timu “hata mie nashangaa sana. Maana tangu amiminiwe shaba Tunduni, sijasikia chama twawala kikifanya mandingo lau kutuma ujumbe rasmi kwenda Nairoberry kumujulia hali.  Hii inatisha na kusikitisha. Twapelekeshwa wapi ambapo sihasa inageuka uhasama.”           Kabla ya kuendelea Sofia Lion aka Kanungaembe anamchomekea “namna wanene walivyoshughulikia kashfa hii, licha ya kuwa aibu, inaonesha kuna namna. Hivi kweli Tunduni angekuwa mhishimiwa wa twawala wangekaa kimya hivi? Wameshindwa hata kutoa tamko hata kwenye vyombo vya umbea! Nani hataonja mauti huyu nimsujudie?”
            Mheshimiwa Bwege hataki kupitwa leo. Anakula mic “wafanye wafanyavyo ila kul nafsin zalikatu mauti yaani kila nafsi itaonja mauti. Kama wababe kama Farao aka Filauni na Nabukadnezza walionja mauti, nani atasalia zaidi ya kujilisha pepo tokana na ujuha na usahaulifu? Kama Nelson Mandela, Mzee Mchonga na wengine walipotea, nani huyu mjanja na shujaa atabakia? Shame on them all! Sijui wadanganyhika twapelekeshwa na kupelekwa wapi kiasi cha kuanza kuhukumiana na kujaliana au kutojaliana tokana na imani zao za kisiasa? Inatisha na kuhuzunisha; sina mfano.”
            Mpemba anarejea “hata mie sielewi wallahi.  Yaani mhishimiwa mzima anamiminiwa shaba na washenzi waliofanya hivi hawashikwi! Yethu! Laillah illa Allah! Ni sheitwan gani ametuingilia hivi kiasi cha kukosa mwelekeo huruma na utu!  Hii yashangaza, kutisha na kutia shaka wallahi.”
            Mipawa anaamua kutia guu “namuona Tunduni kama mdogo wangu, ndugu yangu, mbongo mwenzangu na binadamu mwenzangu anayepaswa kuhurumiwa sawa nami au yeyote yakimkuta kuhusisha hata hawa wauaji na washenzi waliotaka kumnyotoa roho bila sababu zaidi ya woga na upumbavu wao. Najitahidi kuvaa viatu vya Tunduni nimdeku mkewe na watoto na ndugu na mashabiki wake ukiachia mbali wenzake. Simdeku Tunduni sawa na nguruwe waliomuumiza.” Anakohoa na kuendelea “namuona kama mwanaume, baba, mwana, raia, binadamu na asiye na hatia kama mimi na wewe na wao. Namuona Tunduni kama ninavyojiona na kukuona wewe.  Laiti wengi–hasa wale waliotaka afe–wangevaa viatu vyangu na vyake na kuondoa upumbavu wao, naamini unyama aliofanyiwa usingetokea.”
           Kabla ya kuendelea Msomi Mkatatamaa anakula mic “Usemayo mazito na kweli. Hivi Tunduni angekuwa ndata, kweli nguruwe na wanaharamu waliomshambulia wangekuwa bado uraiani wakifaidi malipo ya jinai yao? Hata hivyo, sitakata tamaa. Kwani, malipo ni hapa hapa duniani. Laiti binadamu angejaliwa kujua yanayomgoja–sina shaka–wahalifu waliomfanyia kitu mbaya Tunduni wangelia na kusaga meno na kuchelea kutenda unyama waliotenda tokana na upumbavu na upofu na upogo wao. Hawa waliommimia shaba Tunduni au waliowatuma wangekuwa wanaume kama si watoto si riziki, wasingetenda unyama waliotenda. Hata nguruwe–pamoja na uchafu na udogo wa ubongo wake–asingeweza kutenda upumbavu na unyama huu.”
           Kanji hataki apitwe. Anachumpa “mimi tamani Tunduni ive jesi. Kama nakuva nene navezajali yeye sana. Kama nakuva hiyo vote hata nene naabudia yeye. Mimi sangaa sana hapana nene yoyote nakwenda Nairobi ona yeye kwanini? Sasa kama natibiva Bmbei navesa sema mbali au nakwenda fanya shopping.”
            Mheshimiwa Bwege anaamua kurejea “hawa kweli wanashangaza kama alivyosema Kanji. Wako wapi akina nduli Amin, Gaddafi, Hitler na Mussolini? Wako wapi akina Osami bin Ladin na Mura Umar? Wako wapi akina Augustine Pinochet?  Wako wapi akina baby na papa Duvallier? Wako wapi akina Samuel Kanyon Doe? Nambie. Wako wapi akina Botha the Croc? Wako wapi akina Pol Pot wa Kampuchea na mahabithi wengine wengi waliofanya unyama usiomithalika? Binadamu ni nini zaidi ya kuwa manii na matope?”
             Anapiga chafya na kuendelea “leo naongea kifalsafa kama mzee Mchonga tunayeadhimisha miaka 18 ya kifo chake kama si Mandela au Nkrumah na Lumumba. Wamanga husema: pen is mightier than a sword japo sisi tumebadili ukweli huu na kuuweka kinyume kiasi cha wageshi kuwa muhimu kuliko wahishimiwa.”
           Msomi anamchomekea “tunapaswa kujenga kaya ya usawa bila kujali tunayemjali ni mgeshi au mhishimiwa, msukuma mkokoteni au rubani au mtumwa na bwana na mtawaliwa na mfalme. Wote tulizaliwa uchi; na siku moja tutatoweka na kugeuka matope na kusahaulika. Tutendeeni haki mkijua kuwa ujivuni na ukatili havilipi; na malipo ni hapa hapa duniani.”
            Kijier kikiwa kinanoga si nikamuona jamaa anayenidai! Guess what. Nilikitoa.
Chanzo: Tanzania Daima J'tano leo.

No comments: