How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Monday, 28 October 2013
Siku ya kufa CCM itakuwa hivi
Siku ya kifo cha Chama Cha Mapinduzi kama kilivyotabiriwa na mwenyekiti wake rais Jakaya Kikwete itakuwa hivi. Magazeti, runinga hata nyavuti zitapokea tangazo namna hii.
Ndugu Jakaya Kikwete wa Ikulu Dar es salaam anasikitika kutangaza kifo cha bosi wake Chama Cha Mapinduzi kilichotekea kule Dodoma mnamo tarehe 24 Oktoba 2913 kutokana na kipigo cha watanzania baada ya CCM kupatikana akifanya ujambazi, ufisadi na kuuza madawa ya kulevya.
Mazishi yatafanyika kwenye sanduku la kura mwaka 2015 baada ya kufika ndugu wa marehemu.
Habari ziwafikie TLP na NCCR-Maangamizi wakiwa pale Moshi, CUF akiwa Pemba, UDP akiwa Bariadi Simiyu, UPDP akiwa Uzaramoni.
Pia habari ziwafikie Rostam Aziz akiwa Igunga, Edward Lowassa akiwa Monduli, Nazir Karamagi akiwa Bukoba na Andrew Chenge akiwa Bariadi.
Pia habari ziwafikie jamaa ndugu na marafiki ndani na nje ya nchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment