How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Monday, 9 March 2015

Kipanya leo umeua


Kibonzo hiki kimenikuna na usomi wa majambazi wanaoibia taifa. Ni bahati mbaya kuwa Tanzania inaongozwa na profesa hata kama ni wa kuzawadiwa lakini ni ya hovyo kuliko hata viinchi vidogo vilivyotoka vitani karibuni. Walemavu wa ngozi hawana usalama. Fedha za umma zinaibiwa na wasomi uchwara kama huyu. Kusoma si kukariri vitabu viwe vya sheria au uchumi bali kuonyesha njia. Karume hakuwa amesoma lakini alifanya makubwa kuliko akina Dk Salmin Amour. Hawa si wasomi kitu bali makanjanja waliopita darasani kwa bahati mbaya. Sijui kama porofwesa Tibaijuka au profedha Muhongu aka Muongo ni wasomi zaidi ya makanjanja wenye shahada za udaktari. Huwa siwatofautishi na walioghushi kama vile Makongoro Mahanga, Mary Nagu, Didace Masaburi, Emanuel Nchimbi, Wiliam Lukuvi na wahalifu wengine wengi waliojazana serikalini wakiiba kana kwamba hawatakufa.

1 comment:

Anonymous said...

Imekaa vizuri Bravo Kipanya!