The Chant of Savant

Saturday 19 August 2017

Kunyonyesha hadharani si aibu wala kosa; ni haki ya mtoto na mama


Katika nchi za kimagharibi kunyonyesha mtoto hadharani ni kosa tena aibu inayopaswa kukemea. Hata hivyo, hali ni tofauti katika tamaduni za Kiafrika. Mama wa Kiafrika hujisikia fahari kumnyonyesha mtoto wake mahali popote bila kujali nani anaona, anaudhika, anapenda au kuchukia. Hivi karibuni kwenye jimbo la Arizona nchini Marekani, akina mama wanaonyonyesha waliamua kukataa aibu na utumwa wa kupangiwa ni wapi wanyonyeshe; na wapi wasinyonyeshe. Waliamua kupiga picha hiyo juu kama ishara ya kupinga ukatili huu kwa mama na mtoto.
           Japo kila mtu ana haki ya kuthamini, kulinda, kutangaza na kutetea mila zake, mengine yamezidi na yanakera. Inakuwaje tunawavumilia washenzi wanaotembea uchi au kufanya vitendo vya hovyo hadharani kama kubusiana lakini hapo hapo tunashindwa kuvumilia watoto na akina mama kupata haki zao? Tafakarini.

No comments: