The Chant of Savant

Wednesday 23 August 2017

Dege let kung'an'ganiwa Ukanadani

          Image result for tundu lissu photos
                   TAARIFA kuwa bomba letu limeng’ang’aniwa kule Kanata zimekichefua kijiwe kiasi cha kuamua kutoa ushauri wa bure kwa sirikali kaya yetu isiendelee kuwa shamba la bibi au kichwa cha mwendawazimu mlevi kujifunzia kunyoa kama ilivyokuwa tangu aondoke mzee Mchonga. Msomi Mkatatamaa anaingia akiwa na jarida la kimataifa la Inquirer. Anaamkua na kulitua jarida kwenye meza. Bahati mbaya hakupata mashabiki wengi kutokana na kuandikwa kwa kimombo. Anakohoa kidogo na kuchonga: “Mnazo habari kuwa bomba letu aina ya Bombardier lililokuwa litue kayani mwezi jana limeng’ang’aniwa na matapeli wa kimatifa tuliowaendekeza huku tukiua wajasiriamali wetu?” Kabla ya kuendelea Mchunguliaji anakula mic: “Unamaanisha lile bomba la Magu siyo? Hapa lazima Magu atumbue waliosababisha kadhia hii kwa kuruhusu matapeli kupata upenyo wa kutula kijinga hivi.” Mpemba anadakia “yakhe jana niliponsikia Tunduni Lissu akikinukisha wallahi nilidhani siasa; kumbe ukweli! Je, nani walisababisha nchezo huu hadi bomba letu likang’ang’aniwa kirahisi hivi au kuna nkono wa ntu?”Mgoshi Machungi anakamua mic: “Mgoshi unauiza chooni kwanuka nini wakati ukijua kaya yetu? Hapa timeishaingizwa mkenge. Kama aivosema Mchunguliaji, tingoje tione kama Magufui atatumbua watu hapa. “Si bue kuna mkono wa mtu hapa. Kwanza, iikuwakuwaje tikaingia mikataba ya kijinga kiasi cha kuuhusu tiiibiwe hivi kama hatina akiii?” Mijjinga anakula mic: “Mie sikushangaa; na sitashangaa wakijitokeza wengine kutufanyia ushenzi kama huu. Waliodhani Tunduni hana data walikosea. Jamaa linajua linachosema. Hukumsikia binti wa Waziri Mkuu wa zamani akifoka akidai watu wasishabikie hasara hii bali walisaidie lisirikali kumaliza tatizo.” Mipawa anakwatua mic: “Tunduni anajua kila kitu. 
Bombardier, Kijiwe chashauri sirikali
Nani alijua kuwa kumbe kaya yetu ilikuwa imeshtakiwa tangu mwaka 2009? Je, kwanini serikali ilikaa kimya hadi mambo yakawa mabaya hivi? Nadhani siku nyingine wakitaka kununua pipa kama hili wasinunue kama sirikali. Badala yake waje kwangu na mzee Mpayukaji watupe njuluku twenda tukawanunulie kama watu binafsi au vipi?” Kapende anakamua mic: “Nadhani huu si wakati wa kulaumiana wala kushabikia bali kuishauri sirikali iache kufanya mambo kitoto. Nashauri ianzishe shirika lake la ukandarasi ili kuziba mianya ya matapeli wa kigabacholi na kimataifa kuendelea kutugeuza nyanya. Kama haitaki hili basi iwape tafu makandarasi wazawa ili wafanye hizi kazi zinazotumika kama uchochoro wa kutupia au vipi?”Msomi anarejea: “Japo wazo lako linaweza kuonekana kama utani, lina mashiko sana. Laiti walaji wetu wasingekuwa wanaendekeza masilahi binafsi, nadhani hili lilipaswa kufanyiwa kazi haraka katika miradi yoyote tutakayoingia kama kaya. Tuwatumie watu wetu hasa wazawa waweze kutuepusha na jinai hii ya kujitakia kutokana na ufisadi na uroho vya kipumbavu.” Kanji anakula mic: “Sasa kama nasema zawa peke yake sisi hapana zaliwa hapa lakini iko 
raia tafanya nini? Fisadi vote ni fisadi; haina zawa au geni. Kwani ile vote nakula juluku ya IptL iko geni tu au gacholi? Iko unga kono wazo ya Kapende lakini nakataa hii ya zawa.” Da Sofia Lion aka Kanungaembe anaamua kutia guu: “Kanji umesema ukweli; ufisadi hauna mgeni wala mzawa ingawa wengi wanaoweza kutuliza kirahisi ni wageni kwa vile hatuna namna ya kuwakamata kama tunavyoweza kuwafanyia wazawa. Hivyo, kuna haja ya kufanya mambo kwa kuzingatia uhalisia na si mazoea.” Kabla ya Sofia kuendelea Mheshimiwa Bwege anaamua kumchomekea: “Da Sofi acha nikuchomekee. Wazo lako ni la maana sana kuwa tusifanye mambo kwa mazoea bali kuzingatia hali halisi. Nadhani unachotaka kumaanisha hapa ni kumtaka bwana Magu abadilishe mfumo wetu wa uendeshaji sirikali badala ya kudhani yeye peke yake anaweza kuleta mabadiliko kwenye mfumo mchovu na mbovu wa kiwizi ule ule japo naye ni sehemu yake. Kama walivyosema waliotangulia, hapa kuna mikono ya mafisadi tena wakubwa na wasioguswa hasa wale anaowakingia kifua asijue watamkwamisha hata kumteketeza. Haiwezekani kesi ifunguliwe 
mwaka 2009 ikae tu bila kushughulikiwa. Je, huu utitiri wa wanasheria tulio nao kwenye lisirikali unalipwa kwa kazi gani kama mauzauza yenyewe ni haya?” Mzee Maneno anaamua kumwaga cheche: “Kaka unasema eti unadhani kuna mikono ya watu. Kuna miguu na mikono na makalio ya wanene hapa bila shaka. Hii ndiyo hasara ya watu kutumia makalio na makinikia ya akili kufikiri badala ya vichwa. Kama Magu atataka kufanikiwa, awavue kinga wapendwa wake na kuwasulubu lau tujue nani alikula nini na nani  alipewa nini na lini? Naunga mkono wazo la kuwawezesha makandarasi wazawa ili watakapovurunda tuwasweke lupango kama kina Rugetumbuliwa na Singatumbua wanaoendelea kuimba kwaya na kina Hasi Kitilia na wengine waliodhani hawawezi kutumbuliwa. Pia asisahau kuachana na ubashiteshite wa kuendekeza mafisadi wa kila aina kama alivyofanya kwenye kadhia ya kughushi.” Kijiwe kikiwa kinanoga si akatokea Tunduni. Acha tumbebe na kumshangilia kabla ya kumpa ofa za kahawa kama heshima ya kunena ukweli ambao wengi wanaogopa kuunena.
Chanzo: Tanzania Daima J'tano leo.

No comments: