The Chant of Savant

Tuesday 13 August 2013

Mtawala gani wa ki-Afrika anaweza kurejea darasani?

German Chancellor Angela Merkel in front of her class in Berlin, Tuesday.
Chancellor wa Ujerumani, Angela Merkel ametoa mpya kwa kurejea darasani kufundisha historia ya taifa lake. Wakati wa maadhimisho ya 52 ya kujengwa kwa ukuta wa Berlin ambao kuangushwa kwake kulimaliza vita baridi kati ya kambi za Magharibi na Mashariki, Merkel aliwaacha hoi wajerumani alipoamua kurejea darasani kufundisha historia. Merkel ambaye ana shahada ya uzamivu katika Fizikia aliyeandika karatasi nyingi za kisomi, aliamua kufundisha somo la historia. Je ni viongozi wangapi wa kiswahili wanaweza kurejea darasani kufundisha? Hebu piga picha marais kama Jakaya Kikwete, Jacob Zuma,  Joseph Kabila, Paul Kagame,Yahya Jammeh, Uhuru Kenyatta na  wengine wenye elimu za kuokoteza. Hakika bado Afrika ina ukame wa viongozi! Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.

14 comments:

Jaribu said...

Warejee darasani kufundisha au kufundishwa?

Anonymous said...

Jaribu, kweli umepokonya maneno kotoka kinywani mwangu!!
Jamaa si kuwa tu hawataki / wezi kurejea darasani, bali pia wanatamanii jamii nzima isielimike ili waendelee kuiba mchana kweupeee. Nchi ambayo waziri mwenye dhamana ya "elimu" anasema ni muungano kati ya Tanganyika na visiwa vya Zimbabwe ulioundwa mwaka gani sijui...! Tutegemee nini tena??

Mkuu Mhango, maskani hii nimeipenda sana.

NB: Nimesoma kidogo intro ya "Nyuma ya Pazia". Kinapatikana Amazon pia?

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

ANON,
Nyuma ya Pazia inapatikana kwenye amazon hivyo unaweza kugoogle na kujisomea. Umenikumbusha naibu waziri Murongo sijui muongo sijui nani kihiyo kama akina Nchimbi.

Anonymous said...

Hivi fr. Mhango, Jaribu na Anon wa kwanza, nisaidieni hili... Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amepata chuo gani shahada ya uzamivu? Na katika fani ipi? Tukishapata majibu hapo basi tutahitimisha vizuri na kwa usahihi juu ya kadhia hii!

Jaribu said...

Chuo cha Kujipendekeza, Kitivo cha Nigaie Ulaji. Nafikiri ni Fani ya Kucheka cheka.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Nijuavyo PhD yake ni ya kupewa na Chuo Kikuu cha Kenyatta nchini Kenya aliyempa shahada hiyo ni Dr.Harris Mule mkuu wa chuo hicho Rais Jakaya Kikwete wakati wa mahafali ya 25 ya chuo hicho mjini Nairobi. Phd hiyo inatokana na jitihada zake za utatuzi wa migogoro kwa nchi za Afrika hasa mgogoro wa Kenya. Huenda kesho atapewa shahada nyingine ya kukamata wauza unga kama siyo kula na kunywa na mateja

Anonymous said...

Inasemekana pia Vasco anajiandaa kupewa na ka-Pii Echi Dii kengine ka urubani (au hata usaidizi). Jamaa ana masaa mengi angani mpaka sasa kushinda marubani wengi wa wengi ATC (kama bado ipo). Pia kuna wengine wanafikiria kumtunukia ya kuweka mawe ya msingi na kuzindua vitu hata vya hovyo hovyo tu. Inasemekana "nyenzo" muhimu ya kazi ya jamaa Si kalamu kwa kusaini lolote lile, ni mkasi kwa ajili ya kukata tepe.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon umeua! Umeniacha hoi unaposema zana yake kuu ni mkasi kukata utepe. Umesahau kuwa ni bingwa wa 'mikasi' pia yaani mpenda urodaz na totoz.

Anonymous said...

Na hiyo ya 'urodaz' itakuwa phD somedays. Basi tumeshapata majibu!

ntayega said...

Mkuu viongozi wetu wanao uwezo wa kuingia darasini na kufundisha.kwa habati mbaya wanakabiliwa na majukumu mengi kiasi amabacho kupata muda wa kujitolea kufundisha haupo.Na katika maraisi uliowataja mkuu, nadhani Rais Uhuru Kenyatta anaweza kujitolea kufundisha siku moja.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Shehe Ntayega nakiri jina lake limeingia kwa bahati mbaya ila nadhani ni kutokana na tabia yake ya kupenda kanywaji, Waliobaki ni vihiyo, Umemsika Kikwete alivyopambana na maunga kwa kula na kunywa na mateja? Mhuni kama huyu anaweza kufundisha nini shehe wangu?
Wakati mwingine tatizo si kufundisha bali ubunifu kama alioonyesha Merkel.

Jaribu said...

Anonymous wa 15 August 2013 07:46 naona wewe mkali wa vipande! Mimi nilifikiri sifa ya kuwa mwenyekiti wa CCM ni uwezo wa kushika kalamu lakini wewe unasema hata kusaini nako kunahitaji jitihada kubwa ya ubongo, labda mkasi wa kukatia utepe tu? Hebu kwanza nitafakari picha hiyo

Anonymous said...

Halafu mkuu Mhango ndiyo akamalizia kabisa kuwa "Nyapala" wetu yule ni mtu wa mikasi kwa kwenda mbele. Mwenyekiti wa CCM aliwahi kuwa mmoja tu, Hayati JK Nyerere. wengine wote ni waganga njaa tu. Iko siku utasikia Nape au Mwigulu wako kwenye kigoda kile. Kutumia mkasi ni rahisii kweli, kwa kuwa ni kukata tu hakuna kingine. Kutia sahihi ni lazima usome na uelewe kwanza unachosaini. Hukumbuki huko nyuma ameshasaini uhuni fulani aliletewa na wabunge kumbe hata haujajadiliwa bungeni? Jamaa ni full Ze Komedi!

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Wengine humuita kichwa cha panzi wengine Dr Zilch na mengine mengi. Huoni anavyotanua na wala unga akiwatumia aonekane anawajali wakati analala kitanda kimoja na wauza unga?