The Chant of Savant

Monday 5 August 2013

Swaumu inaanza kupoteza maana

sf5 da738
Hivi karibuni umetokea mtindo wa ajabu sana ambapo watu wasio waislamu huandaa futari. Imefikia mahali hata makampuni fisadi kama ya simu ambayo yanawapa watanzania huduma mbovu eti nayo yanafuturisha. Huwezi kuamini kuona Radio Clouds inayosifika kwa kuvunja maadili eti nayo inafuturisha. Je hapa tatizo ni njaa au kutojua maana ya dhana nzima ya kufunga na kufuturu? Hebe angalia hapa chini 'alhaj' Benjamin Mkapa akitoka kufuturu na marais Jakaya Kikwete na Ali Hassan Mwinyi. Je hii ni aina mpya ya uislamu au aina mpya ya ujinga? Sitashangaa kusikia askofu naye akifuturisha au kufuturu.

5 comments:

Jaribu said...

Shida ni kwamba kila mtu amegundua kuwa dini ni dili; la kupatia kura, kipato au umaarufu. Hata na mimi nataka nianzishe duka la kukodisha kanzu na bhargashia kwa maka... I mean wasioamini.

Ntayega said...

Kanzu na Bharagashia ni vazi tu na sio kitu kingine. kwa mfano vazi rasmi la wanaume wa kabila ya waganda ni kanzu kofia na koti na waislam ni sehemu kidogo tu kabila hilo. Hivyo basi Muislam kumualika jirani, rafiki, na hata wafanyakazi wenza, ni ishara ya mapenzi , ushirikiano,na undugu uliopo baina yetu bila kujali tofauti ya imani zetu na sivinginevyo.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Bwana Ntayega habari za siku nyingi? Vipi Toronto mwatunyima nini? Nakubaliana nawe kuwa kanzu si big deal na kualikana si kosa. Kinachogomba ni udhu wa wale wanaoalika na kualikwa kaka. Hawa wasio waislamu wanakuja kufuturu vipi wakati hawakufunga? Kama hivyo basi chakula hiki kiitwe mlo wa jioni lakini si futari. Kwani afuturuye shurti awe amefunga shehe. Nashukuru kwa kunitembelea na kuacha unyayo wako ya Maulana shehe wangu.

Mtwangio said...

Mhango,inapochukuliwa dini na kuchanganywa na siasa,mila na desturi matokeo yake ndiyo haya tunayoyaona hivi sasa.Dini hivi sasa imekuwa ni utamaduni,mila na desturi na kama hivyo ndivyo uibuka wanasiasa kama kawaida ya wanasiasa daima wanapotaka kufikia malengo yao huwapanda waumini wachanga vichwani,mabegani na migongoni kwa kupitia dini na hatimaye huvaa ngozi ya kondoo na wakati ni chui!Na si wao tu wanasiasa bali hata wafanya biashara wakubwa wakubwa huitumia dini kwa kujitafutia hadhi na nafasi zao za kibiashara na hata kujitangaza kwamba wao ndio wana funguo za kuingia peponi kwa kutoa sadaka zao uchwara ambazo haziwasaidi kwa karibu au kwa mbali waumini hao wachanga kuwatoa katika umasikini wao.Kwa hiyo kufutarisha kwa sasa ni utamaduni,mila na desturi na kutafuta masilahi ya kisiasa au kibiashara au hata umaarufu wa kijamii, kwa hiyo watambue waumini wachanga mtu yoyote yule alikua ni mwanasiasa au mfanya biashara anayeitumia dini kwa manufaa yake binafsi au kutaka umaarufu wa kutaka kufikia malengo yao hao wanakuwa nichui waliojivisha ngozi ya kondoo.Ebu tuangalia kwa sasa jinsi gani wahubiri wa imani ya kikristo je ni kweli wanamuhudimia Yesu kama ni wachungaji au wanatafuta utajiri kwa kila njia kwa kupitia ujinga wa waumini wachanga?Mboni hatuwaoni wachunganji hao wakipigania kuwaondoa wafuasi wao na waumini weziwao katika dimbwi la umasikini zaidi ya wao kumiliki kila aina ya luxury katika maisha?je tumepoteza dira ya kuona tofauti kati ya wachunganji hawa majambazi na majambazi wa missionary ambao walikuwa wanatuibia huku wakitujengea shule ,hospitali na kutuchimbia visima?na hata kutupeleka ng'ambo kwa masomo ya juu zaidi.?

Ntanyega umeeleza kwamba kanzu na bharagashia ni vazi tu na sio kitu kingine,je unadhani kwa waisilamu hoja yako hiyo itanawakinaisha?Vazi la kanzu ni vazi ambalo linaambatana na itikadi au sema utamaduni wa kiisilamu kwetu Afrika Mashariki.Na hao wanamume wa Kiganda uliowataja ambao wamelichukua vazi hilo kama ulivyosema si hoja ya kimsingi wao wameathirika na vazi hilo na kulichagua kama ni vazi kwa wanamume wao lakini ni vazi la kigeni kutoka bara Arabu na wavaaji wa vazi hilo ni waarabu wa Omani ambao huvaa bila ya koti na waarabu wa Yemeni wakiambatanisha na koti.Na hadi hii leo wengi wa wahubiri wa kidini ya kiisilamu kuvaa kanzu,kofia au kilemba ni lazima kulingana na itikadi hiyo ya vazi hilo na uisilamu.

Ntanyage,umedai kwamba muisilamu kumualika jirani,rafiki,na hata wafanya kazi wenza,ni ishara ya mapenzi,ushirikiano na udugu na udugu uliopo baina yetu bila ya kujali tofauti ya imani zetu na si vinginevyo.Naam naweza kukubaliana nawe kwa hoja ya mjadala kwamba huo ni ukweli wa maadili ya dini tena dini ya aina yoyote ile iwe ya mbinguni au ardhini lakini ukweli wa ardhini kwa wakati wetu huu ambapo wakareketwa wa dini wa pande zote ambao wanahubiri chuki na kumkataa mwenye imani nyingine hakuna au akuashirii kile ambacho ulichokidai cha ishara ya mapenzi,ushirikiano na udugu.Nenda wewe leo Zanzibar kisha ujulikane kwamba ni mfuasi wa dini ya kikristo kisha uone hayo mapenzi na udugu kama utayapata!!!



Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Mtwangio umeniacha hoi unaposema kuwa dini sasa inatumiwa na michui kuwararua waumini wachanga. Ulipogusa wahubiri wa kikristu au wachungaji nimecheka. Mie mara nyingi huwaita hawa WACHUNAJI ama PEOPLE OF DOG but not PEOPLE OF GOD. Maelezo yako yanakidhi kila kitu kiasi cha kuninyima upenyo wa kuuliza swali au kupinga jambo. Mfano wako wa Zanzibar nadhani utamfungua macho Ustaadh Ntayega. Nadhani tangu aishi Amerika kwa muda mrefu amesahau baadhi ya maendeleo huko nyumbani ambako chuki za kidini zinazidi kuwa big deal hasa kwa wafuasi wa dini maskini na wenye welewa mdogo wakitumiwa na baadhi ya matajiri uchwara kujifurahisha kwa mgongo wa dini.l