How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Friday, 16 August 2013
Je Mwakyembe anaweza kuwataja wauza unga?
Japo ni jambo jema kuwapa moyo wenzetu wenye uthubutu kama uthubutu wenyewe una ithibati, kitendo cha waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe kusema atawataja vigogo wa mihadarati ni changamoto kubwa.Je Mwakyembe atatimiza ahadi yake au kupiga siasa tu ili kujipatia ujiko?
Kwa wanaokumbuka jinsi Mwakyembe alivyomaliza kashfa ya Richmond kwa kusema kuwa kuna mambo waliyaficha kwa sababu wajuazo, wana shaka kama atawaja waunza unga vigogo. Sitashangaa kumsikia akiwataja vijidagaa huku akiwagwaya mapapa. Sitashangaa kutokana na kutoaminika kwa wanasiasa wetu wasanii. Mwakyembe kwa kitendo cha kuwaficha wakubwa wa Richmond ambao ni zaidi ya Lowassa na akapewa zawadi au tuseme kulipwa fadhila, si mtu wa kuaminika tena. Je Mwakyembe aligundua makosa yake na anataka kuyafuta? Je ataendelea na sanaa kama kawaida yao? Je anafanya hivi ili apewe cheo kingine ambacho hapa ni kugombea urais kupitia CCM? Je amejituma au ametumwa na bosi wake? Kwanini Mwakyembe aibuke baada ya bosi wake, Jakaya Kikwete kukutana na mateja ikulu? Je hatua ya Mwakyembe kuwataja waliomshinda Kikwete ni kupingana au kuna jambo? Je amejiandaa kuyaepa yaliyompata Prof. George Saitoti kule Kenya alipopania kuweka wazi majina ya vigogo wa mihadarati? Je asipowataja vigogo wenyewe tufanye nini? Maswali ni mengi kuliko majibu. Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment