The Chant of Savant

Friday 1 January 2021

JE NI NANI ATABEBA MIKOBA YA MAGUFULI?

Nina tabia ya kuotea visivyowezekana hasa wakati ambao wengi hawategemei. Mwaka 2012 nilimwambia mwanafunzi wangu aishie Ontario kuwa rais wa Tanzania ambaye angechukua mikoba ya Jakaya Kikwete aka Vasco da Gama–––kama wapinzani wake walivyozoea kumuita tokana na tabia yake ya kupenda kufanya ziara–––ni John Pombe Magufuli. Kijana huyu––kwa vile mimi ni mwalimu wake–––hakugusia suala hili hadi Magufuli alipochaguliwa rais miaka mitatu baaday. Nadhani ima alidhani nilikuwa naota au aliogopa kulumbana na mwalimu wake. Kama ilivyokuwa wakati ule, leo ngoja niote tena kuwa mmoja kati ya watatu hapo juu anaweza kubeba mikoba ya Magufuli. Nitatoa sababu. Mwinyi, anaweza kufuata mkondo wa historia ya baba yake ambaye alikuwa rais wa Zanzibar kwa mwaka mmoja na baadaye akachukua mikoba ya jabali jingine kama Magufuli yaani baba wa taifa Mwl Nyerere. Samia anaweza kubebwa na jinsia na namna alivyohudumu chini ya Magufuli bila ya makuu sawa na Majaliwa ambaye–––licha ya upole–––ni mwanafunzi mzuri wa Magufuli. Kitendo cha kumrudisha kina mengi ya kusema kuhusiana na Magufuli anavyomkubali–––hasa ikizingatiwa ukali na uchapakazi wa Magufuli ambaye hana mchezo wala urafiki kwenye kazi. Kwa leo tuishie hapa.

No comments: