Mmoja wa raia wanne wa Nigeria akipelekwa kupigwa risasi nchini Indonesia baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha unga leo (jumatano) saa za kule. Laiti na Tanzania na nchi nyingine za kiafrika zinazoendekeza na kuabudia wauza unga zingechukua hatua hii, huenda vijana wetu wengi wangepona hasa ikizingatiwa kuwa wauzaji wengi wa unga ni wageni waliokuja kutumia ujinga na ubovu wa mfumo wetu wa kifisadi kutengeneza fedha huku wakitutengenezea mauti ya haraka. Natamani wale wanaowalinda wauza unga kama Jakaya Kikwete waone picha hii. Najua watu wao watapita na kuwaeleza mambo ya kukera kama haya. Huu ni ushahid kuwa rais wa sasa wa Indonesia Joko Widodo si muuza unga wala kiongozi anayenufaika kutokana na jinai hii.
How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Tuesday, 28 April 2015
Hawa ndiyo wanaojua kupambana na wauza unga
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment