The Chant of Savant

Wednesday 3 March 2021

KUSIMAMISHWA KUCHANGIA KWENYE NIPASHE JUMAPILI


Wapendwa wasomaji wetu,
Tokana na mgogoro wa kisheria baina yetu na Kampuni ya IPP juu ya kutolipwa malipo ya miaka mitatu, leo nimepokea taarifa kuwa makala zangu za kila jumapili hazitachapishwa tena kwenye gazeti la Nipashe Jumapili hadi mgogoro wa madai haya utakapotatuliwa. Hivyo, tunasikitika kuwataarifu kuwa makala husika, kwa muda, hazitakuwapo kwenye blogu hii. Hata hivyo, tutakuwa tukichapisha makala za jumatano zinazotoka kwenye gazeti la Raia Mwema. Habari ndiyo hiyo.

No comments: