How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Friday, 12 July 2013
Ukiwa na mindset kama hii jua hakuna nchi bali kusanyiko la panya au majuha
Kama kila mtu atafikiria kula mbona tutakulana kama inavyoendelea ambapo mfagiaji hudokoa kwenye eneo lake na rais humogola kila mahali. Je hawa wasio na meno wala uwezo wa kupanga kula kama vile watoto, wazee, wagonjwa na wenye matatizo mbali mbali watakuwa wageni wa nani katika nchi hii ya kulana, kuliwa, kutafunwa na kutafunana? Hata hivyo faraja ni kwamba hata hawa wanaojisifu kuwala wenzao nao wanaliwa na wengine watokao mataifa ya ughaibuni kama tulivyoshuhudia hivi karibuni walaji wetu wakiliwa na Obama.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
2 comments:
Suluhisho ni kuchagua viongozi wenye maadili, au angalau uwezo wa kupambanua tofauti kati ya ngano na makapi yake, siyo kuwapa makatibu kata madaraka ya kutawala nchi.
Suluhisho ni kuwa na mfumo hasa katiba inayotamka wazi kuwa ufisadi ni kosa kubwa linalopaswa kumuondoa mtu madarakani. Tuwe na mfumo unaopambana na ufisadi kuanzia juu kwenda chini badala ya Bottom up kama sasa ambapo wadogo wanalazimishwa wataje mali zao wakati rais hajawahi kufanya hivyo.
Post a Comment