How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Tuesday, 13 August 2013
Angalia watu wenye akili wanavyopambana na janga la moto
Hivi karibuni uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta nchini Kenya ulishika moto na kutekea pakubwa. Hata hivyo, kulikuwa na lawama kuhusiana na uchelewaji wa zima moto kufika na kuuzima moto ule. Sambamba na tukio hili, nchini Kanada kwenye jimbo la Newfoundland and Labrador ulitokea moto mdogo ukilinganishwa na wa JKIA. Link hii inaonyesha jinsi moto huu ulivyoshughullikiwa kwa sekunde. Natamani na nchi zetu za kiswahili zingekuwa na uwezo kama huu badala ya kujikita kwenye ufisadi na ujambazi wa mchana. FUATILIA LINK HI http://www.youtube.com/watch?feature=player_detailpage&v=LQWTTOm6loM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
7 comments:
Meanwhile, Waziri wa Mawasiliano wa Kenya, Engineer Nobody Competent alisema kuwa wanasubiria kibali cha rais Uhuru kutumia VIP lounge kuwashugulikia majeruhi. Kumbe wakina Mizengo Pinda wako wengi. Huyu Bwana Mhandisi inabidi tumpe tuzo ya EINO; Engineer in Name Only.
Umeisikia ya ndata wa Kenya kuchangamikia kuiba bia badala ya kuokoa watu na mali. Ama kweli Africa yote has gone to dogs almost everywhere. Kwani huo uwanja ni wa mama yake rais au wanazuzuliwa na jina la jambazi Jomo Kenyatta aliyeisaliti na kuiuza Kenya kwa waingereza?
Kumbe hata polisi wa Kenya nao hovyo? Basi sifa yao iliyobakia ni ile ya kuwaswaga njemba wanaojisaidia vichakani, "Malisa twende!" Ingekuwa poa kama poliCCM angalau na wao wangekuwa wanasimamia usafi wa mitaa. Kuna sehemu Dar ukipita unaweza kuzimia kwa harufu ya tindikali ya urea!
Kenyatta kuiuza nchi kwa Waingereza ndio kulimwezesha mwanae Uhuru aweze kusoma Amherst College, wakina kamchape hawawezi kulipa ada za chuo hicho.
Nimeishi Nairobi kwa miaka mitatu. Sijawahi kuona askari wa hovyo kama wa Kenya. Wanaua kuliko hata jeshi la wahuni la Polisi la Tanzania. Hukuwasikia waliochangamkia kuiba bia uwanja wa JKIA ulipoungua?
Nimeishi Nairobi kwa miaka mitatu. Sijawahi kuona askari wa hovyo kama wa Kenya. Wanaua kuliko hata jeshi la wahuni la Polisi la Tanzania. Hukuwasikia waliochangamkia kuiba bia uwanja wa JKIA ulipoungua?
Kwa hiyo badala ya kusaidia kuokoa wao wanaiba bia? Kweli ndio Afrika hiyo.
Jaribu umesahau kuwa baadhi ya watu wana akili za kinyama? Hujasikia jinsi ajali inapotokea Bongo watu wanavyokuja kutoa huduma ya kwanza ambayo si huduma chochote bali kuwasachi waathirika?
Nakumbuka kisa cha mama wa kichaga aliyepata ajali akawa anawaruka maiti akisema, "Babangu umelalia ndisi zangu," Hiyo ndiyo Afrika iliyomalizwa na mfumo wa kifisadi na kijambazi.
Post a Comment