How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Tuesday, 8 December 2015

Kijiwe chaunda BEEP na kukosoa uamuzi wa Dk Kanywaji

 
Kwanza tukiri wazi. Kijiwe kinamkubali rahis Dk Kanywaji Makufuli kwa moyo owte na tunaweza kusema kijiwe kinamkubali kichizi kama siyo kinoma. Hata hivyo –baada ya kutangaza msamaha kwa wakwepa kodi –kijiwe kimepania kumkosoa na kumpa ushauri wa bure. Tokana na sakata la kusamehe kodi wanakijiwe wanahema kwa hasira kama Egwugwu kwenye riwaya ya Chinua Achebe, ya Hamkani si Shwari Tena.
Mijjinga anaingia akiwa anatikisa kichwa kama mtu aliyeudhiwa na jambo. Anaamkua na kusema, “Waheshimiwa wasio waishiwa kama wale wa mjengoni mmesikia jinsi Dokta Kanywaji anavyoanza kujipiga mtama?”
Mpemba anakwanyua mic na kujibu, “Yakhe wallahi mie sijakuelewa hasa nkizingatia kuwa jamaa ametia ntu adabu tangu achukue usukani wallahi.”
Mijjinga anakatua mic, “Sina ugomvi na hili Ami. Ugomvi wangu ni ile hali ya kutoa siku saba kwa wakwepa kodi kana kwamba yeye ni mahakama au hakimu. Anapata wapi uhalali wa kufanya hivyo jambo ambalo linaonyesha kuwa ameanza kujipiga mtama?”
Msomi Mkatataama anakula mic, “Dk Mijjinga nakubaliana nawe. Dk Kanywaji hakupaswa kutoa siku saba. Badala yake alipaswa aagize vyombo husika kuchukua hatua za kisheria bila kuangalia nyani usoni. Sijui ni kwa vile jamaa amesoma makemiko na si sheria au sijui ni huruma au kutaka kupata njuluku haraka atimize ahadi zake.”
Kapende anachomekea, “Hata mimi kwa hili sijampata vizuri. Nadhani kinachopaswa kuangaliwa hapa ni kama amefuata sheria na utawala wa sheria badala ya kusikiliza mawazo yake. Maana kwa nijuavyo kaya yetu, kama akifanya mambo bila kufuata sheria mahakama zaweza kumuumbua hasa ikizingatiwa kuwa wengi wa majaji waliteuliwa kiushikaji na wengi wao ni mafisadi kama alivyowahi kusema Tunduni Lisu akapuuziwa na Njaa Kaya akiwalinda watu wake.”
Msomi anajerea, “Kumbuka jamaa ni binadamu tena anayepambana na gendaeka waliodeekezwa na Njaa Kaya na Ben Tunituni Makapi muda mrefu. Nadhani tumsaidie. Kwa vile yeye na waziri wake mkubwa Katelephone Majaliwa wanaonekana kusikiliza ushauri wetu, basi napendekeza tuunde chombo cha kumkabili na kumpa shule ya bure. Napendekeza tuunde Bongo Exclusive Emminent Persons (BEEP) yaani Warume wenye maarufu wa kumsaidia kijana wetu asichemshe hata kabla ya mwaka kwenye ulaji au vipi? Tukishaunda BEEP tusibeep bali kumtwangia kwa kutia guu ikulu na kupinga uamuzi wake. Mko tayari?”
Wanakijiwe wanaitikia, “Tuko tayari.”
Mgosi Machungi anakatua mic, “Hata mimi naunga mkono hii kitu bipu. Lazima tusimbipu bipu ili asije kuewa madaaka akahaibu hatua nzui aiyokwishafikia ya kuwatia jambajamba wezi wa mai zetu. Azima timsadie na kumpa shue ya bue kwa kupinga baadhi ya maamuzi yake.”
Mheshimiwa Bwege hangoji. Anakamua mic, “Hata mimi hatua yake ya kutoa msamaha wa kodi imenikera sana na lazima hili alijue wazi. Suing mkono muungu mtu wala mtu asiyefuata sheria. Anasamehe kama nani? Wiki moja aliyotoa kwangu ni msamaha na kwenye biashara kinachouzwa na kununuliwa ni muda. Mbona hili simpo?”
Sofia Lion aka Kanungaembe anabwia kahawa haraka haraka na kudandia mic, “Mijitu ya kaya hii sijui iliumbwaje?”
Kabla ya kuendelea, Mbwamwitu anamchomekea, “Iliumbwa kama wewe au kamuulize Mungu da Sofi. Hapa najua umeguswa pabaya lazima ustuke.”
Sofia anampuuzia Mbwamwitu na kuendelea, “Mwenzenu katumia mamlaka aliyopewa na katiba na yote hii anafanya kwa ajili ya kuwasaidia nyinyi msio na shukrani. Acha baba wa watu afanye vitu vyake.”
Mipawa aliyekuwa kimya akisoma gazeti anaamua kutia guu, “Najua mheshimiwa lais anaweza kuwa na nia nzuri. Lakini two wrongs never make a right au vipi? Hakuna anayepinga hatua za Dk Kanywaji vinginevyo awe fisadi wa kawaida. Huoni alivyoumbua mijizi iliyokuwa ikijfanya waheshimiwa wakati ni mijizi tu.”
Msomi anakamua mic tena, “Mawazo na mapendekezo yenu ni mazuri. Nadhani tufanye mpango wa ima kumkaribisha Dk Kanywaji –kama Katelephone –aje hapa kijiweni tumpe ushauri au atupe mwaliko kama alivyowafanyia wafanya bihasara ambao wengi wao ni wezi na wakwepa kodi. Twende kule tumpe shule ajue bado Danganyika ina Bongo zinazochemka na siyio Bongolalaland tena au vipi?”
Anapiga chafya na kuendelea, “Nijuavyo mimi kisheria ni kwamba mtu kama amefanya kosa, anaweza kusamehewa au kuadhibiwa na mahakama. Hivyo, kitendo cha Dk Kanywaji –hata kama kimefanywa kwa nia njema –kina kasoro. Unawasamehe wakwepa kodi kwa kuwapa wiki nzima ili iweje?”
Kanji anakamua mic, “Jamani kwanini vatu napenda kosoa kila kitu. Hebu toa muda kwa Dokta Kanyaji iko leta mambo mingi zuri sana kwetu sote. Ile miji nakwepa kodi sasa tumbo joto. Mimi unga kono Beep. Kama nakwenda kulu na kutoa vazo yetu iko sikiliza na chukua hatua kali sana. Twende kuu na ongea siyo beep. Beep nini bwana. Sisi natwanga.”
Mipawa anarejea tena, “Tokana na uchapakazi wa Katelephone, tumshauri Bandari na viwanja vya ndege viwekwe chini ya ofisi ya waziri mkuu au Dk Silaha huku fedha akipewa prof Pumba.”

Kijiwe kikiwa kinanoga si likapita shangingi la yule jambazi wa muuza vipuli vya magari wa Kariakoo aliyetaka kukwepa ushuru wa bilioni 80. Acha tulifukuze na kuvunja vioo huku mhusika akiokolewa na ndata tusimfanyie kitu mbaya!
Chanzo: Tanzania Daima Desemba 6, 2015.

No comments: