How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Monday, 30 April 2012

Mrithi wa WTC huyu hapa

Image Detail

Kipi kitatumika kuunda baraza la mawaziri?


Kibonzo hiki licha ya kuchekesha kinaonyesha mawazo ya watanzania walio wengi hasa wakubwa. Hivi kama wakubwa tena wasomi wako hivi,  hao akina Mimi ni Maimuna hali ikoje? Je Baraza la mawaziri linalongojewa kwa udi na uvumba litaundwa kutegemea ushirikina, ushirika, udugu, kujikomba, sifa, kulindana, usanii au business as usual? Time will surely tell.
Muhimu usishangae kuwakuta ambao hukutegemea na kutegemea kuwakuta ambao uliwategemea. Hii ni CCM ambayo mara nyingi mambo yake ni yale yale. Akitoka kibaka  huyu atakuja jambazi yule. Kwa ufupi ni kwamba hakuna msafi anaweza kutokea CCM kwa sasa na kwa mfumo huu wa ufalme tunaoendelea nao. Laiti Bunge lingekuwa na mamlaka ya kumpa rais  majina ya watanzania na si wanachama wa kuteua kuwa mawaziri baada ya kuyapitisha kwa kura na kupata ushauri toka kwa wananchi! Hata  hivyo vumilieni. Danganyika ni nchi ya mazingaombwe na abracadabra nyingi. Mtafungwa kamba na mtakubali bila shaka.

Haya ndiyo matokeo ya ndoa ya CCM na CUF?


Wengi wanashangaa CCM walikuwa wapi leo huko Tanga Kikwete alipopokelewa na wana CUF.Kikwete yuko Tanga kwa ajili ya maadhimisho ya Mei Mosi. Je atatangazia baraza lake la walaji huko au ndiyo hivyo ziara za bwana mkubwa kama kawa?

Kumbe na Karume ni fisadi au?


Image Detail
 Rais mstaafu wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar Amani Abeid Karume pichani.
Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, amekumbwa na kashfa akidaiwa kutoa amri ya kukodishwa kwa majengo ya Mambo Msiige bila kufuata utaratibu na sheria.

Tume iliyoundwa na Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuchunguza pamoja na mambo mengine, ukodishaji wa ardhi na majengo ya Serikali, imebaini Mambo Msiige ilikodishwa kwa miaka 99 thamani ya dola za Marekani milioni 1.5 kinyume cha sheria

Kwa mujibu wa Ripoti ya Uchunguzi wa kamati hiyo iliyoongozwa na Mwakilishi wa Chakechake, Omar Ali Shehe, majengo hayo yalikodishwa kwa Kampuni ya ASB Holdings Limited kupitia taratibu ambazo hazikuzingatia maslahi ya Taifa.

Ripoti ya kamati hiyo inaonyesha kuwa ukodishwaji huo ulifanyika baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Ikulu) Dk Mwinyihaji Makame Mwadini, kupewa agizo na Rais Karume (mstaafu) kwa maandishi.

“Dk Mwinyihaji aliiambia kamati kuwa yeye ndiye aliyepokea agizo kwa wino mwekundu kutoka kwa Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume kuwa Serikali imepata mwekezaji kampuni ya ASB Holdings Ltd, “sehemu ya ripoti hiyo ilikariri maelezo ya Waziri Mwadini alipohojiwa na kamati hiyo.

Kwa mujibu ripoti hiyo, Dk Mwadini aliiambia kamati kuwa Rais aliagiza kampuni hiyo ikodishwe kwa mkataba wa malipo ya Dola milioni 1.5 na kulipa kiasi cha Dola 10,000 kwa mwaka.

Kwa agizo hilo, Dk Mwadini alimwandikia barua Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na uchumi Zanzibar akimwarifu kupokea fedha kutoka kwa mwekezaji huyo ili aweze kujenga hoteli ya nyota tano na kwamba baada ya kupokea malipo hayo afungue akaunti maalum ya kutunza fedha hizo.

Hata hivyo, kwa mujibu wa ripoti hiyo, Dk Mwadini alipotakiwa kutoa mbele ya kamati ushahidi wa agizo la rais alikataa na kusema kutoa dokezo la rais ambalo limeandikwa kwa wino mwekundu siyo sawa.

“Mpaka wakati huu tunawasilisha ripoti hii agizo la maandishi kutoka kwa rais halikutolewa na Dk Mwadini mbele ya kamati ya uchunguzi.” Kwa mujibu wa ripoti hiyo yenye kurasa 224.

Hata hivyo, ripoti hiyo imesema kwamba pamoja Kamati hiyo kumtaka Katibu wa Baraza kumwandikia Barua ya Desemba 8, mwaka 2011 ya kumtaka kuwasilisha ushahidi wa agizo la Rais mstaafu ameshindwa na kuendelea kutetea msimamo wake kuwa ni “Siri ya serikali.”

Kamati hiyo ya uchunguzi imebaini kuwa nyaraka za mpango wa ukodishwaji majengo na ufukwe wa Shangani zimepotea Wizara ya Ardhi, makazi, Maji, na nishati katika mazingira ya kutatanisha.

“ Katika mafaili ya Ofisi hakuna hata barua ya maombi ya ukodishwaji yaliyofanywa na mwekezaji mwenyewe, kwa ufupi hata faili lenye kumbukumbu za “Lease’ ya majengo ya Mambo Msiige na Starehe Club halipo.” Imeeleza Ripoti hiyo.
Chanzo: Nipashe Jumapili.

Marais wa kwanza wanawake wa Afrika


Kushoto ni rais Sirleaf (Liberia) akiwa na mgeni wake rais Banda (Malawi) pichani kulia.
Rais mpya wa Malawi Bi. Joyce Banda amerejea nchini mwake akitokea Afrika Kusini na Liberia. Anasema alikwenda Afrika Kusini kushukuru kwa kutunza mwili wa mtangulizi wake huku akienda Liberia kujifunza. Je ni changomoto gani inawakabili akina mama hawa kama marais? Rais wa Liberia Ellen Johson Sirleaf anasifika kwa harakati zake za kuleta amani nchini mwake. Banda anasifika kwa kuwainua akina mama hadi akaitwa mama Mandasi au mandazi kwa kiswahili. Kuna imani kuwa wanawake si wabadhirifu kama wanaume. Je tutegemee kuliona hili hivi karibuni katika nchi mbili? Tuwape shime wadhihirishe hili ili angalau wawe kichocheo cha kupata marais wengine wanawake barani Afrika.

Ndoa ya CHADEMA na Sabodo si mtihani tosha kwa upinzani?



Hakuna ubishi kuwa ndoa ya anayeitwa mfanyabiashara maarufu kwa jina la Mustafa Sabodo pichani imeshika kasi. Kwa wanaojua jamaa zetu hawa walivyoletwa na kuchuma, anahofia usafi wa huyu jamaa anayesifika kutumia jina la marehem Mwalimu Julius Nyerere kujinufaisha. Anajiita mpenzi wa Mwalimu ambaye wakati wa uhai wake hata hivyo hatukuwahi kumsikia. Je hii ni janja ya wahindi kuanza kutafuta pa kushika baada ya kuona CCM ikiyoyoma? Je kama wameitosa CCM iliyowalea na kuwakumbatia hadi wengine kuzawadiwa ubunge, CHADEMA ni nani wasiifanyie  hivyo? Je nao falsafa yao ni ya 'Sina adui au rafiki wa kudumu bali maslahi'? Mwanzoni Sabodo aliahidi kuwapa CHADEMA jengo lake la Mwenge. Ghafla amepiga U-turn na kusema eti atawajengea ofisi. Tusije tukaruka mkojo tukaishia kukalia manonihino. Kusema ndoa ya Sabodo na CHADEMA inabindi iangaliwe isijekuwa mtego wa CCM kumtuma kada wake kuwachafua. Kama Sabodo anaipenda CHADEMA anangoja nini CCM? Kimsingi anataka kuweka vyama vyote mfukoni mwake.
Sabodo alikaririwa akisema, “Kwa kweli nimefurahi sana kunialika kwenye mkutano wenu, nimeshawahi kuisaidia CCM, lakini hawajawahi kunishukuru kama mlivyofanya ninyi.”
Je hii ni sababu yenye mashiko kumfanya aipende CHADEMA hivyo au anaandaa pa kushika baada ya CCM kujiishia?

Sunday, 29 April 2012

Ni wakati muafaka kumm-empeach hata kum-recall Kikwete


  • Image DetailKutokana na madudu ambayo yametendwa na serikli ya rais Jakaya Kikwete kwa miaka sita ambayo amekuwa madarakani, kuna haja ya kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye hata kumrecall. Bahati mbaya CCM ni chama cha Mafisadi. Bila hivyo, walipaswa kum-recall Kikwete kama ilivyotokea Afrika Kusini kwa Thabo Mbeki ambaye licha ya uchapakazi wake aliondolewa tena kwa chuki binafsi za uroho wa madaraka. Pia huwezi kumlinganisha Kikwete na Mbeki ambaye alisifika kwa weledi na uwajibikaji.  Kikwete amethibitisha kuwa mzigo kwa taifa. Ni rais dhaifu asiyeweza kufanya lolote hadi asukumwe. Rejea alivyoshindwa kuwatimua mawaziri wake waliotuhumiwa kughushi vyeti vya kitaaluma. Rejea alivyoshindwa kumtimua waziri mkuu na mshirika wake mkuu Edward Lowassa hadi bunge lilipofanya hivyo. Je hii inatokana na ukweli kuwa Kikwete anashiriki karibu katika kila upotevu wa pesa tajwa au woga? Je rais wa namna hii anapaswa kuvumiliwa huku lawama wakitupiwa wasaidizi wake wakati tatizo kuu ni yeye? Je Kikwete ataendelea kuwadanganya watanzania hadi kipindi chake kiishe? Wabunge wa CCM na wa upinzani wanaoliona tatizo bila kupindisha ukweli wapaswa kuendelea kushinikiza Kikwete awajibishwe na watu wake. Hakika ni wakati muafaka kumfurusha Kikwete na siyo kumpa fursa ya kuwatoa sadaka wenzake. Lao ni moja.

Elimu inapokuwa chanzo cha ujinga!


  1. Elimu ya Tanzania na Education for ignorance! Kweli hawa nao ni wasomi au makapi?



    Hilo ni bango mojawapo kati ya yale yaliyobebwa na wanaoitwa wasomi wa vyuo Tanzania! Inasikitisha licha ya kukera. Je hawa ni wasomi kweli au waganganjaa wanaoweza kutumiwa na fisadi yoyote awe mtu au chama kufikia malengo yake. Usomi maana yake ni uasi siyo ukondoo, ukuku wala upunda. Yaani hawa hawajui tatizo la CCM siyo wale wanaokihama bali walioking'ang'ania na ufisadi wake? Hivi kweli gamba ni yupi kati ya wale waliojazana CCM na wale wanaochoshwa na ufisadi na kuhama chama? Hawa wanafunzi wanamdanganya nani? Kwanini wasiseme wanaganga njaa? Ajabu makapi haya  yanapoanza kubwagwa na kuchomwa moto yanaanza kulalama! Acheni kutumia matumbo hata masabauri kufikiri. Tumieni vichwa vyenu vizuri.

Mjue bilionea asiyetaka makuu kama akina Ezekiel Maige


Common sense ingetumika tungeepuka uharibifu kiasi gani?


Askari wa Sudan akiwa ameshikilia silaha wakati wa mapambano baina ya Sudan ya Kusini na Sudan juu ya eneo la Heglig hivi karibuni.

Unaposhindwa kutofautisha Askof na mhuni mwingine wa kawaida!


Yesu alisema kuwa watakuja wachungaji  wengi  wa uongo na watapoteza wengi. Tanzania inaweza kuongoza kwa kuruhusu upuuzi unaoitwa madhehebu ya dini ambako matapeli wengi wamejipatia mradi toka kwa wajinga na maskini wengi waliotamalaki. Tubadilike na kuanza kuwapiga vita wezi hawa waliojifunika majoho ya dini. Mengine ukiyaangalia hata usoni unajua kabisa hili ni jambazi.Angalia mavazi yao, lugha zao, fasheni zao hata maisha yao utawajua.

Saturday, 28 April 2012



Baada ya kukaa pamoja kwa miaka saba na kufanya kila kitu kuanzia chumbani hadi bustanini na kupata watoto si haba eti Brad na Angelina ndiyo wametangaza uchumba! Wenye nazo kweli wana vituko. Hakuna kilichovuita blogu hii kama pete ya uchumba yenye thamani ya dola 500,000. Wenzetu wanazo lakini hawana uwezo wa kupata vitu tulivyopata bila hata kutumia senti tano kama ndoa na watoto wenye kuzaliwa ndani ya ndoa. Wao wana pesa sisi hatuna. Sisi tuna amani wao hawana. Maana wangekuwa na amani na kuaminiana isingewachukua miaka yote hiyo kuridhishana kuwa wanapaswa kuwa mme na mke. Kweli wahenga walisema kuwa pesa na ukwasi haviwezi kununua amani, upendo na ridhiko la moyo. Usishangae wawili katika ndoa kutoka kwenye ubavu wa mbwa wakicheka ilhali matajiri wakitoka kwenye hekalu na kasri wakilia hata kununiana. Binadamu ni nini hadi awe mtumwa wa vitu sifa vyeo ukwasi na kujilisha pepo?


China yazidi kuzinyanyasa nchi za magharibi kimaslahi


South Sudan President Salva Kiir and Chinese President Hu Jintao

Taarifa kuwa serikali ya Uchina imeridhia kutoa mkopo wa dola bilioni nane kwa Sudan ya Kusini ni pigo kwa nchi za magharibi. Taarifa iliyotolewa na serikali ya Sudan Kusini baada ya rais wake Salva Kiir Mayardit kuhitimisha ziara yake nchini Uchina ni kwamba Uchina imepania kuhakikisha Sudan ya Kusini inasimama kwa miguu yake. Kwa habari zaidi Bonyeza hapa.

Nini fundisho la mbunge kunusurika kichapo?


Taarifa zilizotufikia ni kwamba mbunge wa Geita Donald Kevin Max alinusurika kichapo baada ya kumtetea diwani fisadi wa kata ya Nkome. Wananchi walichukizwa na kitendo hiki kiasi cha kuamua kumpa kisago mbunge. Je tukio hili la kuondokewa woga kwa wananchi linatabiri na kutufundisha nini? Bila shaka wenye nchi yao wamechoka kugeuzwa shamba la bibi kana kwamba wao ni mataahira. Wahusika tieni akilini mambo yanaanza kubadilika na hakuna kisichobadilika. Walatini husema,Omnia mutantur nos et mutamur in illis yaani kila jambo hubadilika hivyo nasi tubadilike. Ubabaishaji, usanii na kulindana havina nafasi tena katika jamii ya sasa inayoanza kujitambua na kujikomboa.

Mjue mama mwenye mimba ya watoto tisa

Karla Vanessa Perez NueveMom Reveals Pregnancy with Nine Kids in Mexico
Karla Vanessa Perez anaingia kwenye vitabu vya historia kwa kuwa mmojawapo wa wanamama waliowahi kufanya kitu ambacho si kawaida-kubeba ujauzito wa watoto tisa wavulana watatu na wasichana sita. Kuibuka kwa hbari hii licha ya kuitangaza nchi yake ya Mexico umeiacha dunia kwenye mshangao. Kwa habari zaidi Bonyeza hapa.

Mheshimwa anapoangua kilio



Wengi wameshangaa ni kwanini mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alilia aliposikia kuwa ameshinda kesi ya kupinga ubunge wake iliyiokuwa ikimkabili. Tunadhani alilia kuonyesha ambavyo hakuwa na imani na mahakama zetu hasa kutokana na jinai iliyotendeka Arusha ambapo mtu aliyedaiwa kukashifiwa alishinda hata bila kufika mahakamani. Hii ni kinyume na sheria ya kashfa. Kitu kingine ni kwamba kwa majaji hawa wa kupeana na kulipana fadhila, yeyote angelia. Bwana Lissu hongera kwa kuvuka kikwazo hasa ikizingatiwa kuwa wewe ni mwiba kwa magamba na mafisadi. Alluta Continua.

Mjue Osama bin Laden wa kizungu


  • Al'Qa...  Adolf Hit...Caligula

Andre Behring Brevik ni kijana mdogo wa  Norway lakini mhafidhina, katili, bazazi na mjinga. Brevik amekuwa maarufu kutokana na kuwaua watu wapatao 69 wengi wakiwa vijana waliokuwa kwenye kambi kwenye kisiwa cha Utoya tarehe 22 Julai 2011.  Muuaji huyu hajutii wala kuona kama alichofanya ni kosa. Kwetu sisi, kutokana na kasumba alizolishwa kupitia michezo ya runinga, hana tofauti na gaidi Osama bin Laden. Hawa wawili wanafanana kutokana na ukweli kuwa wote ni watetezi wa dini na imani zao kwa kutumia maangamizi bila kuangalia hata upande wa pili.Wawili hawa wana sifa zinazofanana. Licha ya wote kuzaliwa kwenye familia zenye uwezo, wanachukia watu wasio wa dini zao. Wote hawajui historia za kile wanachokitetea kuwa ni matokeo ya dhuluma, ukoloni na ukandamizaji wa watu wengine. Wakati Osama aliwachukia wasio waislamu, Brevik anawachukia Waislamu na Wasoshalisti. Wote pamoja na bangi zao, hawakufanikiwa. Je Brevik angekuwa mwarabu vyombo vya magharibi vingesita kumuita gaidi tena mfuasi wa Al Qaeda? Wawili hawa hawana tofauti na wawili wengine waliotangulia yaani Adolf Hitler na Gaius Carigula.

Je wakuu wa EAC wataridhia upuuzi wa wabunge wao?




Hakuna kitu kilichotustua kama wabunge wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA) kujiingiza kwenye mjadala wa kijinga kuhusiana na watuhumiwa wa mauaji na vurugu za baada ya uchaguzi wa Kenya wa 2007. Bunge la Afrika Mashariki lilipitisha hoja ya kutaka eti Kenya iunde mahakama yake ya kuwashughulikia watuhumiwa wa nne wajulikanao kama Moreno Four. 
Kimsingi, wabunge wenye busara hawawezi kuanza kupingana na sheria za kimataifa tena kwa faida ya kikundi kidogo cha watu. Heri wabunge hao wangetumia fursa hiyo kupitisha sheria bora za uchaguzi ili kuondokana na uchakachuaji ambao ni chanzo cha upuuzi na mauaji ya Kenya. Je marais wote wa EAC wataingia mkenge wa Kenya na kujitia kwenye aibu ya kuanza kupambana na ICC jambo ambalo ni sawa na kutwanga maji?

Friday, 27 April 2012

Seriously, natafuta mwekezaji anunue ikulu

Image Detail
Kama mtanzania ninayeambiwa nina haki juu ya nchi yangu, nimeona heri nibinafsishe ikulu yetu kwa vile imegeuka yao na haiingizi faida. Nafanya hivyo baada ya kusikia maoni ya gwiji la uwekezaji Benjamin Mkapa aliyesema kuwa waliamua kubinafsisha mali za umma kwa vile zilikuwa haziingizi faida zaidi ya hasara. Hivyo nami naona tuanze na ikulu kwa vile, licha ya kuwa chaka la mafisadi, imekuwa ikiliingizia taifa hasara  hasa kutokana na wakazi wa mle kufanya watakavyo bila kuguswa. Wanapenda sana matumizi makubwa na kuzurura hata bila kujipa nafasi ya kufikiri na kufanya kazi yoyote zaidi ya uharibifu. Hivyo natangaza rasmi kuwa kama mtanzania nataka nipewe haki yangu ambayo ni  kubinafsisha ikulu ilil angalau tupate watu wenye akili ili tutie akili.

Taarifa ya Kamati Kuu ya CCM changa jingine la macho


Balozi mpya wa Tanzania nchini Ubelgiji Diodorus Kamala akiongea na Rais Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam wakati balozi huyo alipokwenda kumuaga.
Taarifa iliyotolewa kuhusiana kikao cha dharura cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yaweza kuwa usanii mwingine kama ukiisoma kipengele baada ya kingine. Kwa ufupi ni kwamba eti Kamati imeridhia shinikizo la wabunge kutaka kuwawajibisha mawaziri mafisadi. Ajabu taarifa hiyo haitoi muda wa utekelezaji wa hatua hii muhimu! Pili Kamati inaposema eti utekelezaji ufanywe mapema iwezekanavyo inamaanisha nini? Ajabu Kamati kuu haijapendekeza wahusika kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria. Kutofanya hivyo ni sawa na kuwakingia kifua wahusika.Kimsingi, hata kama Kikwete atafanya mabadiliko ya baraza la mawaziri, kuna mambo makuu mawili au matatu yatajitokeza. Mosi, ataondoa uoza na kuweka uoza maana CCM yote imeoza. Pili atawarudufu (recycle) makapi yaliyotajwa kwa kuwapa nafasi nyingine nono kama vile ubalozi kama alivyofanya kwa aliyekuwa katibu mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii, Ladislaus Komba ambaye alimteua balozi nchini Uganda au akina Adadi  Rajabu ambaye ni balozi Zimbabwe pamoja na kuvurunda kote.
Jikumbushe makapi aliyorudufu rais. Diodrous Kamala, Dk. Batilda Burian, Philip Marmona Mwantumu Mahiza. Hapa hujagusia watuhumiwa wegine wa ufisadi kama Mwanaidi Majaar balozi wa Tanzania nchini Marekani au Peter Noni, mkuu wa Benki ya Uwekezaji (TIB) ambao wanajulikana wazi wazi walivyoshiriki kwenye wizi wa EPA iliyomwezesha kuingia madarakani kwa njia ya rushwa na uchakachuaji mkubwa.
The Tanzanian ambassador to the U.S. talks about how increasing economic ties could benefit both countries. -

Kamati Kuu iliyokutana leo tarehe 27/04/2012 chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete Jijini Dar es salaam, pamoja na mambo mengine imefanya yafuatayo.;

A. UTEUZI
Kamati Kuu imeteua wafuatao kuwa makaimu Katibu wa mikoa. Vituo vyao vya kazi vitapangwa baadae. Uteuzi huu unatokana na kuwepo kwa mikoa wazi mitano, mikoa hiyo ni;

Geita
Njombe
Simiyu
Katavi
Magharibi
Hivyo wafuatao wameteuliwa kuwa makaimu katibu wa CCM wa Mikoa.

1. Ndg. Hilda Kapaya
2. Ndg. Shaibu Akwilombe
3. Ndg. Hosea Mpangile
4. Ndg. Alphonce Kinamhala
5. Ndg. Aziz Ramadhani Mapuri

B. HALI YA KISIASA:
Rais amepokea taarifa na maazimio ya Kamati ya wabunge wa CCM na Kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM juu ya kilichotokea kwenye bunge lililopita mjini Dodoma.

Taarifa hizo zimewasilishwa kwenye kamati kuu na kujadiliwa. Pamoja na taarifa hizo kamati Kuu imepokea taarifa ya jinsi Rais alivyojipanga kuchukua hatua za kuwawajibisha mawaziri na watendaji wa serikali na wale wa mashirika ya umma waliobainika kuhusika na ubadhirifu ulioinishwa na taarifa ya Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali, Kamati za kudumu za bunge na wabunge bungeni.

Kamati Kuu imeamua yafuatayo;
1. Kamati Kuu inatambua na kuheshimu haki na wajibu wa wabunge kujadili utendaji wa serikali yao.Inapongeza juhudi za serikali kuhakikisha kuwa ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali inajadiliwa kwa uwazi na hivyo kuibua mapungufu yaliyojadiliwa.

2. Kamati Kuu imeridhika na imebariki uamuzi wa Rais KULISUKA UPYA BARAZA LA MAWAZIRI na taasisi zingine zilizoanishwa katika ripoti hizo. Imesisitiza utekelezaji wa uamuzi huo ufanywe mapema iwezekanavyo.

Aidha kamati Kuu imeipongeza Kamati Teule ya baraza la wawakilishi Zanzibar iliyoundwa kuchunguza utendaji katika sekta mbalimbali kwenye serikali ya mapinduzi Zanzibar kwa taarifa yao.

Kamati Kuu inawapongeza wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa jinsi walivyojadili taarifa hiyo na pia Kamati Kuu inaipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuipokea taarifa na kuanza kuifanyia kazi.


Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
The Ideology and Publicity Secretary

Rais Banda amfurusha Mutharika


Malawi's new President Joyce Banda at a press conference on 10 April 2012 in Lilongwepeter_mut...



Baada ya mazishi ya aliyekuwa rais wa Malawi, Bingu wa Mutharika, Rais Joyce Banda wa Malawi amemwachisha kazi waziri wa mambo ya nchi za nje Peter Mutharika. Wengi wanasema Banda anaanza kuwang'oa watu wote waliowekwa na mtangulizi wake kwa maslahi binafsi badala ya taifa. Hata hivyo, pamoja na kuondoka kwa mdogo wa rais, Banda amemteua mtoto wa rais wa zamani Bakili Muluzu, Atupele kuwa waziri wa mipango na maendeleo.

Tumpongeze Maige kabla ya kumsulubu



  • Tell Tale...

Taarifa ya kufumka siri za utajiri wa kutisha wa waziri kijana wa Maliasili na Utalii Ezekiel Maige zinapaswa kutufanya tumpende na ikiwezekana tumsaidie kumfikisha mbele ya vyombo husika ingawa vyombo vyenyewe vinatia shaka.
Kwanza, Tanzania ina akina Maige wengi kiasi cha kushindwa hata kujua idadi yao. Tuwape mfano, hao vijana wengi mnaowaona Mipakani, Viwanja vya ndege, Uhamiaji, Benki kuu, Bandari, mita za mafuta na kwingineko ni akina Maige sema hawajafichuliwa.
Pili akina Maige wana wazazi wao waliowatengeneza. Hawako peke yao hawa. Wanaweza kufanya kila watakalo kuuza wanyama, unga, madini hata watanzania na hakuna anayewagusa. Hii ndiyo siri ya kila kitu nchini kujiendea bila yeyote kujali hasa uhujumu na ufisadi.
Kama vijana kama Maige wana ukwasi kiasi hicho, hao baba zao wana ukwasi kiasi gani? Hapa hatujaongelea wale wageni wetu akina Chavda ambao Idd Simba aliwahi kusema kumi tu wanamilki uchumi wa Tanzania. Kimsingi hao ndiyo wenye fweza maana akina Maige ni vijikuadi na limbukeni vinavyohongwa kupitisha mizigo na mambo ya wakubwa wenyewe.  Tumpongeze Maige kabla ya kumsulubu.

Thursday, 26 April 2012

Kuna siku tutataifisha haya mahekalu haki ya nani


Taarifa kuwa waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige alinunua nyumba kwa zaidi ya shilingi bilioni moja licha ya kuwastua wananchi na kuwachukiza, ni pigo kwa tambo za rais Jakaya Kikwete kuwa atawaletea maisha bora kwa watanzania wakati kumbe watanzania wenye aliomaanisha ni akina Maige na wateule wake! Ila amini msiamini kuna siku haya majumba tutayataifisha pale wahusika wakishindwa kutuambia walikopata hayo mabilioni ndani ya muda mfupi.  Kama nyumba ya Bwana Maige ni ya mabilioni hiyo akaunti yake ina matrilioni mangapi? Hapa hatujaona yale mahekalu yaliyoporomoshwa baada ya Benjamin Mkapa na wenzake kuiba nyumba zetu.
 Hivi hawa watu ni wazima kiakili au vichaa wasiosoma hata alama za nyakati? Huu ni ujambazi wa mchana kwa kijana mdogo aliyechaguliwa juzi kuwa mbunge kuweza kuwa na ukwasi kiasi hiki. Je hawa siyo wale wanaopata pesa tokana na kuuza wanyama wetu hata kuuza madawa ya kulevya? Anayebisha ajitokeze atwambie amepataje hayo mabilioni. Je rais Jakaya Kikwete anayewafumbia macho ana maslahi gani na jinai hii? Kweli chanzo cha umaskini wa watanzania si mapenzi ya Mungu bali ya mwandamu na mwanadamu mwenyewe mmojawapo ni Kikwete!Image Detail
Nyumba ya waziri Ezekiel Maige inayodaiwa kununuliwa kwa dola 700,000 huko kwa walio nazo.

Linganisha hizo picha mbili uniambie umegundua nini.


Habari kamili  kuhusiana na picha hii BONYEZA HAPA.
Image Detail
Rais anapopiga picha na model na rais anapopiga picha na mwanafunzi. Je tafsiri yaweza kuwa aliyepiga na model anathamini sana usanii na yule aliyepiga picha na mwanafunzi anathimini elimu? Wewe unasemaje?

Wakubwa kutembea na dola ni fasheni?


Pichani ni Kikwembe (juu) na Malima (chini)
Baada ya waziri mdogo wa Nishati na Madini, Adam Malima kukiri kuibiwa vitu mbalimbali hotelini mjini Morogoro hivi karibuni, hakuna kilichovuta hisia kama kumilki bunduki mbili na pesa za kigeni dola 4,000. Wengi walijiuliza dola za nini ndani ya nchi? Jana mjini Dodoma kwa mara nyingine mbunge mmoja aitwaye Prudensiana Kikwembe aliibiwa kadi za benki na pesa taslimu dola 600 na shilingi 180,000. Je inakuwaje wakubwa wahusudu kutumia dola huku wakimomonyoa sarafu yetu? Je hiki ndicho chanzo cha kuendelea kushuhudia shilingi yetu ikiporomoka bila ya wakubwa kujali kwa vile wana uwezo wa kujipatia dola kwa njia wajuazo ziwe halali au haramu?

Taylor bai Gbagbo Bashir na Moreno 4 kazi kwenu

Former Liberian President Charles Taylor looks down in the courtroom of the Special Court for Sierra Leone in The Hague
william r...Uhuru Ken...


Francis M...Image Detail
Kupatikana na hatia kwa aliyekuwa rais wa Liberia aliyesababisha umwagaji damu sana Charles Taylor ni ujumbe kwa watuhumiwa wengine. Inafurahisha kuona kuwa tuna mfumo wa kuweza kuwaadhibu wakubwa waliotumia madaraka vibaya. Kuna haya ya kuwa na mahakama ya ufisadi ili kuwashikisha adabu wezi wengi barani Afrika. Kupatikana na hatia kwa Taylor ni ujumbe kwa akina Laurent Gbagbo, Omar Bashir, Uhuru Kenyatta, William Ruto na Francis Muthaura. Angalau haki imetendeka kwa watu wa Liberia na majirani zake.

Wednesday, 25 April 2012

Mmeigeuza Tanzania nchi ya majambazi?

Mkurugenzi wa Uendeshaji Biashara wa NHC, Shambwe na  Meneja Uhusiano wa NHC Sanguya wakizindua utapeli wa nyumba kuuza nyumba za Ubungo mwaka 2011..
Hakuna kitu kimetutisha na kutushangaza kama tangazo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) la kuuza nyumba maeneo ya Ilala. Ukiangalia tangazo mwanzoni ni zuri tu. Lakini ukifikia kwenye kipengee cha bei ya nyumba zinazoitwa za watu wa kawaida, unapata kichefuchefu.  Bila aibu wanasema eti nyumba moja ni shilingi 168,239,748.62 tena bila VAT! Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uendeshaji Biashara, David Shambwe, hiyo ndiyo eti bei wanayoona inamfaa mwananchi wa kawaida!  Ukifanya hesabu ya haraka ni kwamba ili mfanyakazi au mkulima kununua nyumba moja anapaswa kufanya kazi kwa miaka 35 akiwa anapokea mshahara wa shilingi 400,578.83 kwa mwezi. Na kama anapata kiwango hicho cha mshahara ahakikishe hatumii hata senti tano ndipo aweze kuwa na kiwango kinachotakiwa. Utakaposhangaa nusu ya kufa ni pale utakapogundua kuwa wengi wa watakaonunua nyumba hizi tena bila kukopa benki kuwa vijana ambao hawajafikia hata miaka 50. Je ni watanzania wangapi wa kawaida wanapata mshahara kiasi hicho? Shame on you! Hivi kweli watu wa kawaida ambao karibu kwa maisha yao wengi wao walikuwa wajamaa haya mamilioni ya shilingi wayatoe wapi kama siyo kufanya ujambazi na ufisadi? Je hii ni biashara au ni aina nyingine ya wakubwa kutumia cha biashara kuhalalisha pesa yao chafu? Haiwezekani mtu wa kawaida mkulima na mfanyakazi akapata hiyo pesa bila kuwapo jinai nyuma yake. Je namna hii siyo kuigeuza Tanzania nchi ya majambazi na wauza unga? Ajabu hata serikali nayo inachekelea wakati hii ni taarifa kuwa asiyeliibia taifa au kujihusisha na biashara haramu alie tu hatapata kuwa na nyumba kwenye maeneo yaliyopimwa na yanaoyoeleweka.

Taifa linaomba eti lahitaji kuombewa!


Wanohitaji kuombewa wawezaje kuliombea taifa?





Je tatizo ni maombi au maadili?
Je kuomba ni jibu au sehemu ya tatizo?
Kura tunaomba
Misaada tunaomba
Haki tunaomba
Kila kitu tunaomba
Kweli sisi ombaomba. 
Kwa sasa wamejitokeza matapeli wengi wanaotaka kuwa karibu na watawala ili wafaidi mabaki ya ufisadi. Hawa si wengine bali wale wanaojiita viongozi wa dini wanaojua fika tatizo la nchi yetu kuwa ufisadi lakini wanalikwepa na kusema ni laana! Maana unaposema nchi inapaswa kuombewa badala ya kuambiwa ukweli kuwa utawala uliopo hauna visheni na ni wa hovyo, unamaanisha nchi yetu imelaaniwa. Kuna haja ya kuwaogopa hawa kama ukoma. maana nao ni sehemu ya tatizo. Tanzania aihitaji kuombewa bali kuwajibika na kutenda haki. Badala ya kuombea nchi shinikizeni watawala waache ufisadi na usanii.